Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu wa Mungu walioko Laodikia, na kwa ajili ya wengine wote ambao hawajapata kuniona. Shabaha yangu ni kuwa wafarijiwe moyoni na kuunganishwa katika upendo, ili wapate uta jiri wa ufahamu kamili, wajue siri ya Mungu, yaani Kristo; ambaye kwake hupatikana hazina yote ya hekima na maarifa. Nawaambia haya ili mtu ye yote asije akawadanganya kwa maneno ya kuvutia. Maana ingawa mimi niko mbali nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi mnaendelea vizuri na kwamba imani yenu katika Kristo ni imara.

Maisha Kamili Katika Kristo

Basi, kama mlivyompokea Kristo Yesu kuwa Bwana, endeleeni kuishi ndani yake. Muwe na mizizi ndani yake, na kujengwa juu yake; mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa na kububu jika kwa shukrani.

Angalieni mtu ye yote asiwateke kwa falsafa duni na potofu ambazo hutegemea mapokeo ya kibinadamu na mafundisho ya kidunia, na wala si Kristo mwenyewe. Maana, ukamilifu wote wa kimungu umo ndani ya Kristo katika umbile lake la kibinadamu. 10 Nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Kristo, ambaye yeye ni mkuu juu ya kila uwezo na kila mamlaka. 11 Katika Kristo mmetahiriwa kwa kuondolewa hali yenu ya asili ya dhambi. Hii si tohara inayofa nywa kwa mikono ya binadamu bali inafanywa na Kristo. 12 Mli zikwa pamoja naye katika ubatizo na kufufuliwa pamoja naye kwa kuamini uweza wa Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu.

13 Mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya dhambi zenu na kwa sababu ya kutotahiriwa kwa hali yenu ya asili ya dhambi, Mungu aliwafa nya hai pamoja na Kristo. Alitusamehe dhambi zetu zote, 14 baada ya kufuta kabisa hati ya mashtaka iliyokuwa inatukabili na kutu pinga pamoja na masharti yake; aliiondoa akaipigilia msalabani. 15 Na baada ya kuvunja nguvu na mamlaka ya shetani, Mungu alim fedhehesha hadharani kwa kuonyesha ushindi wa msalaba juu yake.

16 Kwa hiyo msimruhusu mtu awahukumu kuhusu chakula au kiny waji, au juu ya kuadhimisha sherehe za dini, sikukuu ya mwezi mpya au siku ya sabato. 17 Maana hizi zilikuwa ni kanuni za muda tu au vivuli vya yale mambo ambayo yangekuja; lakini hakika ya mambo yenyewe ni Kristo. 18 Msikubali kuhukumiwa na mtu ye yote anayejifanya mnyenyekevu na asemaye kwamba ni lazima kuabudu mal aika, mkapoteza tuzo yenu. Mtu kama huyo hufurahia kueleza kwa kirefu maono aliyoona na mawazo yake yasiyo ya kiroho humfanya awe na kiburi. 19 Mtu kama huyo amepoteza uhusiano na Kristo ambaye ni kichwa ambacho kimeunganika na mwili wote na kushika manishwa pamoja kwa mishipa yake na kukua kama Mungu apendavyo.

Kufa Na Kuishi Pamoja Na Kristo

20 Ikiwa mmekufa pamoja na Kristo na hamtawaliwi tena na kanuni za dunia hii, kwa nini bado mnaishi kana kwamba bado mna tawaliwa na masharti ya kidunia? 21 “Usishike hiki! Usionje hiki! Usiguse hiki!” 22 Masharti haya yote hayana budi kuteke tea kwa sababu yanatokana na sheria na mafundisho ya binadamu. 23 Masharti yenyewe yanaonekana kuwa ni ya hekima, maana yana jiwekea namna zake za ibada, unyenyekevu bandia na kuuadhibu mwili. Lakini hayana uwezo wo wote kuzuia tamaa za mwili.

Ninataka mfahamu ni kwa kiwango gani ninawajali ninyi pamoja na ndugu waishio Laodikia na wengine ambao hawajawahi kuniona. Ninataka ninyi nyote pamoja na wao mtiwe moyo na kuunganishwa pamoja katika upendo na kupata uhakika unaoletwa kwa kuielewa ile kweli. Pia, ninataka waijue kweli iliyokuwa siri ambayo sasa imefunuliwa na Mungu. Kweli hiyo ni Kristo mwenyewe. Yeye peke yake ndiye ambaye ndani yake watu wanaweza kupata hazina zote za hekima na ufahamu zilizofichwa katika Kristo.

Nawaambia hili ili asiwepo yeyote atakaye wadanganya kwa maneno na hoja zinazoonekana kuwa ni nzuri, lakini ni mbaya. Ingawa niko mbali kimwili, niko pamoja nanyi katika roho. Ninafurahi kuona jinsi mnavyofanya kazi vizuri pamoja na jinsi imani yenu ilivyo thabiti katika Kristo.

Endeleeni Kumfuata Kristo Yesu

Mlimpokea Kristo Yesu kama Bwana, hivyo mwendelee kumfuata yeye. Na mizizi yenu ikue hata ndani ya Kristo, na maisha yenu yajengwe juu yake. Kama mlivyofundishwa imani ya kweli mwendelee kuwa imara katika ufahamu wenu katika hilo. Na msiache kumshukuru Mungu.

