Yesu Ahukumiwa Kifo

19 Ndipo Pilato akamtoa Yesu akaamuru apigwe viboko. Askari wakasuka taji ya miiba wakamwekea Yesu kichwani, wakamvika na kanzu ya zambarau.

Lakini walipomkaribia Yesu wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu.

Mfalme wa Wayahudi!’

Kwa hiyo Yesu akatoka nje akiwa amevaa ile taji ya miiba na kanzu ya zambarau. Pilato akawaambia, “Huyu hapa mtu wenu.” Wale makuhani wakuu na viongozi wa Wayahudi walipomwona wakapiga kelele, “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawajibu, “Mchukueni mumsulubishe ninyi, kwa sababu mimi sioni kosa alilo tenda.” Wao wakamjibu, “Sisi tunayo sheria ambayo inamhukumu kifo kwa sababu yeye anajiita Mwana wa Mungu.” Pilato aliposi kia haya aliingiwa na hofu. Akaingia ukumbini tena akamwuliza Yesu, “Wewe unatoka wapi?” Lakini Yesu hakumjibu. 10 Pilato akamwambia, “Kwa nini hunijibu? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukuachilia huru au kukusulubisha?” 11 Ndipo Yesu akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka ye yote juu yangu kama Mungu hakukupa mamlaka hayo; kwa hiyo mtu aliyenishtaki kwako ana dhambi kubwa zaidi.” 12 Tangu wakati huo Pilato akaanza kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakasema, “Ukimwachilia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu ye yote anayejifanya kuwa mfalme anampinga Kaisari.” 13 Pilato aliposi kia maneno haya alimtoa Yesu nje tena akaketi katika kiti chake cha kuhukumia, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe - kwa Kiebrania paliitwa Gabatha.

14 Siku hiyo ilikuwa ni siku moja kabla ya Pasaka, siku iliyoitwa siku ya Matayarisho, yapata kama saa sita hivi. Pilato Akawaambia Wayahudi, “Huyu hapa Mfalme wenu!” 15 Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!” Pilato akawauliza, “Je, nimsulubishe Mfalme wenu?” Wale makuhani wakuu wakamjibu, “Hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.” 16 Ndipo Pilato akawaka bidhi Yesu wamsulubishe.

Yesu Asulubishwa

17 Kwa hiyo wakamchukua Yesu, naye akatoka akiwa amebeba msalaba wake kuelekea mahali palipoitwa, ‘Fuvu la kichwa,’ au kwa Kiebrania, Golgotha. 18 Hapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja naye walisulubishwa watu wengine wawili, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia wa Yesu. 19 Pilato aliandika maneno yafuatayo kwenye kibao, kikawekwa juu kwenye msalaba wa Yesu: “YESU WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI” 20 Kwa kuwa mahali hapo palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maneno haya ambayo yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kilatini na Kigiriki. 21 Makuhani wakuu wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali ‘Mtu huyu alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi.”’ 22 Pilato akawajibu, “ Nilichokwisha andika, nimeandika.”

Mavazi Ya Yesu Yagawanywa

23 Maaskari walipokwisha msulubisha Yesu, walichukua mavazi yake wakayagawa mafungu manne; kila askari akapata moja. Ila wal ikubaliana wasipasue ile kanzu yake kwa maana ilikuwa imefumwa tangu juu hadi chini na haikukatwa mahali po pote. 24 Wakaam biana, “Tusiipasue ila tupige kura tuone ni nani aichukue.” Hii ilitimiza yale Maandiko yaliyosema, “Waligawana mavazi yangu, na kanzu yangu wakaipigia kura.” 25 Kwa hiyo wakapiga kura. Karibu na msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama: Mariamu mama yake, shan gazi yake, Mariamu mke wa Klopa na Mariamu Magdalena. 26 Yesu alipomwona mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, alimwambia mama yake, “Mama, huyo ni mwanao!” 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Na huyo ni mama yako.” Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.

