Yesu Ajaribiwa Na Shetani

Kisha Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa hadi jangwani. Alikaa huko jangwani siku arobaini akijaribiwa na shetani. Siku zote hizo hakula cho chote , kwa hiyo baada ya muda huo aliona njaa.

Shetani akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”

Yesu akamjibu, “Imeandikwa katika maandiko, ‘mtu haishi kwa chakula tu.’ ”

Kisha shetani akamchukua hadi juu ya mlima mrefu akamwo nyesha kwa mara moja milki zote za dunia. 6-7 Akamwambia, “Uki piga magoti na kuniabudu, nitakupa uwezo juu ya milki zote hizi na fahari yake; maana ni zangu na ninaweza kumpa ye yote nita kaye.” Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.’ ”

9-11 Ndipo shetani akamfikisha Yerusalemu, akampand isha juu ya mnara wa Hekalu, akamwambia: “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kwani imeandikwa, ‘Mungu ataamrisha mal aika wake wakulinde

12 Yesu akamwambia, “Pia imeandikwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”

Mungu wako.’ ”

13 Basi Shetani alipomaliza majaribu yote, akamwacha Yesu kwa muda.

Yesu Ahubiri Galilaya

14 Kisha Yesu akarudi Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu. Habari zake zikaenea katika sehemu zote za wilaya ile. 15 Alifundisha katika masinagogi yao na wote wakamsifu.

Yesu Akataliwa Na Watu Wa Nazareti

16 Baadaye Yesu akaenda Nazareti, mahali alipokulia. Siku ya sabato alikwenda katika sinagogi kama kawaida yake. Akasimama ili asome Maandiko. 17 Akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifun gua mahali palipoandikwa: 18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu. Amenichagua kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatan gazia wafungwa kuwa wako huru, kuwaambia vipofu kuwa wanaweza kuona tena; na kuwaweka huru wanaoonewa, na nitangaze mwaka ambao Bwana atawabariki watu wake.” 20 Akakifunga kitabu, akamrud ishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 Ndipo akasema: “Maandiko haya mliyosikia nikisoma, leo yametimia.”

22 Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake mazuri, wakaulizana, “Je, huyu si yule mtoto wa Yusufu?” 23 Lakini akawajibu, “Bila shaka mtaniambia, ‘Daktari, jiponye! Mbona hutendi hapa kijijini kwako miujiza tuliyosikia kuwa umeifanya kule Kapernaumu?’ 24 Ningependa mfahamu ya kwamba hakuna nabii anayekubaliwa na watu kijijini kwake. 25 Nawahakik ishieni kwamba walikuwepo wajane wengi katika Israeli wakati wa Eliya, mvua ilipoacha kunyesha kwa miaka mitatu na nusu, pakawepo na njaa kuu nchi nzima. 26 Lakini Eliya hakutumwa kumwokoa hata mmojawapo wa hawa wajane, isipokuwa alitumwa kwa mjane mmoja wa kijiji cha Sarepta katika nchi ya Sidoni. 27 Na pia wakati wa nabii Elisha, walikuwepo wakoma wengi katika Israeli; lakini hakumtakasa hata mmoja wao, ila Naamani ambaye alikuwa raia wa Siria.”

Siria.”

28 Watu wote katika sinagogi waliposikia maneno haya, waka kasirika sana. 29 Wakasimama wote wakamtoa nje ya mji hadi kwe nye kilele cha mlima ambapo mji huo ulijengwa ili wamtupe chini kwenye mteremko mkali. 30 Lakini yeye akapita katikati yao akaenda zake. Yesu Afukuza Pepo Mchafu

31 Kisha akaenda Kapernaumu, mji ulioko wilaya ya Galilaya, na siku ya sabato akawafundisha watu katika sinagogi. 32 Walis taajabishwa na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka. 33 Alikuwepo mtu mmoja katika sinagogi aliyekuwa ame pagawa na pepo mchafu, naye alianza kupiga kelele kwa nguvu akisema, 34 “Unataka kutufanya nini, Wewe Yesu wa Nazareti? Ume kuja kutuangamiza? Nakufahamu wewe ni nani. Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.” 35 Yesu akamwamuru yule pepo: “Nyamaza! Mtoke!” Yule pepo akamwangusha chini yule mtu mbele yao, akamtoka pasipo kumd huru. 36 Watu wote wakashangaa wakaambiana, “Mafundisho ya mtu huyu ni ya ajabu. Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka! 37 Habari zake zikaenea pote katika mkoa ule.

