Ibada Ya Kiroho

12 Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa sababu ya huruma zake Mungu, jitoeni kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu, ambayo ndio ibada yenu ya kiroho. Msiige tabia na mien endo ya dunia hii bali mbadilishwe, nia zenu zikifanywa kuwa mpya, ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi ya Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na makamilifu.

Kwa sababu ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja wenu: Msijifikirie kuwa watu wa juu kuliko mlivyo. Badala yake, muwe na kiasi katika mawazo yenu, kila mmoja wenu ajipime kutokana na kiasi cha imani aliyopewa na Mungu. Kama vile ambavyo kila mmoja wenu ana mwili mmoja wenye viungo vingi, na kila kiungo kina kazi yake, hali kadhalika, ndani ya Kristo sisi tulio wengi tunakuwa mwili mmoja na kila mmoja wetu ni sehemu ya we ngine wote. Tumepewa vipawa tofauti kulingana na neema tuliy opokea kutoka kwa Mungu. Kama mtu ana kipawa cha kutoa unabii basi akitumie kulingana na imani yake. Kama kipawa chake ni kuwahudumia wengine, basi awahudumie. Kama ni kufundisha, basi na afundishe. Kama kipawa chake ni kuwatia moyo wengine, na afanye hivyo. Kama ni ukarimu, basi na atoe kwa moyo. Mwenye kipawa cha uongozi na afanye hivyo kwa bidii. Mwenye kipawa cha huruma na aonyeshe huruma yake kwa furaha.

Upendo Wa Kweli

Upendo wenu uwe wa kweli. Chukieni uovu, mshikilie yaliyo mema. 10 Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kindugu. Waheshimuni wengine kuliko mnavyojiheshimu wenyewe. 11 Juhudi yenu isipungue, moto wenu wa kiroho uendelee kuwaka mkimtumikia Mungu. 12 Muwe na furaha katika tumaini lenu, na katika dhiki muwe na subira. Ombeni wakati wote. 13 Wasaidieni watu wa Mungu walio na shida. Muwe wakarimu kwa matendo.

14 Waombeeni baraka za Mungu wanaowatesa. Wabarikini wala msiwalaani. 15 Furahini pamoja na wenye furaha; huzunikeni pamoja na wenye huzuni. 16 Muishi kwa amani ninyi kwa ninyi. Msitake makuu bali muwe tayari kushirikiana na wanyonge. Kamwe msiwe watu wenye majivuno.

17 Msimlipe mtu uovu kwa uovu. Jitahidini kutenda yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Kama ikiwezekana, kaeni kwa amani na watu wote. 19 Wapendwa, msijilipizie kisasi, bali mtoe nafasi kwa ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa:“Kisasi ni juu yangu; Mimi nitalipa, asema Bwana. 20 Badala yake, adui yakoakiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kitu anywe. Maana ukifanya hivyo, utampalia mkaa wa moto kichwani pake. 21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Yatoeni Maisha Yenu kwa Mungu

12 Hivyo, dada na kaka zangu, upokeeni wema mkuu ambao Mungu alituonyesha. Itoeni miili yenu[a] kama sadaka hai kwake. Ishini kwa ajili ya Mungu tu na mweze kumpendeza yeye. Mkizingatia kwa makini yale aliyoyatenda, ni sahihi na inapasa kumwabudu Mungu kwa njia hii. Msifikiri au kuenenda kama watu wa ulimwengu huu, bali mruhusuni Mungu aibadilishe namna yenu ya kufikiri ndani yenu. Ndipo mtaweza kuelewa na kuyathibitisha yale Mungu anayotaka kutoka kwenu; yote yaliyo mema, yanayompendeza yeye na yaliyo makamilifu.

