Add parallel Print Page Options

Yesu Afundisha Kuhusu Kisasi

(Lk 6:29-30)

38 Mmesikia ilisemwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’(A) 39 Lakini ninawaambia msishindane na yeyote anayetaka kuwadhuru. Mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na la kushoto pia. 40 Mtu akitaka kukushitaki ili akunyang'anye shati, mpe na koti pia. 41 Askari akikulazimisha kwenda naye maili moja,[a] nenda maili mbili pamoja naye. 42 Mpe kila anayekuomba, usimkatalie anayetaka kuazima kitu kwako.

Wapende Adui Zako

(Lk 6:27-28,32-36)

43 Mmesikia ilisemwa kuwa, ‘Wapende rafiki zako(B) na wachukie adui zako.’ 44 Lakini ninawaambia wapendeni adui zenu na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. 45 Mkifanya hivi mtakuwa watoto halisi walio kama Baba yenu wa mbinguni. Yeye huwaangazia jua watu wote, bila kujali ikiwa ni wema au wabaya. Huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 Ikiwa mnawapenda wale wanaowapenda ninyi, kwa nini mpate thawabu toka kwa Mungu? Hata watoza ushuru hufanya hivyo. 47 Na ikiwa mnakuwa wema kwa rafiki zenu tu, ninyi si bora kuliko wengine. Hata watu wasiomjua Mungu ni wakarimu kwa rafiki zao pia. 48 Ninalosema ni kuwa, mkue hata kufikia upendo kamili[b] alionao baba yenu wa Mbinguni kwa watu wote.

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:41 maili moja Kama kilomita moja na nusu.
  2. 5:48 kamili Neno “kamilifu”, hapa lina maana “imeendelezwa kwa ukamilifu”, na inaelezea aina ya upendo ambao watoto wanaweza kujifunza kutoka kwa baba.