Muwe Na Umoja, Furaha Na Amani

Kwa hiyo ndugu zangu wapendwa, ninaotamani mno kuwaona; ninyi ambao ni furaha yangu na taji yangu, hivi ndivyo mnavyop aswa kusimama imara katika Bwana. Nawasihi Euodia na Sintike wapatane katika Bwana. Na wewe ndugu yangu uliye mwaminifu katika Bwana, nakuomba uwasaidie hawa akina mama, kwa maana wame fanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii wakiwa nami pamoja na Kle menti na watumishi wenzangu wengine, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.

Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! Upole wenu ufahamike kwa watu wote. Bwana anakaribia kuja. Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu.

Hatimaye ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo na sifa, yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo uzuri wo wote, pakiwepo na cho chote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. Mambo yote mliyojifunza au kupokea au kusikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatekelezeni. Na Mungu wa amani ata kuwa pamoja nanyi. 10 Nina furaha kubwa katika Bwana kwa maana hatimaye mmeanza tena kunikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikum buka lakini mlikuwa hamjapata nafasi ya kuonyesha upendo wenu. 11 Sisemi hivyo kwa sababu nahitaji kitu, la. Kwa maana nimeji funza kuridhika katika hali yo yote niliyo nayo. 12 Nimepata kupungukiwa, pia nimepata kuwa na wingi wa vitu. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa shibe na wakati wa njaa; wakati wa kuwa na wingi wa vitu na wakati wa kupungukiwa. 13 Naweza kufanya mambo yote katika yeye anipaye nguvu.

14 Hata hivyo, mlifanya vizuri kunisaidia kwa kushirikiana nami katika taabu zangu. 15 Ninyi ndugu zangu Wafilipi mnajua kwamba nilipoanza kuhubiri Injili, nilipokuwa natoka Makedonia, hakuna kanisa lililoshirikiana nami katika kutoa na kupokea isi pokuwa ninyi. 16 Hata nilipokuwa Thesalonike, mliniletea msaada zaidi ya mara moja. 17 Msifikiri kwamba napenda sana kupokea zawadi, sivyo. Ninachotaka kuona ni matunda ambayo kama yak iongezeka ni faida kwenu. 18 Nimekwishapokea malipo yangu yote na ziada. Sasa ninavyo vitu tele kwa sababu Epafrodita amekwisha niletea zawadi zenu. Hakika zawadi hizi ni matoleo yenye harufu nzuri ya manukato inayokubaliwa na kumpendeza Mungu. 19 Na Mungu wangu atawapeni ninyi kila kitu mnachohitaji kwa kadiri ya uta jiri wake mtukufu katika Kristo Yesu. 20 Mungu wetu na Baba yetu apewe utukufu milele na milele. Amina. 21 Natuma salamu zangu kwa kila mtu wa Mungu katika Kristo Yesu. Ndugu ninaokaa nao pia wanawasalimu. 22 Vile vile watu wote wa Mungu wa hapa na hasa wale wa nyumba ya Kaisari, nao pia wanawasalimu.

Maagizo ya Mwisho

Kaka na dada zangu wapenzi, ninawapenda na ninataka kuwaona. Mnanifurahisha na ninajivuna kwa sababu yenu. Endeleeni kuwa imara kumfuata Bwana kama nilivyowaambia.

Ninawasihi Euodia na Sintike, ninyi nyote wawili ni wa Bwana, hivyo muwe na mtazamo mmoja. Kwa ajili ya hili ninamwomba rafiki yangu aliyetumika pamoja nami kwa uaminifu: Wasaidieni wanawake hawa. Waliwahubiri watu Habari Njema kwa bidii kama watendaji wenzangu tukiwa pamoja na Klementi na wengine waliofanya kazi pamoja nami. Majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.[a]

Furahini katika Bwana daima. Ninasema tena, furahini.

Kila mtu auone wema na uvumilivu wenu. Bwana yu karibu kuja. Msisumbuke kitu chochote, lakini salini na kumwomba Mungu kwa mahitaji yenu. Mshukuruni Mungu wakati mnapomwomba yale mnayohitaji. Na kwa kuwa ninyi ni milki ya Kristo Yesu, amani ya Mungu itailinda mioyo na mawazo yenu isipate wasiwasi. Amani yake inaweza kutenda haya zaidi ya akili za kibinadamu.[b]

Na sasa, mwisho kabisa, kaka na dada zangu, fikirini kuhusu yale yaliyo ya kweli, ya kuheshimiwa, ya haki, yaliyo safi, yenye kupendeza, na yanayosemwa vema. Yatendeni yale mliyojifunza na kupokea kutoka kwangu, niliyowaambia na yale mliyoyaona nikitenda. Na Mungu atoaye amani atakuwa pamoja nanyi.

Paulo Apokea Zawadi Kwa Furaha

10 Nimefurahi sana katika Bwana kwa sababu mmeonesha tena kuwa mnanijali. Mmeendelea kujali juu yangu, lakini haikuwepo njia ya kuonesha hili. 11 Ninawaambia hili, si kwa sababu ninahitaji msaada kutoka kwa yeyote. Nimejifunza kuridhika na kile nilichonacho na chochote kinachotokea. 12 Ninajua namna ya kuishi ninapokuwa na vichache na ninapokuwa na vingi. Nimejifunza siri ya kuishi katika hali zote, ninapokuwa na vyakula vingi au ninapokuwa na njaa, ninapokuwa na vingi zaidi ya ninavyohitaji au ninapokuwa sina kitu. 13 Kristo ndiye anayenitia nguvu kuyakabili mazingira yote katika maisha.

14 Lakini mlifanya vyema mliposhiriki nami katika kipindi changu kigumu. 15 Enyi watu wa Filipi kumbukeni nilipokuja mara ya kwanza kuwahubiri Habari Njema watu wa Makedonia. Nilipoondoka huko, ninyi ndiyo kanisa pekee ambalo lilishirikiana nami katika uhusiano ulioendelea wa kutoa na kupokea. 16 Ukweli ni kuwa hata nilipokuwa Thesalonike, zaidi ya mara moja mlinitumia kila kitu nilichohitaji. 17 Si kwamba natafuta msaada wa kifedha kutoka kwenu. Bali ninataka ninyi mpokee manufaa yanayozidi kukua yanayotokana na kutoa. 18 Nina kila kitu ninachohitaji. Nina zaidi ya hata ninavyohitaji kwa sababu Epafrodito ameniletea kila kitu mlichompa aniletee. Zawadi zenu ni kama sadaka yenye harufu nzuri inayotolewa kwa Mungu. Ni sadaka anayoikubali, na inampendeza. 19 Mungu wangu atatumia utajiri wake wenye utukufu kuwapa ninyi kila kitu mnachohitaji kupitia Kristo Yesu. 20 Utukufu kwa Mungu na Baba yetu milele na milele. Amina.

21 Wasalimuni watakatifu wote wa Mungu walio wake Kristo Yesu. Wale walio katika familia ya Mungu walio pamoja nami wanawasalimu. 22 Na watu wote wa Mungu walio hapa wanawasalimu, hasa wale walio katika utumishi wa Kaisari.

23 Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na utu wenu wa ndani.

Footnotes

  1. 4:3 kitabu cha uzima Kitabu cha Mungu chenye majina ya wateule wake. Tazama Ufu 3:5; 21:27.
  2. 4:7 kutenda … kibinadamu Yaani, “Inazidi (ni bora kuliko) akili zote”. Hii inaweza kumaanisha pia kuwa “Ni zaidi ya uelewa wote.”