23 Wote waliokuwepo katika Baraza wakasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. Wakafungua mashtaka yao kwa kusema: “Tumem wona huyu mtu akipotosha taifa letu. Yeye anawaambia watu wasi lipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.” Basi Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamjibu, “Ni kama ulivyosema.” Pilato akawaambia maku hani wakuu na watu wote waliokuwapo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki huyu mtu!” Lakini wao wakakazana kusema, “Anawa chochea watu kwa mafundisho yake katika Yudea yote. Alianzia huko

Yesu Apelekwa Kwa Herode

Pilato aliposikia hayo akauliza, ‘Huyu mtu ni Mgalilaya?” Alipofahamu kwamba Yesu alitoka katika mkoa unaotawaliwa na Herode, akampeleka kwa Herode ambaye wakati huo alikuwa Yerus alemu. Herode alifurahi sana kumwona Yesu. Alikuwa amesikia habari zake na kwa muda mrefu akatamani sana kumwona; na pia alitegemea kumwona Yesu akifanya mwujiza. Kwa hiyo akamwuliza Yesu maswali mengi, lakini yeye hakumjibu neno. 10 Wakati huo, makuhani wakuu na walimu wa sheria walikuwepo wakitoa mashtaka yao kwa nguvu sana. 11 Herode na maaskari wake wakamkashifu Yesu na kumzomea. Wakamvika vazi la kifahari, wakamrudisha kwa Pilato. 12 Siku hiyo, Herode na Pilato, ambao kabla ya hapo walikuwa maadui, wakawa marafiki.

Yesu Ahukumiwa Kifo

13 Pilato akawaita makuhani wakuu, viongozi na watu 14 aka waambia, “Mmemleta huyu mtu kwangu mkamshtaki kuwa anataka kuwa potosha watu. Nimemhoji mbele yenu, na sikuona kuwa ana hatia kutokana na mashtaka mliyoleta. 15 Hata Herode hakumwona na kosa lo lote; ndio sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lo lote linalostahili adhabu ya kifo. 16 Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko, kisha nimwachilie.” [ 17 Kwa kawaida, kila sikukuu ya Pasaka ilimlazimu Pilato kuwafungulia mfungwa mmoja].

18 Watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “ Auawe huyo! Tufungulie Baraba!” 19 Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini. 20 Pilato ali taka sana kumwachilia Yesu kwa hiyo akasema nao tena. 21 Lakini wao wakazidi kupiga kelele, “Msulubishe! Msulubishe!” 22 Kwa mara ya tatu Pilato akasema nao tena, “Amefanya kosa gani huyu mtu? Sioni sababu yo yote ya kutosha kumhukumu adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko kisha nimwachilie .”

23 Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu na kusisi tiza kwamba Yesu asulubiwe. Hatimaye, kelele zao zikashinda. 24 Pilato akaamua kutoa hukumu waliyoitaka. 25 Akamwachia huru yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini; akamkabidhi Yesu mikononi mwao, wamfa nyie watakavyo. Yesu Asulubiwa Msalabani

26 Na walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja ait waye Simoni wa Kirene aliyekuwa anatoka mashambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha atembee nyuma ya Yesu. 27 Umati mkubwa wa watu wakamfuata Yesu ikiwa ni pamoja na wanawake waliokuwa wakimlilia na kuomboleza. 28 Lakini Yesu akawageukia, akawaam bia, “Enyi akina mama wa Yerusalemu, msinililie mimi bali jilil ieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29 Kwa maana wakati utafika ambapo mtasema, ‘Wamebarikiwa akina mama tasa, ambao hawakuzaa na matiti yao hayakunyonyesha.’ 30 Na watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni’ na vilima, ‘Tufunikeni’. 31 Kwa maana kama watu wanafanya mambo haya wakati mti ni mbichi, itakuwaje utakapo kauka?”

