Onyo Kuhusu Upendeleo

Ndugu zangu wapendwa, msiwe na upendeleo mnapoishika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu. Tuseme mtu mmoja aliyevaa pete ya dhahabu na nguo maridadi anakuja katika mkutano wenu; kisha fukara mmoja mwenye nguo chafu na mbovu akaingia pia. Ikiwa utamshughulikia zaidi yule mtu aliyevaa nguo maridadi ukamwambia, “Keti hapa kwenye kiti kizuri,” lakini yule fukara ukamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti sakafuni, miguuni pangu,” je, hamtakuwa mmefanya ubaguzi mioyoni mwenu na kutoa hukumu itokanayo na mawazo maovu?

Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa: je, Mungu hakuwachagua wale walio fukara hapa duniani kuwa matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidi wale wampendao? Lakini ninyi mmemvunjia heshima aliye fukara. Je, si matajiri ndio wanaowagandamiza na kuwapelekeni mahakamani? Je, si wao wanaolikufuru jina lile jema mliloitiwa? Kama kweli mnatimiza ile sheria ya kifalme iliyomo katika Maandiko, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe,” mnafanya vema. Lakini kama mnafanya ubaguzi, mna tenda dhambi na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji. 10 Kwa maana mtu ye yote anayetimiza sheria yote isipokuwa akashindwa kutimiza sehemu moja tu, amekuwa na hatia ya kuvunja sheria yote. 11 Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini” ndiye huyo huyo aliyesema, “Usiue.” Kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria yote.

12 Kwa hiyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru. 13 Maana hukumu haina huruma kwa mtu asi yekuwa na huruma. Lakini huruma huishinda hukumu.

Imani Na Matendo

14 Kuna faida gani, ndugu zangu, ikiwa mtu atasema, “Ninayo imani,” na huku hana matendo? 15 Tuseme ndugu fulani au dada hana nguo wala chakula. 16 Ikiwa mmoja wenu atawaambia, “Nendeni salama, mkaote moto na kushiba,” pasipo kuwapatia mahitaji yao ya mwili, kuna faida gani? 17 Vivyo hivyo imani peke yake kama haina matendo, imekufa.

18 Lakini mtu mwingine atasema, “Wewe unayo imani; mimi ninayo matendo.” Nionyeshe imani yako pasipo matendo nami nita kuonyesha imani yangu kwa matendo yangu. 19 Unaamini kuwa kuna Mungu mmoja. Vema. Lakini hata mashetani huamini hivyo, nao hutetemeka!

20 Ewe mpumbavu, unataka ushahidi wa kuthibitisha kwamba imani bila matendo ni bure? 21 Je, Abrahamu baba yetu hakuhesa biwa haki kwa matendo, alipomtoa mwanae Isaki madhabahuni? 22 Unaona jinsi ambavyo imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake na imani ikakamilishwa kwa matendo. 23 Kwa njia hiyo yaka timizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akahesabiwa kuwa mtu mwenye haki”; naye akaitwa rafiki wa Mungu.

24 Mnaona kwamba mtu huhesabiwa haki kwa matendo wala si kwa imani peke yake. 25 Hali kadhalika Rahabu, yule kahaba, yeye je, hakuhesabiwa haki kwa matendo yake alipowapokea wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine? 26 Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika imani pasipo matendo imekufa.

Favoritism Forbidden

My brothers and sisters, believers in our glorious(A) Lord Jesus Christ must not show favoritism.(B) Suppose a man comes into your meeting wearing a gold ring and fine clothes, and a poor man in filthy old clothes also comes in. If you show special attention to the man wearing fine clothes and say, “Here’s a good seat for you,” but say to the poor man, “You stand there” or “Sit on the floor by my feet,” have you not discriminated among yourselves and become judges(C) with evil thoughts?

Listen, my dear brothers and sisters:(D) Has not God chosen those who are poor in the eyes of the world(E) to be rich in faith(F) and to inherit the kingdom(G) he promised those who love him?(H) But you have dishonored the poor.(I) Is it not the rich who are exploiting you? Are they not the ones who are dragging you into court?(J) Are they not the ones who are blaspheming the noble name of him to whom you belong?

If you really keep the royal law found in Scripture, “Love your neighbor as yourself,”[a](K) you are doing right. But if you show favoritism,(L) you sin and are convicted by the law as lawbreakers.(M) 10 For whoever keeps the whole law and yet stumbles(N) at just one point is guilty of breaking all of it.(O) 11 For he who said, “You shall not commit adultery,”[b](P) also said, “You shall not murder.”[c](Q) If you do not commit adultery but do commit murder, you have become a lawbreaker.

12 Speak and act as those who are going to be judged(R) by the law that gives freedom,(S) 13 because judgment without mercy will be shown to anyone who has not been merciful.(T) Mercy triumphs over judgment.

Faith and Deeds

14 What good is it, my brothers and sisters, if someone claims to have faith but has no deeds?(U) Can such faith save them? 15 Suppose a brother or a sister is without clothes and daily food.(V) 16 If one of you says to them, “Go in peace; keep warm and well fed,” but does nothing about their physical needs, what good is it?(W) 17 In the same way, faith by itself, if it is not accompanied by action, is dead.(X)

18 But someone will say, “You have faith; I have deeds.”

Show me your faith without deeds,(Y) and I will show you my faith(Z) by my deeds.(AA) 19 You believe that there is one God.(AB) Good! Even the demons believe that(AC)—and shudder.

20 You foolish person, do you want evidence that faith without deeds is useless[d]?(AD) 21 Was not our father Abraham considered righteous for what he did when he offered his son Isaac on the altar?(AE) 22 You see that his faith and his actions were working together,(AF) and his faith was made complete by what he did.(AG) 23 And the scripture was fulfilled that says, “Abraham believed God, and it was credited to him as righteousness,”[e](AH) and he was called God’s friend.(AI) 24 You see that a person is considered righteous by what they do and not by faith alone.

25 In the same way, was not even Rahab the prostitute considered righteous for what she did when she gave lodging to the spies and sent them off in a different direction?(AJ) 26 As the body without the spirit is dead, so faith without deeds is dead.(AK)

Footnotes

  1. James 2:8 Lev. 19:18
  2. James 2:11 Exodus 20:14; Deut. 5:18
  3. James 2:11 Exodus 20:13; Deut. 5:17
  4. James 2:20 Some early manuscripts dead
  5. James 2:23 Gen. 15:6