Na Sauli aliunga mkono kuuawa kwa Stefano Tangu siku hiyo waamini katika kanisa la Yerusalemu walianza kuteswa sana. Waamini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia katika majimbo ya Yudea na Samaria. Watu waliomcha Mungu walimzika Stefano na kumwombolezea sana. Lakini Sauli alitaka kulianga miza kanisa kabisa. Akawa akienda kila nyumba akawaburura waamini, wanaume kwa wanawake, akawatia jela.

Injili Yahubiriwa Samaria

Wale waamini waliotawanyika walihubiri neno la Mungu kila mahali walipokuwa. Filipo naye alikwenda katika mji mmoja wa Samaria akahubiri habari za Kristo. Watu wengi walipomsikiliza Filipo na kuona ishara za ajabu alizofanya, walizingatia kwa makini ujumbe wake. Pepo wachafu walikuwa wakiwatoka watu wengi, huku wakipiga makelele; na wengi waliopooza na viwete, waliponywa. Pakawa na furaha kuu katika mji huo.

Lakini katika mji huo alikuwepo mtu mmoja aitwaye Simoni, ambaye alikuwa mchawi. Kwa muda mrefu alikuwa amewapumbaza na kuwashangaza watu kwa mazingaombwe, akawa anajigamba kuwa yeye ni mtu maarufu. 10 Watu wa tabaka zote, wakubwa kwa wadogo, walivu tiwa sana naye, wakawa wanasema, “Bila shaka mtu huyu ndiye ile nguvu ya Mungu iitwayo ‘Uwezo Mkuu.’ ” 11 Wakamsikiliza kwa makini kwa sababu aliwastaajabisha kwa mazingaombwe yake. 12 Lakini watu walipoamini mahubiri ya Filipo kuhusu Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, waume kwa wake. 13 Hata Simoni naye aliamini na alipokwisha batizwa aliambatana na Filipo. Alipoona ishara na miujiza aliy ofanya Filipo alistaajabu sana .

14 Basi mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia kuwa watu wa Samaria wameamini neno la Bwana, waliwatuma Petro na Yohana waende huko. 15 Nao walipofika waliwaombea ili wapokee Roho Mta katifu; 16 kwa maana walikuwa wamebatizwa tu katika jina la Bwana Yesu na Roho Mtakatifu alikuwa bado hajawashukia. 17 Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao waka pokea Roho Mtakatifu. 18 Simoni alipoona kuwa watu walipokea Roho Mtakatifu mitume walipoweka mikono juu yao, aliwapa fedha 19 akasema, “Nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakayeweka mikono yangu juu yake apokee Roho Mtakatifu.” 20 Petro akam jibu, “Uangamie wewe na fedha zako, kwa maana unadhani unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!” 21 Wewe huwezi kuwa na sehemu wala fungu katika jambo hili kwa kuwa moyo wako hauko sawa mbele za Mungu. 22 Kwa hiyo tubu, uache huu uovu wako; na umwombe Mungu ili kama inawezekana akusamehe makusudio maovu uliyo nayo moyoni. 23 Kwa maana ninaona wazi kwamba wewe umejawa na wivu na ni mfungwa wa dhambi. 24 Simoni akajibu, “Niombeeni kwa Bwana, ili hayo mliyosema yasije yakanipata.” 25 Nao wali pokwisha kutoa ushuhuda na kufundisha neno la Bwana, walirudi Yerusalemu; na walipokuwa wakisafiri walihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.

