Paulo Akubaliwa Na Mitume

Kisha, baada ya miaka kumi na minne, nilikwenda tena Yeru salemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito ili awe pamoja nami. Nilikwenda kwa sababu nilikuwa nimefunuliwa na Mungu, kwamba nikawaeleze kwa faragha wale waliokuwa viongozi, Injili ninayohubiri kwa watu wa mataifa mengine. Nilifanya hivyo ili kazi yangu niliyokwisha fanya na hii ninayofanya sasa isije ikawa bure. Hata hivyo Tito ambaye alikuwa ni Mgiriki, hakulazimika kutahiriwa. Lakini walikuwepo ndugu wengine wa uongo ambao walikuja kwa siri kupeleleza uhuru tulio nao katika Kristo Yesu, ili waturudishe kwenye utumwa wa sheria. Sisi hatukukubaliana nao hata kidogo ili ukweli wa Injili uendelee kutunzwa kwa ajili yenu. Lakini wale ambao walionekana kuwa viongozi wao, mimi sijui wala sijali kama walikuwa na vyeo gani, kwa sababu Mungu haangalii cheo cha mtu; nasema kwamba hao watu hawakuongezea cho chote katika ujumbe wangu. Badala yake walitambua kwamba Mungu alikuwa amenipa kazi ya kuhubiri Injili kwa watu wa mataifa mengi ne kama vile Petro naye alivyotumwa kuhubiri Injili kwa Wayahudi. Kwa maana ilikuwa dhahiri kwamba Mungu aliyemwezesha Petro kuwa mtume kwa Wayahudi ndiye aliyekuwa akifanya kazi katika huduma yangu kama mtume kwa watu wa mataifa mengine. Basi, Yakobo, Kefa na Yohana, ambao walikuwa nguzo za kanisa, walipotambua kwamba Mungu alikuwa amenijalia neema yake, walitushika mikono, mimi na Barnaba, kama ishara ya ushirikiano wetu. Walikubaliana kwamba sisi twende kwa watu wa mataifa mengine na wao waende kwa Wayahudi. 10 Walichotuomba ni kwamba katika huduma yetu tuende lee kuwasaidia maskini; jambo ambalo nimekuwa nikijitahidi kufa nya.

Paulo Anampinga Petro

11 Lakini Petro alipofika Antiokia, mimi nilimpinga hadhar ani kwa kuwa alikuwa amekosea. 12 Kwa sababu kabla ya watu kadhaa waliotoka kwa Yakobo hawajafika, alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini baada ya hao watu kufika ali ji tenga, akaacha kula pamoja na watu wa mataifa mengine, kwa kuwaogopa wale wa kundi la tohara. 13 Pia Wayahudi wengine wal iungana naye katika unafiki huu, hata Barnaba naye akashawishika kuwaunga mkono.

14 Nilipoona kwamba msimamo wao kuhusu ukweli wa Injili hau kuwa wazi, nilimwambia Petro mbele za watu wote, “Ikiwa wewe uliye Myahudi unaishi kama watu wa mataifa, na huishi kama Myahudi, unawezaje kuwalazimisha watu wa mataifa mengine waishi kama Wayahudi?” Habari Njema Aliyohubiri Paulo

15 Sisi tulio Wayahudi wa kuzaliwa na sio watu wa mataifa ‘wenye dhambi,’ 16 tunafahamu kwamba mtu hawezi kuhesabiwa haki kwa kutii sheria bali kwa kumwamini Yesu Kristo. Kwa hiyo sisi pia tumemwamini Yesu Kristo ili tupate kuhesabiwa haki kwa kumwa mini Kristo, na wala si kwa kuitii sheria. Maana hakuna mtu ata kayehesabiwa haki kwa kutii sheria. 17 Lakini ikiwa sisi katika jitihada ya kuhesabiwa haki katika Kristo, bado tunaonekana tun gali wenye dhambi, je, hii ina maana kwamba Kristo amekuwa mwene zaji wa dhambi? La hasha! 18 Lakini ikiwa mimi nina jenga tena kile ambacho nimekwisha bomoa, basi ninadhihirisha kwamba mimi ni mvunja sheria. 19 Kwa maana mimi kwa njia ya sheria, nimeifia sheria, ili nipate kuishi kwa ajili ya Mungu. 20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; si mimi tena ninayeishi bali ni Kristo anayeishi ndani yangu. Maisha ninayoishi sasa naishi kwa kumwa mini Mwana wa Mungu, aliyenipenda hata akatoa maisha yake kwa ajili yangu. 21 Siwezi nikadharau neema ya Mungu; kwa maana kama haki ingeweza kupatikana kwa kutimiza sheria, basi Kristo alikufa bure.

Mitume Wengine Wamkubali Paulo

Baada ya miaka 14 nilirudi tena Yerusalemu nikiwa na Barnaba na nilimchukua Tito pia. Nilikwenda kule maana Mungu alinionyesha kuwa ninapaswa kwenda. Niliwafafanulia Habari Njema kama nilivyoihubiri kwa watu wasio Wayahudi. Pia nilikutana faragha na wale waliokuwa wanatazamiwa kuwa viongozi. Nilitaka niwe na uhakika kuwa tulikuwa tunapatana ili kazi yangu ya nyuma na ile niliyokuwa naifanya sasa zisipotee bure.

Tito, aliyekuwa pamoja nami ni Myunani. Hata hivyo viongozi hawa hawakulazimisha kumtahiri. Tulihitaji kuyazungumzia matatizo haya, kwa sababu wale waliojifanya kuwa ni ndugu zetu walikuja kwenye kundi letu kwa siri. Waliingia kama wapelelezi kutafiti kuhusu uhuru tuliokuwa nao ndani ya Kristo Yesu. Walitaka watufanye sisi watumwa, lakini hatukujiweka chini ya chochote ambacho hawa ndugu wa uongo walikitaka. Tulitaka ukweli wa Habari Njema ubaki ule ule na hatimaye uwafikie na ninyi.