32 Wahalifu wengine wawili pia walipelekwa wakasulubiwe pamoja na Yesu. 33 Walipofika mahali paitwapo “Fuvu la kichwa,” wakamsulubisha Yesu hapo pamoja na hao wahalifu; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.

34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui wali tendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. 35 Watu wakasi mama pale wakimwangalia. Viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Si aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama kweli yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.” 36 Askari nao wakam wendea, wakamdhihaki. Wakamletea siki anywe, 37 wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe tuone.”

38 Na maandishi haya yaliwekwa kwenye msalaba juu ya kichwa chake: “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.” 39 Mmoja kati ya wale wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”

40 Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa. 41 Adhabu yetu ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini huyu hakufanya kosa lo lote.” 42 Kisha akasema, “Bwana Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”

Yesu Afa Msalabani

44 Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa, 45 kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili. 46 Yesu akapaza sauti akasema, “Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.

47 Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 48 Na watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hilo walipoy aona hayo, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.

49 Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wanawake wal iokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyata zama mambo haya. Yesu Azikwa Kaburini

50 Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yusufu mwenyeji wa mji wa Arimathaya, ambaye alikuwa anautazamia Ufalme wa Mungu. Yeye ali kuwa mjumbe wa Baraza na pia alikuwa mtu mwema na mwenye kuheshi mika. 51 Lakini yeye hakukubaliana na wajumbe wenzake katika uamuzi wao na kitendo cha kumsulubisha Yesu. 52 Basi, Yusufu alikwenda kwa Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. 53 Akaushusha kutoka msalabani, akauzungushia sanda, akauhifadhi katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kaburi hilo lilikuwa halijatumika bado. 54 Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, Siku ya Maandalizi, na sabato ilikuwa karibu ianze. 55 Wale wanawake waliokuwa wamefuatana na Yesu kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa humo. 56 Kisha wakarudi nyumbani wakaandaa marashi na manukato ya kuupaka huo mwili. Lakini waka pumzika siku ya sabato kama ilivyoamriwa.

Gavana Pilato Amhoji Yesu

(Mt 27:1-2,11-14; Mk 15:1-5; Yh 18:28-38)

23 Kisha kundi lote likasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. Wakaanza kumshitaki Yesu na kumwambia Pilato, “Tumemkamata mtu huyu akijaribu kuwapotosha watu wetu. Anasema tusilipe kodi kwa Kaisari. Anajiita Masihi, mfalme.”

Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ni mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akajibu, “Ndiyo, unaweza kusema hivyo.”

Pilato akawaambia wakuu wa makuhani na watu, “Sioni kosa lolote kwa mtu huyu.”

Lakini waliendelea kusema, “Mafundisho yake yanasababisha matatizo katika Uyahudi yote. Alianzia Galilaya na sasa yupo hapa!”

Pilato Ampeleka Yesu Kwa Herode

Pilato aliposikia hili, akauliza, “Mtu huyu anatoka Galilaya?” Akatambua kuwa Yesu yuko chini ya mamlaka ya Herode. Siku hizo Herode alikuwa Yerusalemu, hivyo Pilato alimpeleka Yesu kwake.

Herode alipomwona Yesu alifurahi sana. Alikuwa akisikia habari zake na kwa muda mrefu alikuwa anataka kukutana na Yesu. Herode alitaka kuona muujiza, hivyo alitegemea kwamba Yesu angefanya muujiza mmoja. Akamwuliza Yesu maswali mengi, lakini Yesu hakusema chochote. 10 Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wamesimama pale wakipaza sauti zao wakimshitaki kwa Herode. 11 Ndipo Herode na askari wake wakamcheka. Wakamfanyia mzaha kwa kumvalisha mavazi kama ambayo wafalme huvaa. Kisha Herode akamrudisha Yesu kwa Pilato. 12 Nyakati za nyuma Pilato na Herode walikuwa maadui daima. Kuanzia siku ile wakawa marafiki.