Filipo Ambatiza Afisa Wa Ethiopia

26 Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara itokayo Yerusalemu kuelekea Gaza.” Hii ilikuwa barabara iendayo jangwani. 27 Filipo akaondoka akaenda. Wakati huo Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa waziri wa fedha wa Kandake, Malkia wa Ethiopia, alikuwa anarudi nyumbani baada ya kumwabudu Mungu huko Yerusalemu. 28 Alikuwa amekaa kwenye gari la kuvutwa na farasi akielekea makwao, akisoma kitabu cha nabii Isaya. 29 Roho wa Mungu akamwambia Filipo, “Nenda kasimame karibu na lile gari.” 30 Kwa hiyo Filipo aka harakisha kulikaribia, na alipofika karibu akamsikia yule afisa akisoma katika kitabu cha nabii Isaya, akamwuliza, “Je, unaelewa unachosoma?” 31 Yule afisa akamjibu, “Nitaelewaje mtu asipo nielekeza? Akamkaribisha Filipo katika gari, akaketi pamoja naye. 32 Maneno aliyokuwa akisoma ni haya, ‘Alipelekwa kama kon doo anayetolewa kuchinjwa na kama mwana-kondoo anavyotulia anapo katwa manyoya, naye hakusema neno lo lote. 33 Aliaibishwa, aka nyimwa haki yake. Ni nani awezaye kuelezea juu ya kizazi chake? Kwa maana uhai wake umeondolewa duniani.’ 34 Yule towashi akam wuliza Filipo, “Tafadhali niambie, Isaya alikuwa akisema haya juu yake mwenyewe au juu ya mtu mwingine?” 35 Ndipo Filipo akaanza kusema naye, akitumia Maandiko haya akamweleza Habari Njema za Yesu. 36 Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, na yule towashi akamwambia Filipo, “ Tazama, hapa kuna maji! Kuna kitu gani cha kunizuia mimi nisiba tizwe? [ 37 Filipo akamwambia, “Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”] 38 Akaamuru gari lisimamishwe. Wakateremka, yule towashi na Filipo, wakaenda pale kwenye maji. Filipo akamba tiza. 39 Walipotoka katika yale maji, Roho wa Bwana akamchukua Filipo na yule towashi hakumwona tena. Kwa hiyo akaendelea na safari yake akiwa amejawa na furaha. 40 Filipo akajikuta yuko Azoto; akasafiri akihubiri Injili katika miji yote mpaka alipo fika Kaisaria.

1-3 Sauli aliridhia kuwa kuuawa kwa Stefano lilikuwa jambo jema. Baadhi ya wacha Mungu walimzika Stefano, wakaomboleza na kumlilia kwa sauti kuu.

Matatizo Kwa waamini

Kuanzia siku hiyo Wayahudi walianza kulitesa sana kanisa na waamini katika mji wa Yerusalemu. Sauli pia alijaribu kuliharibu kanisa. Aliingia katika nyumba za waamini, akawaburuta wanaume na wanawake, na kuwafunga gerezani. Waamini wote walikimbia kutoka Yerusalemu, mitume peke yao ndiyo walibaki. Waamini walikwenda mahali tofauti tofauti katika Uyahudi na Samaria. Walitawanyika kila mahali, na kila walikokwenda waliwahubiri watu Habari Njema.

Filipo Ahubiri Katika Samaria

Filipo[a] alikwenda katika mji mkuu wa jimbo la Samaria na kuwahubiri watu kuhusu Masihi. Watu wa Samaria walimsikiliza Filipo na kuona miujiza aliyotenda. Wote walisikiliza kwa makini yale aliyosema. Watu wengi miongoni mwao walikuwa na mapepo, lakini Filipo aliyakemea mapepo na yaliwatoka watu. Mapepo yalipiga kelele nyingi yalipokuwa yanawatoka watu. Walikuwepo pia watu wengi waliopooza na walemavu wa miguu pale. Filipo aliwaombea na wote walipona. Kulikuwa furaha kubwa katika mji ule wa Samaria siku ile!

Mtu mmoja aliyeitwa Simoni alikuwa anaishi katika mji huo. Kabla Filipo hajaenda huko, Simoni alikuwa akifanya uchawi na kuwashangaza watu wote wa Samaria. Alijigamba na kujiita mtu mkuu. 10 Watu wote, kuanzia mdogo hadi mkubwa, waliamini yale aliyosema Simoni. Walisema, “Mtu huyu ndiye anayeitwa ‘Nguvu Kuu ya Mungu.’” 11 Simoni aliwashangaza watu kwa muda mrefu kwa uchawi wake na watu wote wakawa wafuasi wake. 12 Lakini Filipo alipowahubiri watu Habari Njema kuhusu Ufalme wa Mungu na Nguvu za Yesu Kristo. Wanaume na wanawake waliamini alichosema Filipo na wakabatizwa. 13 Simoni mwenyewe aliamini, na baada ya kubatizwa, alikaa karibu na Filipo. Alipoona miujiza na matendo makuu ya ajabu yaliyofanyika kupitia Filipo, alishangaa.

14 Mitume mjini Yerusalemu, waliposikia kuwa watu wa Samaria wameupokea Ujumbe wa Mungu, waliwatuma Petro na Yohana kwenda kwa watu wa Samaria. 15 Petro na Yohana walipofika, waliomba ili Roho Mtakatifu awashukie waamini wa Samaria. 16 Watu hawa walikuwa wamebatizwa katika jina la Bwana Yesu, lakini Roho Mtakatifu alikuwa bado hajamshukia hata mmoja wao. Na hii ndiyo sababu Petro na Yohana waliomba. 17 Mitume hawa wawili walipoweka mikono yao juu ya watu, Roho Mtakatifu aliwashukia.

