Kuzingatia Mafundisho

Kwa hiyo, hatuna budi kuzingatia kwa makini mambo tuliyof undishwa tusije tukatanga-tanga mbali na yale tuliyosikia. Kwa maana kama ujumbe ulioletwa na malaika ulithibitika kuwa kweli, na kila aliyeasi na kutokutii akaadhibiwa ilivyostahili, sisi je? Tutaepukaje kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu kwanza ulitangazwa na Bwana, na ulithibitishwa kwetu na wale wal iomsikia. Mungu pia aliushuhudia kwa ishara na miujiza na maaj abu mbalimbali, pamoja na karama za Roho Mtakatifu alizogawa kufuatana na mapenzi yake.

Wokovu Umeletwa Na Kristo

Maana Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, tunaouzungumzia, chini ya mamlaka ya malaika. Bali kama inavyothibitishwa katika sehemu fulani ya Maandiko, “Mwanadamu ni kitu gani hata umfi kirie, au mwana wa binadamu ni nani hata umjali? Umemfanya kuwa chini kidogo ya malaika; wewe umemvika taji ya utukufu na heshima, umemfanya kuwa mtawala wa vitu vyote.” Mungu ali poweka vitu vyote chini ya mamlaka ya mwanadamu, hakubakiza cho chote ambacho mwanadamu hakitawali. Lakini kwa wakati huu hatuoni kama kila kitu kiko chini ya mamlaka yake. Lakini tunamwona Yesu, ambaye kwa muda mfupi alifanywa kuwa chini kidogo ya mal aika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu aliteseka na kufa, ili kwa neema ya Mungu, aonje mauti kwa ajili ya watu wote.

10 Kwa maana ilikuwa ni sawa kabisa kwamba Mungu, ambaye kwa ajili yake na kwa uweza wake vitu vyote vimekuwepo, amfanye Mwan zilishi wa wokovu wao kuwa mkamilifu kwa njia ya mateso, ili awalete wana wengi washiriki utukufu wake. 11 Maana yule anayetakasa na wale wanaotakaswa, wote wanatoka katika uzao mmoja. 12 Ndio maana Yesu haoni aibu kuwaita wao ndugu zake, akisema: “Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katikati yao nitakusifu.” 13 Na tena anasema, “Nitamwekea Mungu tumaini langu.” Na tena, “Niko hapa, mimi pamoja na watoto niliopewa na Mungu.”

Mungu.”

14 Basi, kwa kuwa watoto hao wana mwili na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kufa kwake apate kumwan gamiza yule mwenye mamlaka juu ya kifo, yaani shetani; 15 na hivyo awaweke huru wale ambao walikuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa kifo. 16 Maana ni wazi kwamba hakuja kuwa saidia malaika bali kuwasaidia uzao wa Ibrahimu. 17 Kwa sababu hii ilibidi awe kama ndugu zake kwa kila hali, apate kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu katika huduma ya Mungu, ili aweze kujitoa kama sadaka kwa ajili ya dhambi za watu. 18 Na kwa kuwa yeye mwenyewe ameteswa na kujaribiwa, anaweza kuwasaidia wanaoj aribiwa.

Therefore we ought to give the more earnest heed to the things which we have heard, lest at any time we should let them slip.

For if the word spoken by angels was stedfast, and every transgression and disobedience received a just recompence of reward;

How shall we escape, if we neglect so great salvation; which at the first began to be spoken by the Lord, and was confirmed unto us by them that heard him;

God also bearing them witness, both with signs and wonders, and with divers miracles, and gifts of the Holy Ghost, according to his own will?

For unto the angels hath he not put in subjection the world to come, whereof we speak.

But one in a certain place testified, saying, What is man, that thou art mindful of him? or the son of man that thou visitest him?

Thou madest him a little lower than the angels; thou crownedst him with glory and honour, and didst set him over the works of thy hands:

Thou hast put all things in subjection under his feet. For in that he put all in subjection under him, he left nothing that is not put under him. But now we see not yet all things put under him.

But we see Jesus, who was made a little lower than the angels for the suffering of death, crowned with glory and honour; that he by the grace of God should taste death for every man.

10 For it became him, for whom are all things, and by whom are all things, in bringing many sons unto glory, to make the captain of their salvation perfect through sufferings.

11 For both he that sanctifieth and they who are sanctified are all of one: for which cause he is not ashamed to call them brethren,

12 Saying, I will declare thy name unto my brethren, in the midst of the church will I sing praise unto thee.

13 And again, I will put my trust in him. And again, Behold I and the children which God hath given me.

14 Forasmuch then as the children are partakers of flesh and blood, he also himself likewise took part of the same; that through death he might destroy him that had the power of death, that is, the devil;

15 And deliver them who through fear of death were all their lifetime subject to bondage.

16 For verily he took not on him the nature of angels; but he took on him the seed of Abraham.

17 Wherefore in all things it behoved him to be made like unto his brethren, that he might be a merciful and faithful high priest in things pertaining to God, to make reconciliation for the sins of the people.

18 For in that he himself hath suffered being tempted, he is able to succour them that are tempted.