Add parallel Print Page Options

Yesu Afariki

(Mt 27:45-56; Mk 15:33-41; Lk 23:44-49)

28 Baadaye, Yesu akajua kuwa kila kitu kimekwisha kamilika. Ili kuyafanya Maandiko yatimie akasema, “Nina kiu.”[a] 29 Palikuwapo na bakuli lililojaa siki[b] mahali pale, wale askari wakachovya sponji ndani yake. Wakaiweka ile sponji kwenye tawi la mwanzi na kuliinua hadi kinywani kwa Yesu. 30 Alipoionja ile siki, akasema, “Imekwisha.” Baada ya hapo akainamisha kichwa chake na kufa.

Read full chapter

Footnotes

  1. 19:28 Nina kiu Tazama Zab 22:15; 69:21.
  2. 19:29 siki Divai chungu; yaani, siki ya mvinyo (au divai chungu) uliochanganywa na maji. Hiki kilikuwa kinywaji rahisi na kilichojulikana sana wakati wa Yesu.