Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni

18 Wakati huo, wanafunzi walimjia Yesu wakamwuliza, “Ni nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa mbinguni?” Yesu akam wita mtoto mdogo akamsimamisha mbele yao. Kisha akasema, “Nawa hakikishieni kwamba msipobadilika na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni. Kwa hiyo mtu ye yote anayejinyenyekeza akawa kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa mbinguni.

“Na ye yote anayemkaribisha mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, ananikaribisha mimi.

Read full chapter