Yesu Akamatwa

18 Baada ya sala hii Yesu aliondoka na wanafunzi wake waka vuka kijito cha Kidroni wakaingia katika bustani iliyokuwa upande wa pili. Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, pia alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana na wanafunzi wake hapo mara kwa mara. Kwa hiyo Yuda akaja kwenye bustani hiyo akiongoza kikundi cha askari wa Kirumi na walinzi wa Hekalu kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo wakiwa na taa na silaha. Yesu alijua yata kayompata, kwa hiyo akawasogelea akawauliza, “Mnamtafuta nani?” Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawaambia, “Ni mimi.” Yuda ambaye alimsaliti alikuwa amesimama na wale askari. Yesu alipowaambia, ‘Ni mimi,’ walirudi nyuma wakaanguka chini! Akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Nao wakajibu, “Yesu wa Nazareti .” Yesu akawaambia, “Nimekwisha waeleza kuwa ni mimi; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi waachilieni hawa wengine waende.” Alisema haya ili lile neno alilosema lipate kutimia, ‘Kati ya wale ulionipa sikupoteza hata mmoja.’ 10 Ndipo Simoni Petro akachomoa upanga aliokuwa amechukua akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu. Jina la mtumishi huyo lilikuwa Malko. 11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala. Je, nisinywe kikombe cha mateso alichonipa Baba?” 12 Kwa hiyo mkuu wa kikosi na askari wake pamoja na wale walinzi wa Hekalu waliot umwa na viongozi wa Wayahudi, wakamkamata Yesu wakamfunga mikono. 13 Kisha wakampeleka kwanza kwa Anasi mkwewe Kayafa ambaye ali kuwa ndiye kuhani mkuu mwaka ule. 14 Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauri viongozi wengine wa Kiyahudi kwamba ingekuwa afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.

Petro Anamkana Yesu

15 Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa kuhani mkuu kwa hiyo aliingia ndani ya ukumbi pamoja na Yesu. 16 Lakini Petro alisimama nje karibu na mlango. Ndipo yule mwanafunzi mwin gine akazungumza na msichana aliyekuwa analinda mlangoni, akamru husu amwingize Petro ndani. 17 Yule msichana akamwuliza Petro, “Je, wewe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro aka jibu, “Hata! Mimi sio.” 18 Wale watumishi na askari walikuwa wamesimama wakiota moto wa mkaa ambao walikuwa wamewasha kwa sababu pale ukumbini palikuwa na baridi kali. Petro naye alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.

Kuhani Mkuu Amhoji Yesu

19 Kuhani mkuu akamwuliza Yesu maswali kuhusu wanafunzi wake na mafundisho yake. 20 Yesu akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza wazi wazi mbele ya watu wote. Nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni ambapo Wayahudi wote hukusanyika. Sijasema jambo lo lote kwa siri. 21 Mbona unaniuliza mimi maswali? Waulize walionisiki liza nimewaambia nini. Wao wanajua niliyosema.” 22 Mmoja wa wale walinzi akampiga Yesu kofi, kisha akasema, “Unathubutuje kumjibu kuhani mkuu hivyo?” 23 Yesu akamjibu, “Kama nimesema jambo baya waeleze watu wote hapa ubaya niliosema. Lakini kama nimesema yaliyo kweli, mbona umenipiga?” 24 Ndipo Anasi akampeleka Yesu kwa kuhani mkuu Kayafa, akiwa bado amefungwa.

Petro Amkana Yesu Tena

25 Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya wale waliokuwepo wakamwuliza, “Wewe ni mmoja wa wana funzi wake?” Petro akakana, akasema, “Mimi sio.” 26 Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ndugu yake yule mtu ambaye Petro alim kata sikio, akamwuliza, “Je, sikukuona kule bustanini ukiwa na Yesu?” 27 Kwa mara nyingine tena Petro akakataa kwamba alimfa hamu Yesu. Wakati huo huo jogoo akawika.

Yesu Apelekwa Kwa Pilato

28 Ndipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa wakampeleka kwenye ikulu ya gavana wa Kirumi. Ilikuwa ni alfa jiri. Wayahudi waliokuwa wanamshtaki Yesu hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa wachafu kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika sikukuu ya Pasaka. 29 Kwa hiyo Pilato akatoka nje kuwaona akawauliza, “Mmeleta mashtaka gani kumhusu mtu huyu?” 30 Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa ametenda maovu tusingemleta kwako.” 31 Pilato akawaambia, “Basi mchukueni ninyi mkamhukumu kwa kufuata sheria zenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisi haturuhusiwi kutoa hukumu ya kifo kwa mtu ye yote.” 32 Walisema hivyo ili yale maneno aliyosema Yesu kuhusu atakavy okufa, yapate kutimia. 33 Kwa hiyo Pilato akaingia ndani akam wita Yesu akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” 34 Yesu akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwe nyewe au kutokana na ulivyoambiwa kunihusu mimi?” 35 Pilato akamjibu, “Unadhani mimi ni Myahudi? Watu wa taifa lako na maku hani wao wakuu wamekushtaki kwangu. Umefanya kosa gani?” 36 Ndipo Yesu akamwambia, “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Ingekuwa hivyo, watumishi wangu wangenipigania na kuhakikisha kuwa siwekwi mikononi mwa Wayahudi; lakini Ufalme wangu hautoki ulimwenguni.” 37 Pilato akasema, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema mimi ni mfalme. Nimezaliwa na nime kuja ulimwenguni kwa makusudi ya kushuhudia kweli. Mtu ye yote anayepokea yaliyo ya kweli anakubaliana na mafundisho yangu.” 38 Pilato akamwuliza Yesu, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu, “Sioni kosa lo lote ali lotenda mtu huyu.