Pilato Ajaribu Kumwachia Huru Yesu

(Mt 27:15-26; Mk 15:6-15; Yh 18:39-19:16)

13 Pilato aliwaita viongozi wa makuhani, viongozi wa Kiyahudi na watu wote pamoja. 14 Akawaambia, “Mlimleta mtu huyu kwangu. Mlisema alikuwa anawapotosha watu. Lakini nimemchunguza mbele yenu nyote na sijaona hatia juu ya kitu chochote mnachomshitakia. 15 Hata Herode hakumwona kuwa ana hatia yo yote. Akamrudisha kwetu. Tazameni, hajafanya jambo lolote baya linalostahili adhabu ya kifo. 16 Kwa hiyo, baada ya kumwadhibu kidogo nitamwacha aende zake.” 17 [a]

18 Lakini wote walipaza sauti zao pamoja, “Mwue! Mwachie huru Baraba!” 19 (Baraba alifungwa gerezani kwa sababu ya kuanzisha fujo mjini na kwa mauaji.)

20 Pilato alitaka amwachie huru Yesu. Hivyo Pilato akawaambia atamwachilia. 21 Lakini walipaza sauti tena wakisema, “Mwue, Mwue msalabani!”

22 Mara ya tatu Pilato akawaambia watu, “Kwa nini? Amefanya kosa gani? Hana hatia. Sioni sababu ya kumwua. Hivyo nitamwachia huru baada ya kumwadhibu kidogo.”

23 Lakini watu waliendelea kupaza sauti. Walidai Yesu auawe msalabani. Kelele zao zikawa kubwa kiasi kwamba 24 Pilato aliamua kuwapa kile walichotaka. 25 Walitaka Baraba aliyekuwa gerezani kwa sababu ya kuanzisha fujo na mauaji aachiwe huru. Pilato akamwachia Baraba. Na kumtoa Yesu ili auawe. Hili ndilo watu walitaka.

Yesu Awambwa Msalabani

(Mt 27:32-44; Mk 15:21-32; Yh 19:17-27)

26 Askari wakamwongoza Yesu kumtoa nje ya mji. Wakati huo huo mtu mmoja kutoka Kirene alikuwa anaingia mjini kutoka maeneo nje ya Yerusalemu. Askari wakamlazimisha kuubeba msalaba wa Yesu na kumfuata Yesu kwa nyuma.

27 Kundi kubwa wakamfuata Yesu. Baadhi ya wanawake waliokuwemo kwenye kundi walilia na kuomboleza. Walimwonea huruma. 28 Lakini Yesu aligeuka na kuwaambia, “Wanawake wa Yerusalemu, msinililie. Jililieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29 Wakati unakuja ambapo watu watasema, ‘Wanawake wasioweza kuwa na watoto ndio ambao Mungu amewabariki. Hakika ni baraka kwamba hawana watoto wa kutunza.’ 30 Watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni!’ Wataviambia vilima, ‘Tufunikeni!’(A) 31 Kama hili linaweza kutokea kwa mtu aliye mwema, nini kitatokea kwa wenye hatia?”

32 Walikuwepo pia wahalifu wawili waliotolewa nje ya mji pamoja na Yesu ili wauawe. 33 Walipelekwa mahali palipoitwa “Fuvu la Kichwa.” Askari walimpigilia Yesu msalabani pale. Waliwapigilia misalabani wahalifu pia, mmoja aliwekwa upande wa kulia na mwingine kushoto kwa Yesu.

34 Na Yesu alikuwa anasema, “Baba uwasamehe watu hawa, kwa sababu hawajui wanalofanya.”

Askari waligawana nguo zake kwa kutumia kamari. 35 Watu walisimama pale wakiangalia kila kitu kilichokuwa kinatokea. Viongozi wa Kiyahudi walimcheka Yesu. Walisema, “Kama kweli yeye ni Masihi, Mfalme Mteule wa Mungu, basi ajiokoe. Je, hakuwaokoa wengine?”