Yesu Awaponya Wengi

38 Alipotoka katika sinagogi Yesu alikwenda nyumbani kwa Simoni na alipofika huko alimkuta mama mkwe wa Simoni ana homa kali. Wakamwomba sana amponye. 39 Basi Yesu akasimama kando ya kitanda chake akaiamuru ile homa imtoke. Homa ikamtoka yule mama. Akaamka mara moja akaanza kuwahudumia. 40 Jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwa Yesu. Akamgusa kila mgonjwa, akawaponya wote. 41 Pepo wachafu pia waliwatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walifahamu kuwa yeye ni Kristo.

42 Kesho yake, kulipopambazuka, Yesu alikwenda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, na walipom wona wakajaribu kumzuia asiondoke. 43 Lakini yeye akawaambia, “Ninao wajibu wa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu sehemu nyingine pia. Hii ndio sababu nilitumwa.” 44 Kwa hiyo akaende lea kuhubiri katika masinagogi ya Yudea. Yesu Awachagua Wanafunzi Wa Kwanza

Yesu Ajaribiwa na Shetani

(Mt 4:1-11; Mk 1:12-13)

Akiwa amejaa Roho Mtakatifu, Yesu akarudi kutoka Mto Yordani. Kisha Roho Mtakatifu akamwongoza mpaka nyikani kwa muda wa siku arobaini, alikojaribiwa na Ibilisi. Katika muda wote huo hakula chakula chochote na baadaye akahisi njaa sana.

Ibilisi akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.”

Yesu akamjibu, “Maandiko yanasema, ‘Watu hawataishi kwa mkate tu.’”(A)

Kisha mwovu akamchukua Yesu na kwa muda mfupi akamwonyesha falme zote za ulimwengu. Mwovu akamwambia, “Nitakufanya uwe mfalme wa sehemu zote hizi. Utakuwa na mamlaka juu yao, na utapata utukufu wote. Yote yametolewa kwangu. Ninaweza kumpa yeyote kadri ninavyopenda. Nitakupa vyote hivi, ikiwa utaniabudu tu.”

Yesu akajibu, “Maandiko yanasema, ‘Ni lazima umwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’”(B)

Ndipo Shetani akamwongoza Yesu mpaka Yerusalemu na kumweka mahali palipo juu katika mnara wa Hekalu. Akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe! 10 Kwani Maandiko yanasema,

‘Mungu atawaamuru
    malaika zake wakulinde.’(C)

11 Pia imeandikwa kuwa,

‘Mikono yao itakudaka,
    ili usijikwae mguu wako kwenye mwamba.’”(D)

12 Yesu akajibu, “Pia, Maandiko yanasema: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”(E)

13 Shetani alipomaliza kumjaribu Yesu katika namna zote, alimwacha akaenda zake hadi wakati mwingine.

Yesu Aanza Kazi yake Galilaya

(Mt 4:12-17; Mk 1:14-15)

14 Yesu alirudi Galilaya akiwa na nguvu za Roho Mtakatifu. Habari zake zilisambaa katika eneo lote lililozunguka Galilaya. 15 Alianza kufundisha katika masinagogi na kila mtu alimsifu.

Yesu Aenda Kwenye Mji wa Kwao

(Mt 13:53-58; Mk 6:1-6)

16 Yesu alisafiri akaenda katika mji aliokulia wa Nazareti. Siku ya Sabato alikwenda kwenye sinagogi kama alivyokuwa akifanya. Alisimama ili asome. 17 Akapewa gombo la nabii Isaya. Akalivingirisha kulifungua na akapata mahali palipoandikwa haya:

18 “Roho wa Bwana yu juu yangu,
    amenichagua ili
    niwahubiri maskini habari njema.
Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao
    na kuwaambia wasiyeona
    kuwa wanaweza kuona tena.
Amenituma kuwapa uhuru wale wanaoteswa
19     na kutangaza kuwa wakati wa Bwana
    kuonesha wema wake umefika.”(F)

20 Yesu akalivingirisha gombo akalifunga, akalirudisha kwa msaidizi na kuketi chini. Kwa kuwa kila mtu ndani ya sinagogi alimwangalia kwa makini, 21 Alianza kuzungumza nao. Akasema, “Maandiko haya yametimilika mlipokuwa mnanisikia nikiyasoma!”

