Ndugu zangu, mkimwona mtu amenaswa katika dhambi fulani, basi ninyi mnaoongozwa na Roho, mrejesheni mtu huyo kwa upole. Lakini mjihadhari, ili na ninyi msije mkajaribiwa. Chukulianeni mizigo yenu; na kwa njia hiyo mtaweza kutimiza sheria ya Kristo. Mtu akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe siyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe. Lakini, kila mtu apime mwenendo wake, ndipo anaweza kuwa na sababu ya kujisifu bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. Kwa maana, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe. Basi, mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake vitu vyote vilivyo vyema.

Msidanganyike, Mungu hadanganywi. Kwa maana kila mtu ata vuna kile alichopanda. Mtu apandaye katika tamaa za mwili, ata vuna kutoka katika mwili uharibifu; lakini yeye apandaye katika Roho, atavuna kutoka katika Roho uzima wa milele. Basi, tusi choke kutenda mema, kwa sababu kama hatukuchoka tutavuna kwa wakati wake. 10 Kwa hiyo basi, kadiri tunavyopata nafasi, tuwa tendee mema watu wote, na hasa wale tunaoshiriki imani moja.

Maonyo Ya Mwisho Na Salamu

11 Tazameni jinsi maandishi ya mkono wangu mwenyewe yalivyo makubwa. 12 Ni wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaowalazimisheni mtahiriwe; na wanafanya hivyo ili wao wenyewe wasije kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo. 13 Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawashiki sheria; lakini wanataka na ninyi mtahiriwe ili wapate kujivunia hiyo alama katika miili yenu. 14 Lakini mimi kamwe sitajivunia kitu cho chote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; kwa maana kwa njia ya msalaba, ulimwengu umesulubiwa kwangu, na mimi nimesulubiwa kwa ulimwengu. 15 Kwa maana, kutahiriwa au kutota hiriwa si kitu kwangu; kitu cha maana ni maisha ya watu kubadili ika kuwa mapya. 16 Amani na rehema ya Mungu ikae na wote wanao fuata kanuni hii, na kwa Israeli ya kweli ya Mungu.

17 Basi, tangu sasa mtu ye yote asije akanisumbua, kwa sababu ninazo alama za Yesu mwilini mwangu.

Tuishi kwa Kusaidiana Sisi kwa Sisi

Ndugu zangu, ikiwa mmoja wenu atakosea, ninyi mnaomfuata Roho mnapaswa kumwendea yule anayetenda dhambi. Msaidieni mtu huyo awe mwenye haki tena. Mfanye hivyo kwa njia ya upole, na muwe waangalifu, kwa maana nanyi pia mnaweza kujaribiwa kutenda dhambi. Msaidiane ninyi kwa ninyi katika kubeba mizigo yenu. Mnapofanya hivi, mtakuwa mnatimiza yote ambayo sheria ya Kristo imewaagiza kufanya. Maana mtu akijiona kuwa yeye ni wa muhimu sana na kumbe sio wa muhimu, anajidanganya mwenyewe. Kila mmoja aipime kazi yake mwenyewe kuona ikiwa kuna chochote cha kujivunia. Kama ndivyo, uyatunze hayo moyoni mwako wala usijilinganishe na mtu mwingine yeyote. Maana sisi sote tunawajibika kwa yale tunayofanya.

Msiache Kutenda Mema

Yule anayefundishwa neno la Mungu anapaswa kumshirikisha mwalimu wake mambo mema aliyonayo.

Ikiwa mnadhani mnaweza kumdanganya Mungu, mtakuwa mnajidanganya wenyewe. Mtavuna yale mnayopanda. Yule anayepanda kwa kuiridhisha nafsi yake ya dhambi, mavuno yatakayopatikana ni uharibifu kabisa. Lakini mkipanda kwa kuiridhisha Roho, mavuno yenu katika Roho yatakuwa uzima wa milele. Hatupaswi kuchoka katika kutenda mema. Tutapata mavuno yetu kwa wakati sahihi, tusipokata tamaa. 10 Tunapokuwa na nafasi ya kumtendea mema kila mtu, tufanye hivyo. Lakini tuzingatie zaidi kuwatendea mema wale walio wa familia ya waamini.

Paulo Amalizia Barua Yake

11 Huu ni mwandiko wa mkono wangu mwenyewe. Mnaweza kuona jinsi herufi zilivyo kubwa.[a] 12 Watu wale wanaojaribu kuwalazimisha ninyi kutahiriwa wanafanya hivyo ili wawaridhishe Wayahudi wenzao. Wanaogopa wasije wakateswa kwa sababu ya msalaba[b] wa Kristo. 13 Maana hata wale waliotahiriwa hawaitii sheria. Na bado wanawataka ninyi mtahiriwe ili waweze kujisifu kwa ajili ya yale waliyowatendea ninyi.

14 Mimi nisijisifu kwa ajili ya mambo kama haya. Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo ndiyo sababu pekee ya kujivuna kwangu. Kupitia kifo cha Yesu msalabani ulimwengu ukafa[c] kwangu, nami nimeufia ulimwengu. 15 Haijalishi kwamba mtu ametahiriwa au hajatahiriwa. Kinachojalisha ni uumbaji mpya wa Mungu katika Kristo.[d] 16 Amani iwe kwa wale wote wanaoifuata njia hii mpya. Na rehema za Mungu ziwe juu ya watu wake Israeli.

17 Kwa hiyo msinitaabishe kwa namna yoyote. Nina makovu mwilini mwangu yanayoonyesha[e] kuwa mimi ni wa Yesu.

18 Ndugu na dada zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amina.

Footnotes

  1. 6:11 Sasa Paulo amechukua kalamu kutoka kwa mwandishi/katibu wake ili mwenyewe aandike sehemu ya mwisho ya barua. Herufi kubwa labda inawezekana ni kwa ajili ya kusisitiza muhtasari unaofuata wa hoja zake kuu, kama vile unapotumia wino mzito au kwa herufi kubwa leo.
  2. 6:12 msalaba Paulo anatumia msalaba kama kielelezo cha Habari Njema, habari ya kifo cha Kristo kwa ajili ya kuwaweka watu huru mbali na dhambi. Msalaba (Kifo cha Kristo) kilikuwa njia ya Mungu ya kuwaokoa watu. Pia katika mstari wa 14.
  3. 6:14 ukafa Kwa maana ya kawaida, “umesulubishwa”.
  4. 6:15 uumbaji mpya wa Mungu katika Kristo Kwa maana ya kawaida, “kiumbe kipya”. Tazama 2 Kor 5:17.
  5. 6:17 makovu … yanayoonyesha Mara nyingi Paulo alikuwa anapigwa na watu waliokuwa wanajaribu kumzuia kufundisha kuhusu Kristo. Makovu yalitokana na mapigo hayo.