Ujumbe Kwa Kanisa La Sardi

“Kwa malaika wa Kanisa la Sardi andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako; na kwamba una sifa ya kuwa hai, na kumbe umekufa. Amka! Imarisha kilichobakia kabla hakijaharibika kabisa, kwa maana nimeona kwamba kazi zako hazijakamilika mbele za Mungu wangu. Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na kutubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwizi wala huta jua saa nitakayokujia.

Bado wako watu wachache huko Sardi ambao hawajachafua mavazi yao. Wao watatembea pamoja nami wakiwa wamevaa mavazi yao meupe kwa maana wanastahili. Atakayeshinda atavikwa vazi jeupe kama wao, nami sitafuta jina lake katika kitabu cha uzima bali nitalikiri jina lake mbele ya Baba yangu na mbele za malaika wake.

Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anayaam bia makanisa.”’

Ujumbe Kwa Kanisa La Filadelfia

“Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, ambaye anao ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, na anachoki funga hakuna awezaye kukifungua.

Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango ulio wazi ambao hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba ingawa nguvu yako ni ndogo lakini umelishika neno langu na hujalikana jina langu. Sikiliza, wale watu ambao ni wa sinagogi la she tani, wale wajiitao Wayahudi kumbe sio, bali ni waongo; nitawafa nya waje wapige magoti mbele yako na wakiri kwamba nimekupenda. 10 Kwa kuwa umeshika agizo langu la kustahimili kwa subira, nitakulinda wakati wa ile dhiki itakayokuja duniani pote kuwajar ibu waishio ulimwenguni.

11 Ninakuja upesi. Shika sana kile ulicho nacho asije mtu akachukua taji yako. 12 Atakayeshinda nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo kamwe. Na nitaan dika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wake Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unakuja kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Pia nitaandika juu yake jina langu jipya.

13 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anay aambia makanisa.’ ”

Ujumbe Kwa Kanisa La Laodikia

14 “Kwa malaika wa kanisa la Laodikia andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aitwaye Amina, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa vyote alivyoumba Mungu.

15 Nayajua matendo yako; kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali kama ungalikuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa kuwa wewe ni vuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu. 17 Unajigamba ukisema, ‘Mimi ni tajiri , nimefanikiwa wala sihitaji kitu cho chote.’ Lakini hutambui kwamba wewe ni mnyonge, mtu wa kuhurumiwa, maskini, kipofu; tena wewe ni uchi. 18 Kwa hiyo ninakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosaf ishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri; na mavazi meupe ili upate kuvaa, ufiche aibu ya uchi wako. Ujinunulie pia mafuta uyapake macho yako ili upate kuona.

19 Wote niwapendao, ninawakaripia na kuwarudi. Kwa hiyo fanya bidii, utubu na kuziacha dhambi zako. 20 Tazama, nasimama mlangoni napiga hodi. Mtu ye yote akisikia sauti yangu na kufun gua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami. 21 Atakayeshinda nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi. 22 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anay aambia makanisa.’ ”

Barua ya Yesu kwa Kanisa la Sardi

Andika hivi kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi:

Huu ni ujumbe kutoka kwake Yeye mwenye roho saba na nyota saba.

Ninayajua matendo yako. Watu husema kuwa u hai, lakini hakika umekufa. Amka! Jitie nguvu kabla ya nguvu kidogo uliyonayo haijakuishia kabisa. Unachofanya hakistahili kwa Mungu wangu. Hivyo usisahau kile ulichopokea na kusikia. Ukitii. Geuza moyo na maisha yako! Amka, la sivyo nitakuja kwako na kukushtukiza kama mwizi. Hautajua wakati nitakapokuja.

Lakini una watu wachache katika kundi lako hapo Sardi waliojiweka safi. Watatembea pamoja nami. Watavaa nguo nyeupe, kwa kuwa wanastahili. Kila atakayeshinda atavikwa nguo nyeupe kama wao. Sitayafuta majina yao katika kitabu cha uzima. Nitawakiri mbele za Baba yangu na malaika zake ya kuwa wao ni wangu. Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa.

Barua ya Yesu kwa kanisa la Filadelfia

Andika hivi kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia:

Huu ni ujumbe kutoka kwake aliye mtakatifu na wa kweli, anayeshikilia ufunguo wa Daudi. Anapofungua kitu, hakiwezi kufungwa. Na anapofunga kitu hakiwezi kufunguliwa.

Ninayajua matendo yako. Nimeweka mbele yako mlango ulio wazi ambao hakuna anayeweza kuufunga. Ninajua wewe ni dhaifu, lakini umeyafuata mafundisho yangu. Hukuogopa kulisema jina langu. Sikiliza! Kuna kundi[a] la Shetani. Wanasema kuwa wao ni Wayahudi, lakini ni waongo. Si Wayahudi halisi. Nitawafanya waje mbele yako na kusujudu kwenye miguu yako. Watajua ya kuwa ninakupenda. 10 Umeifuata amri yangu kwa uvumilivu. Hivyo nitakulinda wakati wa shida itakayokuja ulimwenguni, wakati ambapo kila aishiye duniani atajaribiwa.

11 Naja upesi. Ishikilie imani uliyonayo, ili mtu yeyote asiichukue taji yako. 12 Wale watakaoshinda watakuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu. Hawataliacha hekalu la Mungu tena. Nitaandika juu yao jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu. Mji huo ni Yerusalemu mpya.[b] Unateremka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Pia nitaandika jina langu jipya juu yao. 13 Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa.

Barua ya Yesu kwa Kanisa la Laodikia

14 Andika hivi kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia:

Huu ni ujumbe kutoka kwa yeye aliye Amina,[c] shahidi mwaminifu na wa kweli, aliye chanzo cha uumbaji wa Mungu.

15 Ninayajua matendo yako. Wewe si moto wala baridi. Ninatamani kama ungekuwa moto au baridi! 16 Lakini wewe ni vuguvugu tu, si moto, wala baridi. Hivyo niko tayari kukutema utoke mdomoni mwangu. 17 Unasema wewe ni tajiri. Unadhani ya kuwa umekuwa tajiri na huhitaji kitu chochote. Lakini hujui kuwa wewe ni mnyonge, mwenye masikitiko, maskini, asiyeona na uko uchi. 18 Ninakushauri ununue dhahabu kutoka kwangu, dhahabu iliyosafishwa katika moto. Kisha utakuwa tajiri. Nakuambia hili: Nunua kwangu mavazi meupe. Ndipo utaweza kuifunika aibu ya uchi wako. Ninakuagiza pia ununue kwangu dawa ya kuweka kwenye macho yako, nawe utaweza kuona.

19 Mimi huwasahihisha na kuwaadhibu wale niwapendao. Hivyo onesha kuwa kuishi kwa haki ni muhimu kwako kuliko kitu kingine. Geuzeni mioyo na maisha yenu. 20 Niko hapa! Nimesimama mlangoni nabisha hodi. Ikiwa utaisikia sauti yangu na ukaufungua mlango, nitaingia kwako na kula pamoja nawe. Nawe utakula pamoja nami.

21 Nitamruhusu kila atakayeshinda kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi. Ilikuwa vivyo hivyo hata kwangu. Nilishinda na kuketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi. 22 Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa.”

Footnotes

  1. 3:9 kundi Yaani, “sinagogi”.
  2. 3:12 Yerusalemu mpya Mji wa kiroho ambako Mungu ataishi pamoja na watu wake.
  3. 3:14 Amina Neno hili limetumika hapa kama jina la Yesu, maana yake neno hili ni kukubali kwa dhati kuwa kitu fulani ni sahihi au kweli.