Add parallel Print Page Options

Simulizi Nyingine ya Ufalme

(Mt 13:31-33; Mk 4:30-32)

18 Kisha Yesu akasema, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Niufananishe na nini? 19 Ufalme wa Mungu ni kama mbegu ya haradali. Mtu mmoja aliichukua na kuipanda katika bustani yake. Mbegu ikaota, ikakua na kuwa mti na ndege wakatengeneza viota kwenye matawi yake.”

20 Yesu akasema tena, “Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? 21 Ufalme wa Mungu unafanana na kiasi kidogo cha chachu ambacho mwanamke hutumia kuchanganya na kilo 20 za unga kutengeneza mkate. Hamira huumua kinyunya[a] chote.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 13:21 kinyunya Mchanganyiko wa unga wa ngano na maji Ulio tayari kwa ajili ya kutengeneza mikate.