Mungu amenipa mimi zawadi maalumu, na ndiyo sababu nina kitu cha kusema na kila mmoja wenu. Msifikiri kuwa ninyi ni bora kuliko jinsi mlivyo kwa asili. Mnapaswa kujiona kadri mlivyo. Mjipime wenyewe jinsi mlivyo kwa imani ambayo Mungu alimpa kila mmoja wetu. Kila mmoja wetu anao mwili mmoja, na mwili huo una viungo vingi. Viungo hivi vyote havifanyi mambo yanayofanana. Kwa jinsi hiyo hiyo, sisi ni watu wengi, lakini kwa sababu ni wa Kristo, sote ni mwili mmoja. Sisi sote ni viungo vya mwili huo, na kila kiungo ni sehemu ya viungo vingine vyote.

Sote tunazo karama tofauti tofauti. Kila karama ilikuja kwa sababu ya neema aliyotupa Mungu. Yule aliye na karama ya unabii anapaswa kuitumia karama hiyo kwa namna inayokubalika kiimani. Aliye na karama ya kuhudumia anapaswa kuhudumia. Aliye na karama ya kufundisha anapaswa kufundisha. Aliye na karama ya kufariji wengine anapaswa kufanya hivyo. Aliye na karama ya kuhudumia mahitaji ya wengine anapaswa kutoa kwa moyo mweupe. Aliye na karama ya kuongoza anapaswa kufanya kwa juhudi katika hiyo. Aliye na karama ya kuonesha wema kwa wengine anapaswa kufanya hivyo kwa furaha.

Upendo wenu unapaswa kuwa halisi. Uchukieni uovu. Fanyeni yaliyo mema tu. 10 Pendaneni ninyi kwa ninyi kama wa familia moja. Na jitahidini kuwa wa kwanza katika kumpa heshima kila mmoja baina yenu. 11 Mnapoendelea kumtumikia Bwana, fanyeni kwa juhudi wala msiwe wavivu. Mchangamke juu ya utumishi wenu kwa Mungu.[b] 12 Mfurahi kwa sababu ya tumaini mlilonalo. Mvumilieni mnapokutana na mateso. Ombeni nyakati zote. 13 Washirikishe ulichonacho watu wa Mungu wanaohitaji msaada. Wakaribisheni katika nyumba zenu wale wanaosafiri au wanaohitaji msaada.

14 Watakieni mema wale wanaowafanyia mabaya. Mwombeni Mungu awabariki, na sio kuwalaani. 15 Furahini pamoja na wanaofurahi. Huzunikeni na wanaohuzunika. 16 Ishini kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, lakini iweni radhi kuwa rafiki wa wasio na umuhimu kwa wengine. Msijihesabu kuwa wenye akili kuliko wengine wote.

17 Mtu akikukosea, usimlipize ubaya. Mjaribu kufanya lile ambalo kila mtu anaona kuwa ni sahihi. 18 Mjitahidi kadri mwezavyo kuishi kwa amani na kila mtu. 19 Rafiki zangu, msijaribu kumwadhibu yeyote anayewakosea. Msubiri Mungu katika hasira yake awaadhibu. Katika Maandiko Bwana anasema, “Nitawaadhibu wao kwa ajili ya yale waliyofanya.”(A) 20 Badala yake,

“ikiwa una adui wenye njaa,
    wapeni chakula wale.
Ikiwa wana kiu,
    wapeni kinywaji wanywe.
Kwa kufanya hivyo mtawafanya wajisikie aibu.”[c](B)

21 Msiruhusu uovu uwashinde, bali ushindeni uovu kwa kutenda mema.

Footnotes

  1. 12:1 Itoeni miili yenu Paulo anatumia lugha ya Agano la Kale kuhusu sadaka ya mnyama kuonesha wazo la waamini kuyatoa maisha yao kwa Mungu kikamilifu.
  2. 12:11 Mchangamke … Mungu Au “Muwe katika moto wa Roho!”
  3. 12:20 mtawafanya wajisikie aibu Au, “Mtakuwa mnawawekea makaa ya moto vichwani mwao.” Mara nyingi, nyakati za Agano la Kale watu waliweka majivu katika vichwa vyao kuonesha huzuni au masikitiko yao.