39 Lakini kuna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachilie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mngependa nimwachilie huru huyu ‘Mfalme wa Wayahudi?” ’ 40 Wao wakapiga kelele wakisema, “Hapana, usimwachilie huyo. Tufungulie Bar aba!” Baraba alikuwa mnyang’anyi.

Yesu Akamatwa

(Mt 26:47-56; Mk 14:43-50; Lk 22:47-53)

18 Yesu alipomaliza kuomba, akaondoka pamoja na wafuasi wake kwenda ng'ambo kuvuka bonde la Kidroni. Akaenda katika bustani mahali hapo, akiwa bado pamoja na wafuasi wake.

Yuda, yule aliyehusika kumsaliti Yesu, alipafahamu mahali pale. Alipajua kwa sababu Yesu mara nyingi alikutana na wafuasi wake pale. Kwa hiyo Yuda akaongoza kundi la askari hadi katika bustani hiyo pamoja na walinzi wengine kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Hawa walikuwa wamebeba mienge, taa, na silaha.

Yesu alikwisha kujua yote ambayo yangempata. Hivyo aliwaendea na kuwauliza, “Je, ni nani mnayemtafuta?”

Wakamjibu, “Yesu kutoka Nazareti.”

Akawaambia, “Mimi ni Yesu.”[a] (Yuda yule aliyehusika kumsaliti Yesu alikuwa amesimama hapo pamoja nao.) Yesu aliposema, “Mimi ni Yesu,” wale watu walirudi nyuma na kuanguka chini.

Akawauliza tena, “Je, ni nani mnayemtafuta?”

Wakasema, “Yesu kutoka Nazareti.”

Yesu akasema, “Nimewaambia kwamba mimi ndiye Yesu. Hivyo kama mnanitafuta mimi, basi waacheni huru watu hawa waende zao.” Hii ilikuwa kuonesha ukweli wa yale aliyosema Yesu mapema: “Sikumpoteza hata mmoja wa wale ulionipa.”

10 Simoni Petro akauchomoa upanga aliokuwa ameufunga kiunoni. Akampiga nao mtumishi wa Kuhani Mkuu, na kulikata sikio lake la kulia. (Jina la mtumishi huyo lilikuwa ni Maliko.) 11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha jambia lako mahali pake! Ninapaswa kunywa toka kikombe[b] ambacho Baba amenipa nikinywee.”

Yesu Aletwa Mbele ya Anasi

(Mt 26:57-58; Mk 14:53-54; Lk 22:54)

12 Kisha askari hao pamoja na mkuu wao na walinzi wa Kiyahudi wakamkamata Yesu. Wakamfunga, 13 nao wakampeleka kwanza kwa Anasi, baba mkwe wa Kayafa. Kayafa alikuwa Kuhani Mkuu kwa mwaka huo. 14 Naye ndiye aliyewashauri viongozi wengine wa Kiyahudi kwamba ingemfaa mtu mmoja afe[c] kwa ajili ya watu wote.

Petro Amkana Yesu

(Mt 26:69-70; Mk 14:66-68; Lk 22:55-57)

15 Simoni Petro na mmoja wa wafuasi wengine wa Yesu walienda pamoja na Yesu. Mfuasi huyu alimfahamu kuhani mkuu. Hivyo akaingia pamoja na Yesu ndani ya uwanja wa nyumba ya kuhani mkuu. 16 Lakini Petro alisubiri nje karibu na mlango. Yule mfuasi aliyemjua kuhani mkuu alirudi nje na kuongea na mlinda mlango. Kisha alimleta Petro ndani. 17 Msichana aliyekuwepo langoni alimwambia Petro, “Je! Wewe pia ni mmoja wa wafuasi wa mtu yule?”

Petro akajibu, “Hapana, mimi siye!”

18 Ilikuwa baridi, hivyo watumishi na walinzi waliwasha moto wa kuni. Walikuwa wameuzunguka, wakipasha joto miili yao naye Petro alikuwa amesimama pamoja nao.

Kuhani Mkuu Amhoji Yesu

(Mt 26:59-66; Mk 14:55-64; Lk 22:66-71)

19 Kuhani Mkuu akamwuliza Yesu maswali kuhusu wafuasi wake pamoja na mafundisho aliyowapa. 20 Yesu akamjibu, “Daima nimesema wazi kwa watu wote. Siku zote nimefundisha kwenye masinagogi na kwenye eneo la Hekalu. Wayahudi wote hukusanyika pale. Sijawahi kusema jambo lo lote kwa siri. 21 Sasa kwa nini unaniuliza? Waulize watu waliosikia mafundisho yangu. Wao wanajua niliyosema!”

