Mfano Wa Mbegu

13 Siku hiyo hiyo Yesu alitoka nyumbani akaketi kando ya bahari. Umati mkubwa mno wa watu wakasongamana hata ikabidi aingie katika mashua akaketi humo; na wale watu wakakaa ukingoni mwa bahari. Kisha akawaambia mambo mengi kwa mifano, akasema: “Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. Alipokuwa akitawanya mbegu, baadhi zikaanguka njiani, ndege wakaja wakazila. Nyingine zikaanguka kwenye mawe, ambapo hapakuwa na udongo wa kutosha. Zikakua haraka kwa sababu udongo ulikuwa kidogo. Lakini jua kali lilipowaka, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikwenda chini. Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba. Miiba hiyo ikakua ikazisonga. Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri zikatoa mazao, nyingine mara mia moja zaidi ya mbegu zilizopandwa, nyingine mara sitini na nyingine mara the lathini. Mwenye nia ya kusikia na asikie.”

Sababu Ya Kufundisha Kwa Mifano

10 Wanafunzi wake wakamwendea wakamwuliza, “Kwa nini unazungumza na watu kwa mifano?” 11 Akawajibu, “Ninyi mmejal iwa kuzifahamu siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujal iwa. 12 Kwa maana mtu aliye na kitu ataongezewa mpaka awe navyo tele; lakini mtu asiye na kitu, hata kile alichonacho atany ang’anywa. 13 Hii ndio sababu nazungumza nao kwa mifano; wanata zama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawae lewi. 14 Hali yao inatimiza ule utabiri wa nabii Isaya ali posema:’Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa, na pia mtatazama lakini hamtaona. 15 Kwa maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kuelewa kwa mioyo yao, wakanigeukia, nami nikawaponya.’ 16 Lakini macho yenu yame barikiwa, kwa maana yanaona, na masikio yenu yamebarikiwa kwa maana yanasikia. 17 Nawaambieni kweli, manabii wengi na wenye haki walitamani kuona mnayoyaona, na hawakuyaona; na kusikia mnayosikia lakini hawakuyasikia.”

Maelezo Ya Mfano Wa Mbegu

18 “Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi aliyepanda mbegu. 19 Mtu anaposikia neno la Ufalme na asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake; hii ndio mbegu iliyopandwa njiani. 20 Mbegu iliyopandwa kwenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na kulipokea mara moja kwa furaha. 21 Lakini kwa kuwa hana mizizi ndani yake, neno hilo hukaa kwa muda mfupi; na inapotokea dhiki au mateso kwa ajili ya hilo neno, yeye mara moja huanguka. 22 Mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno na mahangaiko ya maisha haya na anasa za mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda. 23 Lakini mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika huzaa matunda, mara mia, au mara sitini, au mara thelathini zaidi ya mbegu iliyo pandwa.”

Mfano Wa Magugu

24 Yesu akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa mbi nguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. 25 Lakini watu walipokuwa wamelala, adui yake aka ja akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26 Ngano ilipoota na kuzaa, magugu nayo yakachipua.

27 “Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwul iza, ‘Bwana, si ulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Imekuwaje kuna magugu?’ 28 Akawajibu, ‘Adui ndiye amefanya jambo hili’. Wale watumishi wakamwuliza, ‘Sasa unataka tukayang’oe?’ 29 Lakini akasema, ‘Hapana msiyang’oe, kwa maana huenda katika kung’oa magugu mkang’oa na ngano pia. 30 Acheni ngano na magugu yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavu naji wayang’oe magugu kwanza wayafunge katika mafurushi tayari kwa kuchomwa moto, lakini wavune ngano na kuikusanya ghalani mwangu.’ ”

Mfano Wa Haradali

31 Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa mbinguni unafanana na punje ndogo ya haradali ambayo mtu aliichukua akaipa nda shambani mwake. 32 Ijapokuwa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua, mmea wake huwa mkubwa kuliko mimea yote bustanini; nao huwa mti mkubwa ambao ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”

Mfano Wa Chachu

33 Akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika vipimo vitatu vya unga mpaka wote ukaumuka.”

Sababu Ya Yesu Kutumia Mifano

34 Haya yote Yesu aliwaeleza umati wa watu kwa kutumia mifano. Na hakika hakuwaambia lo lote pasipo kutumia mfano. 35 Hii ilikuwa kutimiza utabiri wa nabii, kwamba, ‘Nitazungumza nao kwa mifano; nitatamka mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.’

