Kutoka kwa Paulo, mtume niliyetumwa, si kutoka kwa watu wala sikuchaguliwa na mwanadamu, bali nimetumwa na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu. 0 Nawahakikishieni mbele za Mungu kuwa ninayowaandikieni si uongo.

Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye alijitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa kutoka katika nyakati hizi za uovu. Yeye apewe utukufu milele na milele. Amina.

Nashangaa kuona kwamba mnamwacha upesi hivyo yule aliye waita kwa neema ya Kristo mkaanza kufuata Injili nyingine. Ukweli ni kwamba hakuna Injili nyingine, ila nafahamu kuwa wako watu wanaowavuruga, ambao wanataka kuipotosha Injili ya Kristo. Lakini hata ikiwa ni sisi au ni malaika atokaye mbinguni, kama mtu akiwahubiria Injili ambayo ni tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo na alaaniwe. Kama tulivyokwisha sema kabla, sasa nasema tena, kwamba mtu ye yote atakayewahubiria Injili tofauti na ile mliyokwishaipokea, basi mtu huyo na alaaniwe.

10 Je, sasa mimi nataka nipate upendeleo kutoka kwa bina damu au kutoka kwa Mungu? Au nataka niwapendeze watu? Kama ningekuwa najaribu kuwapendeza watu, nisingekuwa mtumishi wa

Wito Wa Paulo

11 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba Injili niliyo wahubi ria siyo Injili ya binadamu. 12 Kwa maana mimi sikuipokea Injili kutoka kwa binadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali nili pata mafunuo moja kwa moja kutoka kwa Yesu Kristo. 13 Ninyi mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi; jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu na kujaribu kuliangamiza. 14 Nami niliwashinda wengi miongoni mwa Wayahudi wenzangu kwa maana nilikuwa nimejawa na juhudi ya kushika mapo keo ya baba zetu. 15 Lakini yeye aliyenichagua hata kabla sijazaliwa na akaniita kwa neema yake, 16 alipopenda kumdhihiri sha Mwanae kwangu ili nimhubiri miongoni mwa watu wa mataifa, sikushauriana na mtu ye yote. 17 Sikwenda kwanza Yerusalemu kuonana na wale waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda Arabuni, ndipo nikarudi Dameski. 18 Kisha baada ya miaka mitatu nilikwenda Yerusalemu kuo nana na Kefa na nilikaa naye siku kumi na tano. 19 Lakini siku waona wale mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. 21 Baadaye nilikwenda sehemu za Siria na Kilikia. 22 Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa wakristo wa makanisa ya huko Uyahudi. 23 Ila walisikia wengine wakisema, “Yule mtu ambaye zamani alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akitaka kuiangamiza.” 24 Kwa hiyo wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.

Salamu kutoka kwa mtume Paulo. Sikutumwa na kundi lolote la watu au mtu yeyote hapa duniani niwe mtume. Sikupewa mamlaka yangu na mwanadamu yeyote. Nilipewa mamlaka haya moja kwa moja kutoka kwa Kristo Yesu[a] na Mungu Baba, aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu. Salamu pia kutoka kwa wote walio familia ya Mungu, walio pamoja nami.

Kwa makanisa yaliyoko Galatia:[b]

Namwomba Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo awe mwema kwenu na awape neema na amani. Yesu alijitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu ili atuweke huru kutoka katika uovu wa ulimwengu huu tunamoishi. Hili ndilo Mungu Baba yetu alitaka. Mungu Baba yetu anastahili utukufu milele na milele! Amina.

Kuna Ujumbe Mmoja tu wa Habari Njema

Wakati mfupi tu uliopita Mungu aliwaita mkamfuata. Aliwaita katika neema yake kwa njia ya Kristo. Lakini sasa nashangazwa kwamba kwa haraka hivi mmegeuka mbali na kuamini kitu kingine tofauti kabisa na Habari Njema tuliyowahubiri. Hakuna ujumbe mwingine wa Habari Njema, lakini baadhi ya watu wanawasumbua. Wanataka kuibadili Habari Njema ya Kristo. Tuliwahubiri ninyi ujumbe wa Habari Njema tu. Hivyo laana ya Mungu impate mtu yeyote yule anayewahubiri ninyi ujumbe ulio tofauti, hata ikiwa ni mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni! Nitalisema tena lile nililolisema hapo mwanzo. Ninyi mmekwishaipokea Habari Njema. Yeyote atakayewahubiri kitu kingine tofauti na ile Habari Njema mliyoipokea, basi mjue kwamba Mungu atamlaani mtu huyo!