22 Yesu aliposema hivyo, mmoja wa walinzi aliyekuwa amesimama hapo akampiga. Mlinzi huyo akasema, “Hupaswi kusema hivyo kwa kuhani mkuu!”

23 Yesu akajibu, “Kama nimesema vibaya jambo lo lote, mwambie kila mtu hapa kosa lenyewe. Lakini kama niliyosema ni sahihi, kwa nini basi unanipiga?”

24 Hivyo Anasi akampeleka Yesu kwa Kayafa kuhani mkuu. Naye alikuwa bado amefungwa.

Petro Amkana Yesu tena

(Mt 26:71-75; Mk 14:69-72; Lk 22:58-62)

25 Simoni Petro alikuwa amesimama karibu na moto, akijipasha joto. Watu wengine wakamwambia Petro, “Je, wewe si mmoja wa wafuasi wa mtu yule?”

Petro alikataa hilo. Akasema, “Hapana, mimi siye.”

26 Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu alikuwapo pale. Naye alikuwa ni jamaa wa mtu yule aliyekatwa sikio na Petro. Mtumishi akamwambia Petro, “Nadhani nilikuona pamoja naye pale kwenye bustani!”

27 Lakini kwa mara nyingine Petro akasema, “Hapana, sikuwa pamoja naye!” Mara tu alipomaliza kusema hayo, jogoo akawika.

Yesu Apelekwa kwa Gavana Pilato

(Mt 27:1-2,11-31; Mk 15:1-20; Lk 23:1-25)

28 Kisha walinzi wakamchukua Yesu kutoka katika nyumba ya Kayafa kwenda kwenye jumba la mtawala wa Kirumi. Nayo ilikuwa ni mapema asubuhi. Wayahudi waliokuwa pale wasingeweza kuingia ndani ya jumba hilo. Wao hawakutaka kujinajisi wenyewe kwa sababu walitaka kuila karamu ya Pasaka. 29 Kwa hiyo Pilato akatoka nje kuwafuata na akawauliza, “Mnasema mtu huyu amefanya makosa gani?”

30 Wakajibu, “Yeye ni mtu mbaya. Ndiyo maana tumemleta kwako.”

31 Pilato akawaambia, “Mchukueni wenyewe na kumhukumu kufuatana na sheria yenu.” Viongozi wa Wayahudi wakamwambia, “Lakini sheria yako haituruhusu sisi kumwadhibu mtu yeyote kwa kumwua.” 32 (Hii ilikuwa ni kuonesha ukweli wa yale aliyosema Yesu juu ya jinsi ambavyo angekufa.)

33 Kisha Pilato alirudi ndani ya jumba lile. Aliagiza Yesu aje na akamuuliza, “Je, wewe ni Mfalme wa Wayahudi?”

34 Yesu akajibu, “Je, hilo ni swali lako mwenyewe au watu wengine wamekuambia juu yangu?”

35 Pilato akajibu, “Mimi sio Myahudi! Ni watu wako mwenyewe na viongozi wa makuhani waliokuleta kwangu. Je, umefanya kosa gani?”

36 Yesu akajibu, “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ungekuwa hivyo, watumishi wangu wangenipigania ili nisikabidhiwe kwa viongozi wa Wayahudi. Hapana, ufalme wangu sio wa kidunia.”

37 Pilato akasema, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?”

Yesu akamjibu, “Uko sahihi unaposema kuwa mimi ni mfalme. Nami nilizaliwa kwa ajili ya hili: kuwaeleza watu juu ya kweli. Ni kwa sababu hii nalikuja ulimwenguni. Kila mmoja aliye wa upande wa kweli hunisikiliza.”

38 Pilato akasema, “Kweli ndiyo nini?” Kisha alitoka nje tena kwenda kwa viongozi wa Wayahudi na kuwaimbia, “Mimi sipati kitu chochote kibaya cha kumpinga mtu huyu. 39 Lakini ni moja ya desturi zenu kwangu mimi kuwafungulia mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Je, mnataka niwafungulie huyu ‘Mfalme wa Wayahudi’?”

40 Wakajibu kwa kupiga kelele wakisema, “Hapana, siyo yeye! Mwache huru Baraba!” (Baraba alikuwa jambazi.)

Footnotes

  1. 18:5 Mimi ni Yesu Kwa maana ya kawaida, “Mimi ndimi”, ambayo inaweza kuwa na maana ile ile hapa kama ilivyo katika 8:24,28,58; 13:19. Pia katika mstari wa 8.
  2. 18:11 kikombe Kikombe ni ishara ya mateso. Yesu alitumia dhana ya kukinywea kikombe akimaanisha kuyakubali mateso ambayo angeyapata katika matukio ya kutisha ambayo yangetokea muda mfupi ujao.
  3. 18:14 mtu mmoja afe Kifo cha Yesu kilikuwa kwa ajili ya watu wote wa ulimwengu siyo kwa Wayahudi peke yao.