22 Kila mtu pale akasema alipenda namna ambavyo Yesu alizungumza. Walishangaa kumsikia akisema maneno haya ya ajabu. Wakaulizana, “Inawezekanaje? Huyu si mwana wa Yusufu?”

23 Yesu akawaambia, “Ninafahamu mtaniambia mithali hii ya zamani: ‘Daktari, jitibu mwenyewe.’ Mnataka kusema ‘Tulisikia mambo yote uliyotenda Kapernaumu. Yatende pia hapa katika mji wako mwenyewe!’” 24 Lakini Yesu akasema, “Ukweli ni huu, nabii hakubaliki katika mji wa kwao.

25-26 Wakati wa Eliya mvua haikunyesha katika Israeli kwa miaka mitatu na nusu. Chakula hakikuwepo mahali popote katika nchi yote. Palikuwa wajane wengi katika Israeli wakati huo. Lakini Eliya hakutumwa kwenda kwa mmoja wa wajane waliokuwa katika Israeli bali kwa mjane aliyekuwa katika mji wa Sarepta, jirani na Sidoni.

27 Na, palikuwa wenye ugonjwa mbaya wa ngozi wengi walioishi katika Israeli wakati wa nabii Elisha, lakini hakuna aliyeponywa isipokuwa Naamani, aliyetoka katika nchi ya Shamu, siyo Israeli.”

28 Watu wote waliposikia hili, walikasirika sana. 29 Wakasimama na kumlazimisha Yesu atoke nje ya mji. Mji wao ulijengwa juu ya kilima. Wakamchukua Yesu mpaka ukingo wa kilima ili wamtupe. 30 Lakini alipita katikati yao na kwenda zake.

Yesu Amweka Huru Mtu Kutoka Pepo Mchafu

(Mk 1:21-28)

31 Yesu akashuka kwenda Kapernaumu, mji uliokuwa Galilaya. Siku ya Sabato aliwafundisha watu. 32 Nao walishangaa sana namna alivyokuwa akifundisha kwa sababu mafundisho yake yalikuwa na mamlaka.

33 Ndani ya sinagogi alikuwepo mtu aliyekuwa na roho chafu, kutoka kwa yule Mwovu, ndani yake. Akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, “Aiii! 34 Unataka nini kwetu Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninajua wewe ni nani; Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.” 35 Lakini Yesu akamkemea yule pepo na kumwambia, “Nyamaza kimya! Umtoke mtu huyu!” Ndipo pepo akamtupa yule mtu chini mbele ya watu, akamtoka bila kumjeruhi sehemu yoyote ya mwili wake.

36 Watu wakashangaa. Wakasemezana wao kwa wao, “Hii inamaanisha nini? Kwa mamlaka na uwezo anaamuru pepo wachafu na wanatoka!” 37 Hivyo habari kuhusu Yesu zikaenea kila mahali katika eneo lote.

Yesu Amponya Mkwewe Petro

(Mt 8:14-17; Mk 1:29-34)

38 Yesu akatoka katika sinagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni.[a] Mama mkwe wa Simoni alikuwa mgonjwa sana. Alikuwa na homa kali. Nao walimwomba Yesu amsaidie. 39 Yesu alisimama karibu yake na kuiamuru homa kuondoka. Homa ikamwacha, naye akasimama na kuanza kuwahudumia.

Yesu Aponya Wengine Wengi

40 Jua lilipokuchwa, watu wote waliwaleta kwa Yesu jamaa na rafiki zao walioumwa na wenye magonjwa mengi tofauti. Yesu aliweka mikono yake juu ya kila mgonjwa na kuwaponya wote. 41 Pepo nao waliwatoka watu wengi. Mapepo yalipiga kelele yakisema “Wewe ni Mwana wa Mungu.” Lakini Yesu alitoa amri yenye nguvu kwa mapepo yasiseme, kwa sababu yalijua alikuwa ni Masihi.

Yesu Aenda Katika Miji Mingine

(Mk 1:35-39)

42 Siku iliyofuata Yesu alijitenga na kwenda mahali ili awe peke yake. Watu wakawa wakimtafuta. Walipompata, walijaribu kumzuia asiondoke. 43 Lakini akawaambia, “Ni lazima nihubiri Habari Njema kuhusu Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, kwa sababu nilitumwa kufanya hivyo.”

44 Kisha Yesu akahubiri Habari Njema katika masinagogi ya Uyahudi.

Footnotes

  1. 4:38 Simoni Jina jingine la Simoni lilikuwa Petro. Pia katika 5:3,4,5,10.