10 Sasa mnafikiri ninajaribu kuwapendeza wanadamu? Hapana, ninataka kumpendeza Mungu siyo wanadamu. Kama ningekuwa najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumwa wa Kristo.

Mamlaka ya Paulo ni Kutoka kwa Mungu

11 Ndugu zangu, ninawataka mjue kuwa ujumbe wa Habari Njema niliowaambia haukuandaliwa na mtu yeyote. 12 Sikuupata ujumbe wangu kutoka kwa mwanadamu yeyote. Habari Njema siyo kitu nilichojifunza kutoka kwa watu. Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyenifunulia Habari Njema ninayowahubiri watu.

13 Mmesikia juu ya mwenendo wangu hapo zamani nilipokuwa mfuasi hodari wa dini ya Kiyahudi. Nililitesa kwa nguvu kanisa la Mungu, nikiwa na shabaha ya kuliangamiza kabisa. 14 Nilipata maendeleo makubwa katika dini ya Kiyahudi kwa kufanya kazi na kusoma kwa bidii kwa sababu nilikuwa mwaminifu kwa desturi za baba zetu.

15 Lakini Mungu alikuwa na mpango maalumu kwa ajili yangu hata kabla sijazaliwa.[c] Hivyo aliniita kwa neema yake. Na ilimpendeza 16 kumfunua Mwanaye ili niweze kuwahubiri Habari Njema watu wasio Wayahudi. Hicho ndicho nilichofanya baada ya hapo. Sikuomba ushauri ama msaada wowote kutoka kwa mtu yeyote. 17 Sikwenda Yerusalemu kuwaona wale waliokuwa mitume kabla mimi sijawa mtume. Badala yake, kwanza nilienda moja kwa moja Arabia. Kisha baadaye, nikarudi katika mji wa Dameski.

18 Miaka mitatu baadaye nilikwenda Yerusalemu kumwona Petro.[d] Nilikaa naye kwa siku 15. 19 Sikuonana na mtume mwingine yeyote, isipokuwa Yakobo mdogo wake Bwana peke yake. 20 Mungu anajua kuwa hakuna ninachowaandikia kisicho cha kweli. 21 Baadaye, nilielekea katika majimbo ya Shamu na Kilikia.

22 Lakini kwa wakati ule, makanisa ya Kristo yaliyokuwa Uyahudi yalikuwa bado hayajanifahamu mimi binafsi. 23 Walikuwa wamesikia tu juu yangu: “Mtu huyu alikuwa anatutesa. Lakini sasa anawaambia watu juu ya imani ile ile aliyojaribu kuiangamiza huko nyuma.” 24 Waamini hawa walimsifu Mungu kwa sababu yangu.

Footnotes

  1. 1:1 Kristo Yesu Au “Mfalme Yesu”. Neno “Kristo” ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania “Masihi”, ambao ni wadhifa wa kifalme. Tazama Mk 15:32: Lk 23:2. Tazama pia Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno.
  2. 1:2 Galatia Yamkini ni eneo ambako Paulo alianzisha makanisa katika safari yake ya kwanza ya kitume. Soma Mdo 13 na 14. Au katika safari yake ya pili ya kitume katika Mdo 16:6.
  3. 1:15 Tazama Isa 49:1; Jer 1:5.
  4. 1:18 Petro Kwa maana ya kawaida, “Kefa”, jina la Kiaramu la Petro, mmoja wa mitume kumi na wawili wa Yesu. Majina yote mawili yanamaanisha “mwamba”. Pia katika 2:9,11,14.