Ufafanuzi Wa Mfano Wa Magugu

36 Kisha Yesu akaagana na huo umati wa watu, akaingia nyum bani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.”

37 Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni mimi Mwana wa Adamu. 38 Shamba ni ulimwengu, na mbegu nzuri ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu. 39 Yule adui aliyepanda magugu ni shetani. Mavuno ni mwisho wa ulimwengu; na wavunaji ni malaika. 40 Kama vile magugu yanavyong’olewa na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa ulimwengu. 41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika wake wang’oe kutoka katika Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote. 42 Nao wata watupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 43 Ndipo wenye haki watang’aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Mwenye nia ya kusikia, na asikie.”

Mfano Wa Hazina Iliyofichwa

44 “Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani ambayo mtu mmoja aliigundua akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akanu nua lile shamba.” 45 Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na mfanya biashara aliyekuwa akitafuta lulu safi, 46 ambaye alipo pata lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza vyote alivyo kuwa navyo akainunua.”

Mfano Wa Wavu

47 “Na tena Ufalme wa mbinguni ni kama wavu wa kuvulia samaki ambao ulitandazwa baharini ukakamata samaki wa kila aina. 48 Ulipojaa, wavuvi waliuvuta ukingoni, wakachagua samaki wazuri wakawaweka kwenye vyombo safi, lakini wale samaki wabaya wakawat upa.

49 “Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki. 50 Na watawatupa hao waovu katika tanuru ya moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 51 Je, mmeyaelewa haya yote?” Wakam jibu, “Ndio.” 52 Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka katika ghala yake mali mpya na mali ya zamani.”

Yesu Akataliwa Nazareti

53 Yesu alipomaliza kutoa mifano hii, aliondoka. 54 Alipo fika mji wa kwao, aliwafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza? 55 Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si anaitwa Mariamu, na ndugu zake ni Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake si wako hapa nasi? Amepata wapi basi mambo haya yote?” 57 Wakakataa kumpokea. Lakini Yesu aka waambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake na nyumbani kwake.”

58 Na hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.

Simulizi Kuhusu Mkulima Aliyepanda Mbegu

(Mk 4:1-9; Lk 8:4-8)

13 Siku hiyo hiyo Yesu alitoka nje ya nyumba na kukaa kando ya ziwa. Kundi kubwa wakakusanyika kumzunguka. Hivyo akapanda mtumbwini na kuketi. Watu wote wakabaki ufukweni. Kisha Yesu akatumia simulizi kuwafundisha mambo mengi. Akawaambia simulizi hii:

“Mkulima alitoka kwenda kupanda mbegu. Alipokuwa anatawanya mbegu, baadhi ziliangukia njiani. Ndege wakaja na kuzila zote. Mbegu zingine ziliangukia kwenye ardhi yenye mawe, ambako hakukuwa na udongo wa kutosha. Zikakua haraka pale, kwa sababu udongo haukuwa na kina. Lakini jua lilipowaka, likaichoma mimea. Mimea ikafa kwa sababu haikuwa na mizizi mirefu. Baadhi ya mbegu ziliangukia katikati ya miiba. Miiba ikakua na kusababisha mimea mizuri kuacha kukua. Lakini baadhi ya mbegu ziliangukia kwenye udongo wenye rutuba. Hapo zikakua na kuzaa nafaka. Baadhi ya mimea ikazaa nafaka mara mia zaidi, baadhi mara sitini na baadhi mara thelathini zaidi. Ninyi watu mnaoweza kunisikia, nisikilizeni!”

Kwa nini Yesu Alitumia Simulizi Kufundisha

(Mk 4:10-12; Lk 8:9-10)

10 Wafuasi wake wakamwendea Yesu na kumuuliza, “Kwa nini unatumia simulizi hizi kuwafundisha watu?”

11 Yesu akawajibu, “Mungu amewapa ninyi ujuzi wa kuelewa siri za ufalme wa Mungu, lakini hajawapa watu hawa wengine ujuzi huu. 12 Kisha akawaambia, ‘Zingatieni kwa makini kile mnachokisikia. Kwani jinsi mnavyosikiliza kwa makini, ndivyo mtakavyoelewa na kuzidi kuelewa. Kwa kuwa kila aliye na uelewa kidogo ataongezewa zaidi. Lakini wale wasiosikiliza kwa makini watapoteza hata ule uelewa mdogo walio nao.’ 13 Ndiyo sababu ninatumia simulizi hizi kuwafundisha watu: Wanaona, lakini hakika hawaoni. Wanasikia, lakini hakika hawasikii au kuelewa. 14 Hiyo inathibitisha alichosema nabii Isaya kuhusu wao kuwa kweli:

‘Ninyi watu mtasikia na kusikia,
    lakini hamtaelewa.
Mtatazama na kutazama,
    lakini hakika hamtaona.
15 Ndiyo, akili za watu hawa sasa zimefungwa.
    Wana masikio, lakini hawasikii vizuri.
Wana macho, lakini wameyafumba.
    Iwapo akili zao zisingekuwa zimefungwa,
wangeona kwa macho yao;
    wangesikia kwa masikio yao;
Iwapo wangeelewa kwa akili zao.
    Kisha wangenigeukia na kuponywa.’(A)

16 Bahati gani mliyonayo ninyi. Mnaelewa mnachokiona kwa macho yenu. Na mnaelewa mnachosikia kwa masikio yenu. 17 Ninaweza kuwathibitishia, manabii na watakatifu wengi walitaka kuona mnayoyaona. Lakini hawakuyaona. Walitaka kusikia mnayosikia sasa. Lakini hawakuyasikia.

Yesu Afafanua Simulizi Kuhusu Mbegu

(Mk 4:13-20; Lk 8:11-15)

18 Hivyo sikilizeni maana ya simulizi hiyo kuhusu mkulima:

19 Vipi kuhusu mbegu zilizoangukia njiani? Hizo zinafanana na watu wanaosikia mafundisho kuhusu ufalme wa Mungu lakini hawauelewi. Mwovu huja na kuyachukua yaliyopandwa katika mioyo yao.

20 Na vipi kuhusu mbegu zilizoangukia kwenye udongo wenye mawe? Hizo zinafanana na watu wanaosikia mafundisho haraka na kwa furaha huyapokea. 21 Lakini hawaruhusu mafundisho kutawala maisha yao. Huyatunza kwa muda mfupi. Mara tatizo au mateso yanapokuja kwa sababu ya mafundisho waliyoyapokea, wanaacha kuyafuata.

22 Na vipi kuhusu mbegu zilizoanguka katikati ya miiba? Hizo zinafanana na watu wanaosikia mafundisho lakini huyaruhusu mahangaiko ya maisha na kutaka utajiri, hufanya mafundisho yasikue. Hivyo mafundisho hayazai mazao mazuri katika maisha yao.

23 Lakini vipi kuhusu mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye rutuba? Hizo ni sawa na watu wanaosikia mafundisho na kuyaelewa. Hukua na kuzaa mazao mazuri, wakati mwingine mara mia, wakati mwingine mara sitini, na wakati mwingine mara thelathini zaidi.”

Simulizi Kuhusu Ngano na Magugu

24 Kisha Yesu akatumia simulizi nyingine kuwafundisha. Yesu akasema, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. 25 Usiku ule, kila mtu alipokuwa amelala, adui wa yule mtu akaja na kupanda magugu katikati ya ngano kisha akaondoka. 26 Baadaye, ngano ikakua na vichwa vya nafaka vikaota juu ya mimea. Kisha mtumishi akayaona magugu. 27 Watumwa wa mwenye shamba wakaja na akasema, ‘Bwana ulipanda mimea mizuri kwenye shamba lako. Magugu yametoka wapi?’

28 Yule mtu akajibu, ‘Adui alipanda magugu.’

Wale watumwa wakauliza, ‘Je, unataka twende na kung'oa magugu?’

29 Akajibu, ‘Hapana, kwa sababu mtakapokuwa mnang'oa magugu, mtaweza pia kung'oa ngano. 30 Yaacheni magugu na ngano vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati wa mavuno nitawaambia wafanyakazi hivi: Kwanza, yakusanyeni magugu na kuyafunga pamoja ili myachome. Kisha kusanyeni ngano na kuileta ghalani mwangu.’”

Simulizi Nyingine ya Ufalme

(Mk 4:30-34; Lk 13:18-21)

31 Kisha Yesu akawaambia watu simulizi nyingine: “Ufalme wa Mungu unafanana na mbegu ya mharadali ambayo mtu alipanda katika shamba lake. 32 Ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote. Lakini unapokua, ni kubwa kuliko mimea yote ya bustanini. Unakuwa mti mkubwa unaotosha ndege kuja na kutengeneza viota kwenye matawi yake.”