Kifo Cha Yesu

28 Baada ya haya Yesu alifahamu ya kuwa mambo yote yameka milika, kwa hiyo, ili kutimiza Maandiko, akasema, “Naona kiu.” 29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachukua sponji iliyolowanishwa kwenye hiyo siki wakaichomeka kwenye ufito wa hisopo wakampandishia mdomoni. 30 Baada ya kuipokea hiyo siki, Yesu akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa, akakata roho.

31 Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi ya Pasaka Wayahudi hawakutaka miili yao ibaki msalabani siku ya sabato. Hii ingekuwa sabato ya pekee kwa kuwa iliangukia wakati wa Pasaka. Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe ili wafe upesi waondolewe msalabani. 32 Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa na Yesu na wa pili pia. 34 Ila askari mmoja akamchoma mkuki ubavuni, na mara pakatoka damu na maji. 35 Mambo haya yamehakikishwa na mtu aliyeyaona, na ushahidi wake ni wa kuaminika. Yeye anajua ya kuwa aliyosema ni kweli, naye ametoa ushuhuda huu ili nanyi mpate kuamini. 36 Kwa maana mambo haya yalitokea ili kutimiza Maandiko yaliyosema, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” 37 Na pia Maandiko mengine yanasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma kwa mkuki.” 38 Baada ya haya, Yusufu wa Arimathea aliyekuwa mfuasi wa siri wa Yesu, maana aliwaogopa Wayahudi, akamwomba Pilato auchukue mwili wa Yesu; naye akamruhusu. Kwa hiyo akaja, akauchukua mwili wa Yesu. 39 Naye Nikodemo, yule ambaye alimwen dea Yesu kwa siri usiku, alikuja na mchanganyiko wa manukato zaidi ya kilo thelathini. 40 Wakauchukua mwili wa Yesu, wakau vika sanda iliyokuwa na manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Way ahudi. 41 Karibu na pale walipomsulubisha palikuwa na bustani yenye kaburi ambalo lilikuwa halijatumika. 42 Kwa hiyo ili kuka milisha mazishi kabla ya sabato, wakamzika Yesu kwenye hilo kab uri lililokuwa karibu.

19 Kisha Pilato akaamuru Yesu aondolewe akachapwe viboko. Askari wakatengeneza taji kutokana na matawi yenye miiba na kuiweka kichwani kwake. Kisha wakamzungushia vazi la rangi ya zambarau mwilini mwake. Wakaendelea kumkaribia wakisema, “Salamu kwako mfalme wa Wayahudi!” Kisha wakampiga Yesu usoni.

Kwa mara nyingine Pilato alienda nje na kuwaambia viongozi wa Wayahudi, “Tazameni! Ninamtoa nje Yesu na kumleta kwenu. Ninataka mfahamu kuwa sijapata kwake jambo lolote ambalo kwa hilo naweza kumshitaki.” Kisha Yesu akatoka nje akiwa amevishwa taji ya miiba na vazi la rangi ya zambarau. Pilato akawaambia Wayahudi, “Huyu ndiye mtu mwenyewe!”

Viongozi wa makuhani na walinzi wa Kiyahudi walipomwona Yesu wakapiga kelele, “Mpigilieni misumari msalabani! Mpigilieni misumari msalabani!”

Lakini Pilato akajibu, “Mchukueni na mpigilieni msalabani ninyi wenyewe. Mimi sioni kosa lolote la kumshitaki.”

Viongozi wa Wayahudi wakasema, “Tunayo sheria inayosema kuwa ni lazima afe, kwa sababu alisema kuwa yeye ni Mwana wa Mungu.”

Pilato aliposikia haya, aliogopa zaidi. Hivyo akarudi ndani ya jumba lake na kumwuliza Yesu, “Wewe unatoka wapi?” Lakini Yesu hakumjibu kitu. 10 Pilato akasema, “Unakataa kusema nami? Kumbuka, ninao uwezo wa kukuweka huru au kukuua msalabani.”

11 Yesu akajibu, “Uwezo pekee ulio nao juu yangu ni ule uwezo uliopewa na Mungu. Kwa hiyo yule aliyenitoa mimi kwenu anayo hatia ya dhambi kubwa zaidi.”