Angalieni msichukuliwe mateka na mafundisho ya uongo kutoka kwa watu wasio na chochote cha maana kusema, bali kuwadanganya tu. Mafundisho yao hayatoki kwa Kristo bali ni desturi za kibinadamu tu na zinatoka katika nguvu za uovu zinazotawala maisha ya watu. Nasema hili kwa sababu Mungu mwenyewe kama alivyo, ukamilifu wa uungu wake unaishi ndani ya Kristo. Hii ni hata wakati wa maisha yake hapa duniani. 10 Na kwa sababu ninyi ni wa Kristo basi mmekamilika, na mna kila kitu mnachohitaji. Kristo ni mtawala juu ya kila nguvu na mamlaka zingine zote.

11 Mlitahiriwa katika Kristo kwa namna tofauti, si kwa mikono ya kibinadamu. Hii ni kusema ya kwamba, mlishiriki katika kifo cha Kristo, ambacho kilikuwa aina ya tohara kwa namna ya kuuvua mwili wake wa kibinadamu.[a] 12 Na mlipobatizwa, mlizikwa na kufufuka pamoja naye kutokana na imani yenu kwa nguvu za Mungu aliyemfufua Kristo kutoka katika kifo.

13 Mlikuwa wafu kiroho kwa sababu ya dhambi zenu na kwa sababu hamkuwa sehemu ya watu wa Mungu.[b] Lakini Mungu amewapa ninyi uhai mpya pamoja na Kristo na amewasamehe dhambi zenu zote. 14 Kwa sababu tulizivunja sheria za Mungu, tunalo deni. Kumbukumbu ya deni hilo imeorodhesha amri zote tulizoshindwa kuzifuata. Lakini Mungu ametusamehe deni hilo. Ameiondoa kumbukumbu yake na kuipigilia msalabani. 15 Pale msalabani, aliwanyang'anya watawala wa ulimwengu wa roho nguvu na mamlaka. Aliwashinda pale. Na akawafukuza kama wafungwa ili ulimwengu wote uone.

Msizifuate Sheria Zilizowekwa na Watu

16 Hivyo msimruhusu mtu yeyote awahukumu katika masuala yanayohusu kula au kunywa au kwa kutofuata desturi za Kiyahudi (kusherehekea siku takatifu, sikukuu za Mwandamo wa Mwezi,[c] au siku za Sabato). 17 Zamani mambo hayo yalikuwa kama kivuli cha yale yaliyotarajiwa kuja. Lakini mambo mapya yaliyotarajiwa kuja yanapatikana katika Kristo. 18 Watu wengine hufurahia kutenda mambo yanayowafanya wajisikie kuwa ni wanyenyekevu na kisha kushirikiana na malaika katika ibada.[d] Nao wanazungumza juu ya kuyaona mambo hayo katika maono. Msiwasikilize wanapowaambia kuwa mnakosea kwa sababu hamfanyi mambo haya. Ni ujinga kwao kujisikia fahari kwa kufanya hivyo, kwa sababu mambo hayo yote yanatokana na namna mwanadamu anavyofikiri. 19 Hawajafungamanishwa na kichwa; Kristo ndiye kichwa, na mwili wote humtegemea Yeye. Kwa sababu ya Kristo viungo vyote vya mwili vinatunzana na kusaidiana kila kimoja na kingine. Hivyo mwili hupata nguvu zaidi na kufungamana pamoja kadri Mungu anavyouwezesha kukua.

20 Mlikufa pamoja na Kristo na kuwekwa huru kutoka katika nguvu zinazotawala dunia. Hivyo kwa nini mnaishi kama watu ambao bado mngali wa ulimwengu? Nina maana kuwa, kwa nini mnafuata sheria hizi: 21 “Usile hiki”, “Usionje kile”, “Usiguse kile”? 22 Sheria hizi zinazungumzia vitu vya kidunia, vitu vinavyotokomea baada ya kutumiwa. Ni amri na mafundisho ya kibinadamu tu. 23 Sheria hizi zinaweza kuonekana za busara kama sehemu ya dini zilizoundwa na watu ambamo watu huiadhibu miili yao na kutenda mambo yanayowafanya wajisikie wanyenyekevu. Lakini sheria hizi haziwasaidii watu kuthibiti tamaa zao za udhaifu wa kibinadamu.

Footnotes

  1. 2:11 mwili wake wa kibinadamu Kwa maana ya kawaida, “katika kuuvua mwili kwenye tohara ya Kristo”. Tazama Tahiri, kutahiriwa, tohara katika Orodha ya Maneno.
  2. 2:13 na kwa sababu … watu wa Mungu Kwa maana ya kawaida, “na kwa sababu ya kutokutahiriwa kwa miili yenu”.
  3. 2:16 Mwandamo wa Mwezi Siku ya kwanza ya Mwezi kwa Waisraeli au Wayahudi, ambayo waliisherehekea kama siku maalum ya kupumzika na kumwabudu Mungu. Walikusanyika pamoja na kutoa sadaka za imani kama zile zinazoainishwa katika Law 7:16-21.
  4. 2:18 malaika katika ibada Au “kuabudu pamoja na malaika” au “huona maono ya malaika”.