18 Simoni aliyekuwa mchawi alipoona Roho Mtakatifu anatolewa kwa watu kwa kuweka mikono juu yao. Aliwapa pesa mitume. 19 Akasema, “Nipeni na mimi nguvu hii ili nitakapoweka mikono yangu juu ya mtu yeyote, atampata Roho Mtakatifu.”

20 Petro akamwambia Simoni, “Wewe pamoja na pesa zako mwangamie kwa sababu unadhani unaweza kununua karama kutoka kwa Mungu kwa pesa. 21 Huwezi kushirikiana nasi katika kazi hii. Moyo wako si safi mbele za Mungu. 22 Badili moyo wako! Achana na mawazo haya maovu na umwombe Bwana. Yumkini atakusamehe! 23 Kwa kuwa ninaona umejaa wivu mwingi nawe ni mfungwa wa uovu.”

24 Simoni akajibu, “Niombeeni kwa Bwana, ili haya uliyosema yasinipate.”

25 Ndipo wale mitume wawili waliwaambia watu waliyoona Yesu akitenda. Wakawaambia ujumbe wa Bwana. Kisha wakarudi Yerusalemu. Wakiwa njiani kurudi, walipitia katika miji mingi ya Wasamaria na kuwahubiri watu Habari Njema.

Filipo Amfundisha Mtu Kutoka Ethiopia

26 Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jiandae na uende kusini katika barabara ya jangwani inayoteremka kutoka Yerusalemu kwenda Gaza.”

27 Filipo alijiandaa na kwenda. Akiwa njiani alimwona mwanaume kutoka Ethiopia. Alikuwa towashi na ofisa muhimu wa Kandake, malkia wa Ethiopia. Alikuwa na mweka hazina mkuu wa malkia. Mtu huyu alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu. 28 Na alikuwa anarudi Ethiopia. Alikuwa ameketi katika gari lake la kukokotwa na farasi akiwa anasoma kitabu cha nabii Isaya.

29 Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda kwenye gari hilo na uwe karibu yake.” 30 Hivyo Filipo akaenda karibu na gari, akamsikia mtu yule akisoma kutoka katika kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamwuliza, “Unaelewa unachosoma?”

31 Yule mtu akajibu, “Nitaelewaje? Ninahitaji mtu wa kunifafanulia.” Ndipo akamwomba Filipo apande garini na aketi pamoja naye. 32 Sehemu ya Maandiko aliyokuwa anasoma ilikuwa hii:

“Alikuwa kama kondoo
    anayepelekwa kwa mchinjaji.
Alikuwa kama mwana kondoo asivyopiga kelele
    anapokatwa manyoya yake.
    Hakusema kitu.
33 Alidhalilishwa,
    na kunyimwa haki zake zote.
Maisha yake duniani yamekoma.
    Hivyo hakutakuwa simulizi yoyote kuhusu wazaliwa wake.”(A)

34 Afisa[b] akamwambia Filipo, “Tafadhali niambie, nabii anazungumza kuhusu nani? Anazungumza kuhusu yeye mwenyewe au mtu mwingine?” 35 Filipo akaanza kuzungumza. Alianzia na Andiko hili na kumwambia mtu yule Habari Njema kuhusu Yesu.

36 Walipokuwa wanasafiri waliyakuta maji mahali fulani. Afisa akasema, “Tazama! Hapa kuna maji! Nini kinanizuia nisibatizwe?” 37 [c] 38 Ndipo Afisa akaamuru gari lake lisimame. Wote wawili, Filipo na Afisa, wakatelemka wakaingia kwenye maji na Filipo akambatiza towashi. 39 Walipotoka kwenye maji, Roho wa Bwana akamchukua Filipo; afisa hakumwona Filipo tena. Afisa aliendelea na safari yake kurudi nyumbani, akiwa mwenye furaha sana. 40 Lakini Filipo alionekana katika mji ulioitwa Azoto. Alikuwa akienda kwenye mji wa Kaisaria. Aliwahubiri watu Habari Njema katika miji yote wakati anasafiri kutoka Azoto kwenda Kaisaria.

Footnotes

  1. 8:5 Filipo Siyo mtume aliyeitwa Filipo.
  2. 8:34 Afisa Kwa maana ya kawaida, “towashi”. Pia katika mstari wa 36,38,39.
  3. 8:37 Nakala zingine za baadaye za Matendo zimeongeza mstari wa 37: Filipo akajibu, “Ikiwa unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa. Ofisa akasema, ‘Ninaamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.’”