12 Baada ya hayo, Pilato alijaribu kumwacha huru Yesu. Lakini viongozi wa Wayahudi wakapiga kelele, “Yeyote anayejiweka mwenyewe kuwa mfalme yuko kinyume cha Kaisari. Hivyo kama utamwacha huru mtu huyu, hiyo itakuwa na maana kuwa wewe si rafiki wa Kaisari.”

13 Pilato aliposikia maneno hayo, akamtoa nje Yesu na kumweka mahali palipoitwa “Sakafu ya Mawe.” (Kwa Kiaramu jina lake ni Gabatha.) Pale Pilato akaketi katika kiti cha hakimu. 14 Wakati huu, ilikuwa imekaribia kuwa saa sita adhuhuri katika Siku ya Matayarisho ya juma la Pasaka. Pilato akawaambia Wayahudi, “Huyu hapa mfalme wenu!”

15 Wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Mwue msalabani!”

Pilato akawauliza, “Mnanitaka nimwue mfalme wenu msalabani?”

Viongozi wa makuhani wakajibu, “Kaisari ndiye Mfalme pekee tuliye naye!”

16 Hivyo Pilato akamkabidhi Yesu kwao ili auawe juu ya msalaba. Askari wakamchukua Yesu.

Yesu Awambwa Msalabani

(Mt 27:32-44; Mk 15:21-32; Lk 23:26-43)

17 Naye Yesu akaubeba msalaba wake hadi mahali panapoitwa “Fuvu la Kichwa”. (Kwa Kiaramu mahali hapo paliitwa “Golgotha”.) 18 Hapo wakampigilia Yesu kwa misumari katika msalaba. Pia wakawapigilia kwa misumari watu wengine wawili kwenye misalaba miwili tofauti. Kila mmoja akawekwa pembeni upande wa kushoto na kuume wa msalaba wa Yesu naye akawa katikati yao.

19 Pilato akawaambia waandike kibao na kisha kukiweka juu ya msalaba. Kibao hicho kiliandikwa na kilisema, “Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi.” 20 Kibao hicho kiliandikwa kwa Kiaramu, Kirumi na Kiyunani. Wayahudi walio wengi walikisoma kibao hicho, kwa sababu mahali ambapo Yesu alipigiliwa kwa misumari msalabani palikuwa karibu na mji.

21 Viongozi wa makuhani wa Kiyahudi wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi.’ Bali andika, ‘Mtu huyu alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi.’”

22 Pilato akawajibu, “Sitayabadili yale niliyokwisha kuyaandika.”

23 Hivyo baada ya askari kumpigilia Yesu kwa misumari msalabani, walizichukua nguo zake na kuzigawa katika mafungu manne. Kila askari alipata fungu moja. Pia wakalichukua vazi lake lililokuwa limefumwa kwa kipande kimoja tu cha kitambaa kutoka juu hadi chini. 24 Hivyo askari wakasemezana wao kwa wao, “Hatutalichana vazi hili vipande vipande. Hebu tulipigie kura kuona nani atakayelipata.” Hili lilitokea ili kuweka wazi maana kamili ya yale yanayosemwa katika Maandiko:

“Waligawana miongoni mwao mavazi yangu,
    na wakakipigia kura kile nilichokuwa nimevaa.”(A)

Hivyo ndivyo maaskari walivyofanya.

25 Mama yake Yesu alisimama karibu na msalaba wa mwanawe, Dada yake mamaye Yesu pia alikuwa amesimama pale pamoja na Mariamu mke wake Kleopa, na Mariamu Magdalena. 26 Yesu akamwona mama yake na akamwona pia mfuasi aliyempenda sana akisimama pale. Akamwambia mama yake, “Mama mpendwa, mwangalie huyo, naye ni mwanao sasa.” 27 Kisha akamwambia yule mfuasi, “Huyu hapa ni mama yako sasa.” Kisha baada ya hayo, mfuasi huyo akamchukua mama yake Yesu na kuishi naye nyumbani kwake.

Yesu Afariki

(Mt 27:45-56; Mk 15:33-41; Lk 23:44-49)

28 Baadaye, Yesu akajua kuwa kila kitu kimekwisha kamilika. Ili kuyafanya Maandiko yatimie akasema, “Nina kiu.”[a] 29 Palikuwapo na bakuli lililojaa siki[b] mahali pale, wale askari wakachovya sponji ndani yake. Wakaiweka ile sponji kwenye tawi la mwanzi na kuliinua hadi kinywani kwa Yesu. 30 Alipoionja ile siki, akasema, “Imekwisha.” Baada ya hapo akainamisha kichwa chake na kufa.

