Add parallel Print Page Options

Yohana Ambatiza Yesu

(Mk 1:9-11; Lk 3:21-22)

13 Ndipo Yesu alitoka Galilaya na kwenda Mto Yordani. Alikwenda kwa Yohana, akitaka kubatizwa. 14 Lakini Yohana alijaribu kumzuia. Yohana akamwambia Yesu, “Kwa nini unakuja kwangu ili nikubatize? Mimi ndiye ninayepaswa kubatizwa na wewe!”

15 Yesu akajibu, “Acha iwe hivyo kwa sasa. Tunapaswa kuyatimiza mapenzi ya Mungu.” Ndipo Yohana akakubali.

16 Hivyo Yesu akabatizwa. Mara tu aliposimama kutoka ndani ya maji, mbingu zilifunguka na akamwona Roho Mtakatifu akishuka kutoka mbinguni kama hua[a] na kutua juu yake. 17 Sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu, nimpendaye. Ninapendezwa naye.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:16 hua Ndege mfano wa njiwa, aendaye kwa kasi au “njiwa pori”, “tetere”.