33 Kisha Yesu akawaambia simulizi nyingine: “Ufalme wa Mungu unafanana na chachu ambayo mwanamke huichanganya katika bakuli kubwa la unga ili atengeneze mkate. Chachu hufanya kinyunya chote kiumuke.”

34 Yesu alitumia simulizi akasema mambo yote haya kwa watu. Daima alitumia simulizi kuwafundisha. 35 Hii ilikuwa kuweka wazi maana halisi kama manabii walivyosema:

“Nitazungumza kwa kutumia simulizi;
    Nitayasema mambo ambayo yamekuwa siri
    tangu ulimwengu ulipoumbwa.”(B)

Yesu Afafanua Simulizi Kuhusu Magugu

36 Kisha Yesu akawaacha watu na kuingia katika nyumba. Wafuasi wake wakamwendea na akasema, “Tufafanulie maana ya simulizi kuhusu magugu ndani ya shamba.”

37 Akajibu, “Mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba ni Mwana wa Adamu. 38 Shamba ni ulimwengu. Mbegu nzuri ni watoto katika ufalme wa Mungu. Magugu ni watu wa Yule Mwovu. 39 Na adui aliyepanda mbegu mbaya ni ibilisi. Mwisho wa nyakati ndiyo wakati wa mavuno. Wafanyakazi wanaokusanya ni malaika wa Mungu.

40 Magugu hung'olewa na kuchomwa motoni. Itakuwa vivyo hivyo nyakati za mwisho. 41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watawatafuta watu wanaosababisha dhambi na wale wote watendao maovu. Malaika watawatoa watu hao katika ufalme wa Mungu. 42 Watawatupia katika tanuru la moto. Huko watu watakuwa wakilia na kusaga meno kwa maumivu. 43 Kisha wenye haki watang'aa kama jua. Watakuwa katika ufalme wa baba yao. Ninyi watu, mlio na masikio, sikilizeni!

Simulizi Kuhusu Hazina na Lulu

44 Ufalme wa Mungu unafanana na hazina iliyofichwa shambani. Siku moja mtu alipoiona aliificha tena; na kwa sababu alikuwa na furaha sana alikwenda kuuza kila kitu alichonacho na kulinunua shamba.

45 Pia, ufalme wa Mungu unafanana na mchuuzi anayetafuta lulu safi. 46 Siku moja alipoipata, alikwenda na akauza kila kitu alichokuwa nacho ili kuinunua.

Simulizi Kuhusu Wavu wa Kuvulia Samaki

47 Pia, ufalme wa Mungu unafanana na nyavu kubwa iliyowekwa katika ziwa. Nyavu ile ikavua aina nyingi tofauti ya samaki. 48 Ikajaa, hivyo wavuvi wakaivuta mpaka pwani. Wakakaa chini na kutoa samaki wote wazuri na kuwaweka kwenye kikapu. Kisha wakawatupa samaki wabaya. 49 Itakuwa hivyo wakati wa mwisho. Malaika watakuja na kuwatenganisha waovu na watakatifu. 50 Watawatupa waovu katika tanuru la moto. Huko watu watalia na kusaga meno yao kwa sababu ya maumivu.”

51 Kisha Yesu akawauliza wafuasi wake, “Mnaelewa mambo yote haya?”

Wakasema, “Ndiyo, tunaelewa.”

52 Kisha Yesu akawaambia wafuasi wake, “Hivyo kila mwalimu wa sheria aliyejifunza kuhusu ufalme wa Mungu ana baadhi ya vitu vizuri vya kufundisha. Ni kama mmiliki wa nyumba, aliye na vitu vipya na vya zamani nyumbani mwake. Na huvitoa nje vipya na vya zamani.”

Yesu Aenda Kwenye Mji wa Kwao

(Mk 6:1-6; Lk 4:16-30)

53 Yesu alipomaliza kufundisha kwa simulizi hizi, aliondoka pale. 54 Alikwenda katika mji wa kwao. Aliwafundisha watu katika sinagogi lao, nao walishangaa. Walisema, “Mtu huyu alipata wapi hekima na nguvu hii ya kutenda miujiza? 55 Je, yeye si mwana wa seremala tunayemfahamu? Je, jina la mamaye si Mariamu na wadogo zake ni Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake bado wanaishi hapa katika mji huu? Anawezaje kutenda mambo haya?” 57 Hivyo wakawa na mashaka kumpokea.

Lakini Yesu akawaambia, “Watu kila mahali huwaheshimu manabii, lakini katika mji wake au katika nyumba yake nabii hapati heshima yoyote.” 58 Yesu hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu watu hawakumwamini.