31 Hii ilikuwa Ijumaa, Siku ya Matayarisho. Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya Sabato maalumu. Viongozi wa Kiyahudi hawakuitaka ile miili ya waliosulubiwa ikae juu misalabani katika siku ya Sabato. Hivyo wakamwomba Pilato atoe amri kuwa miguu ya wale watu misalabani ivunjwe. Pia wakaomba ile miili ishushwe kutoka kwenye misalaba. 32 Kwa hiyo askari wakaja na kuivunja miguu[c] ya watu wale wawili kwenye misalaba kando ya Yesu. 33 Lakini askari walipomkaribia Yesu, wakaona kuwa tayari alikuwa amekwisha kufa. Hivyo hawakuivunja miguu yake.

34 Lakini mmoja wa askari akauchoma ubavu wa Yesu kwa mkuki wake. Mara hiyo hiyo damu na maji vikamtoka mwilini mwake. 35 (Yeye aliyeona haya yakitokea ametueleza. Aliyaeleza haya ili ninyi pia muweze kuamini. Mambo anayosema ni ya kweli. Yeye anajua kuwa anasema kweli.) 36 Mambo haya yalitokea ili kutimiza Maandiko yaliyosema, “Hakuna mfupa wake utakaovunjwa”[d] 37 na “Watu watamwangalia yeye waliyemchoma.”(B)

Yesu Azikwa

(Mt 27:57-61; Mk 15:42-47; Lk 23:50-56)

38 Baadaye, mtu mmoja aliyeitwa Yusufu wa kutoka Arimathaya akamwomba Pilato mwili wa Yesu. (Yusufu alikuwa mfuasi wa Yesu, lakini hakumweleza mtu yeyote, kwa sababu aliwaogopa viongozi wa Kiyahudi.) Pilato akasema Yusufu anaweza kuuchukua mwili wa Yesu, hivyo naye akaja na kuuchukua.

39 Nikodemu akaenda pamoja na Yusufu. Nikodemu, alikuwa ni yule mtu aliyekuja kwa Yesu hapo kabla na kuzungumza naye usiku. Huyu alileta kadiri ya lita[e] mia moja ya marashi yenye mchanganyiko wa manemane na uvumba. 40 Watu hawa wawili wakauchukua mwili wa Yesu na wakauzungushia vipande vya sanda ya kitani pamoja na marashi yale. (Hivi ndivyo Wayahudi walivyowazika watu.) 41 Pale msalabani sehemu alipouawa Yesu, palikuwepo na bustani. Katika bustani ile palikuwemo na kaburi[f] jipya la kuzikia. Hakuna mtu aliyewahi kuzikwa ndani ya kaburi lile. 42 Wanaume wakauweka mwili wa Yesu katika kaburi lile kwa kuwa lilikuwa karibu, na Wayahudi walikuwa wakijiandaa kuianza siku yao ya Sabato.

Footnotes

  1. 19:28 Nina kiu Tazama Zab 22:15; 69:21.
  2. 19:29 siki Divai chungu; yaani, siki ya mvinyo (au divai chungu) uliochanganywa na maji. Hiki kilikuwa kinywaji rahisi na kilichojulikana sana wakati wa Yesu.
  3. 19:32 kuivunja miguu Miguu ilivunjwa ili kuwafanya wale waliokuwa misalabani wafe haraka zaidi.
  4. 19:36 Zab 34:20. Wazo linatoka katika Kut 12:46; Hes 9:12.
  5. 19:39 lita Kwa maana ya kawaida, “pauni za Kirumi 100” (yaani litras 100), kama kilo 30 hivi.
  6. 19:41 kaburi Kwa neno “kaburi” hapa inamaanisha ni pango la kuzikia, ambalo siyo shimo tu lililochimbwa ardhini. Pia katika mstari wa 42 na 20:1,2,3,4,6,8 na 11.