36 Hata askari walimcheka Yesu na kumfanyia mizaha. Walikuja na kumpa siki ya mvinyo. 37 Wakasema, “Ikiwa wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe!” 38 Waliandika maneno haya kwenye kibao msalabani juu ya kichwa chake: “Huyu ni Mfalme wa Wayahudi”.

39 Mmoja wa wahalifu aliyekuwa ananing'inia pale akaanza kumtukana Yesu: “Wewe siye Masihi? Basi jiokoe na utuokoe sisi pia!”

40 Lakini mhalifu mwingine alimnyamazisha asiendelee kumtukana Yesu. Akasema, “Unapaswa kumwogopa Mungu. Sisi sote tutakufa muda si mrefu. 41 Wewe na mimi tuna hatia, tunastahili kufa kwa sababu tulitenda mabaya. Lakini mtu huyu hajafanya chochote kibaya.” 42 Kisha akamwambia Yesu, “Unikumbuke utakapoanza kutawala kama mfalme!”

43 Yesu akamwambia, “Ninakwambia kwa uhakika, leo utakuwa pamoja nami Paradiso.”

Yesu Afariki

(Mt 27:45-56; Mk 15:33-41; Yh 19:28-30)

44 Ilikuwa yapata saa sita mchana, lakini kulibadilika kukawa giza mpaka saa tisa alasiri, 45 kwa sababu jua liliacha kung'aa. Pazia ndani ya Hekalu lilichanika vipande viwili. 46 Yesu alipaza sauti akasema, “Baba, ninaiweka roho yangu mikononi mwako!”(B) Baada ya Yesu kusema haya, akafa.

47 Mkuu wa askari wa Kirumi aliyekuwa pale alipoona yaliyotokea, alimsifu Mungu, akisema, “Ninajua mtu huyu alikuwa mtu mwema!”

48 Watu wengi walikuwa wametoka mjini kuja kuona tukio hili. Walipoona, wakahuzunika, wakaondoka wakiwa wanapiga vifua vyao. 49 Watu waliokuwa marafiki wa karibu wa Yesu walikuwepo pale. Pia, walikuwepo baadhi ya wanawake waliomfuata Yesu kutoka Galilaya. Walisimama mbali kutoka msalabani, waliyaona mambo haya.

Yesu Azikwa

(Mt 27:57-61; Mk 15:42-47; Yh 19:38-42)

50-51 Mtu mmoja aliyeitwa Yusufu kutoka mji wa Uyahudi ulioitwa Arimathaya alikuwapo pale. Alikuwa mtu mwema, aliyeishi namna Mungu alivyotaka. Alikuwa anausubiri ufalme wa Mungu uje. Yusufu alikuwa mjumbe wa baraza la Kiyahudi. Lakini hakukubali pale viongozi wengine wa Kiyahudi walipoamua kumwua Yesu. 52 Alikwenda kwa Pilato na kumwomba mwili wa Yesu. 53 Aliushusha mwili kutoka msalabani na kuufunga kwenye nguo. Kisha akauweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika ukuta wa mwamba. Kaburi hili lilikuwa halijatumika bado. 54 Ilikuwa jioni Siku ya Maandalizi ya Sabato. Sabato ilikuwa ianze baada ya jua kuzama.

55 Wanawake waliotoka Galilaya pamoja na Yesu walimfuata Yusufu. Wakaliona kaburi. Ndani yake wakaona mahali alipouweka mwili wa Yesu. 56 Kisha wakaenda kuandaa manukato yanayonukia vizuri ili kuupaka mwili wa Yesu.

Siku ya Sabato walipumzika, kama ilivyoamriwa katika Sheria ya Musa.

Footnotes

  1. 23:17 Nakala chache za Kiyunani zimeongeza mstari wa 17: “Kila mwaka wakati wa Siku Kuu ya Pasaka, ilimpasa Pilato kumwachia huru mfungwa mmoja.”