Na watu wale ambao walihesabiwa kuwa viongozi muhimu hawakuongeza lolote katika ujumbe wa Habari Njema niliyowahubiria watu. (Haijalishi kwangu kuwa walikuwa wa “muhimu” au la. Kwa Mungu binadamu wote ni sawa.) Lakini viongozi hawa waliona kuwa Mungu alinipa kazi maalumu ya kuhubiri Habari Njema kwa wasio Wayahudi, kama vile alivyomwagiza Petro[a] kufanya kazi hiyo hiyo ya kuhubiri Habari Njema miongoni mwa Wayahudi. Mungu alimpa Petro uwezo wa kufanya kazi kama mtume lakini kwa walio Wayahudi. Mungu akanipa mimi pia uwezo wa kufanya kazi kama mtume, lakini kwa wasiokuwa Wayahudi. Yakobo, Petro na Yohana walikuwa viongozi muhimu kanisani. Hawa wakaona kuwa Mungu alinipa kipaji hiki maalumu cha huduma, hivyo wakatupa mkono wa shirika mimi pamoja na Barnaba. Wakakubali kuwa sisi tutaendelea kufanya kazi miongoni mwao wasio Wayahudi, na wao wataendelea kufanya kazi miongoni mwao walio Wayahudi. 10 Wakatuomba jambo moja tu, ya kwamba tukumbuke kuwahudumia waaminio walio maskini.[b] Na kwa hakika hili lilikuwa jambo nililojitahidi kufanya.

Paulo Aonesha Kuwa Petro Alikosea Kule Antiokia

11 Petro alipokuja Antiokia, alifanya kitu ambacho hakikuwa sahihi. Nami nikampinga, kwa sababu hakika alikuwa na hatia mbele za Mungu. 12 Hivi ndivyo ilivyotokea: Petro alipokuja Antiokia, hapo awali kabla ya Wayahudi kufika, alikula na kujumuika na wasio Wayahudi. Lakini baada ya Wayahudi kufika kutoka kwa Yakobo, Petro akajitenga na wasio Wayahudi. Akaacha kula pamoja nao kwa sababu aliwaogopa Wayahudi. 13 Hivyo Petro akafanya kama mnafiki, na waamini wengine pale Antiokia wakaungana naye katika unafiki huo. Wakamfanya hata Barnaba naye kuwa mnafiki kama wao. 14 Hawakuwa wakiifuata kweli ya Habari Njema. Nilipoona hili, nilimweleza Petro mbele ya kila mtu. Nilisema, “Petro, wewe ni Myahudi, lakini huenendi kama Myahudi. Unaenenda kama mtu asiye Myahudi. Hivyo kwa nini unajaribu kuwalazimisha wale wasio Wayahudi kuenenda kama Wayahudi?

15 Sisi ni Wayahudi kwa kuzaliwa. Hatukuzaliwa tukiwa ‘watenda dhambi’, kama vile Wayahudi wanavyowaita wale wasio Wayahudi. 16 Lakini tunajua kuwa hakuna mtu anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kuifuata sheria. Ni kwa kuamini katika[c] Yesu Kristo ndiko kunamfanya mtu ahesabiwe haki mbele za Mungu. Hivyo hata nasi Wayahudi tumeiweka imani yetu katika Kristo Yesu, kwa sababu tulitaka kuhesabiwa haki mbele za Mungu. Na tumehesabiwa haki kwa imani[d] ya Yesu Kristo, siyo kwa sababu tuliifuata sheria. Naweza kusema hili kwa sababu hakuna anayeweza kuhesabiwa haki kwa kuifuata Sheria ya Musa.

17 Kwa hiyo tunaamini uhusiano wetu kwa Kristo utatufanya tuhesabiwe haki mbele za Mungu. Ikiwa hiyo inatufanya tuonekane kama ‘watenda dhambi’ wasio Wayahudi, je itakuwa na maana kuwa Kristo anasababisha dhambi kuongezeka. Kwa hakika sivyo? 18 Sheria ilijenga ukuta baina yetu Wayahudi na watu wengine wote, ukuta ambao nilijitahidi kuuvunja. Kweli nitakosea sana kuujenga tena ukuta huo. 19 Sheria yenyewe iliyafikisha mwisho maisha yangu chini ya sheria. Nikafa katika sheria hiyo na kuwa huru ili niweze kuishi kwa ajili ya Mungu. Nimepigiliwa misumari msalabani pamoja na Kristo. 20 Hivyo siyo mimi ninayeishi sasa; ni Kristo ndiye anayeishi ndani yangu. Bado naishi katika mwili wangu, lakini naishi kwa imani katika Mwana wa Mungu aliyenipenda na kujitoa mwenyewe kuniokoa mimi. 21 Si mimi ninayeikataa neema ya Mungu kama vile haina manufaa yoyote. Kwa sababu ikiwa kwa kuifuata sheria ndivyo watu wanahesabiwa haki mbele za Mungu, basi Kristo alikufa pasipo faida!”

Footnotes

  1. 2:7 Petro Jina la Kefa limetumika badala ya Petro katika nakala za kale za Kiyunani. Pia katika mstari wa 11.
  2. 2:10 waaminio walio maskini Maskini wanaozungumziwa hapa ni wale waliokuwemo miongoni mwa waamini katika kanisa la Yerusalemu.
  3. 2:16 kuamini katika Au “uaminifu wa”.
  4. 2:16 tumehesabiwa haki kwa imani Au “kupitia uaminifu wa”.