Ndipo kuhani mkuu alimwuliza Stefano, “Je, mashtaka haya ni ya kweli?” Stefano akajibu, “Ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni! Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, ali pokuwa Mesopotamia, kabla hajahamia Harani, akamwambia, ‘Ondoka kutoka katika nchi yako na kutoka kwa jamii yako uende katika nchi nitakayokuonyesha.’ Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakal dayo akaenda kukaa Harani. Baba yake alipokufa, Mungu akamtoa huko akamweka katika nchi hii ambayo mnaishi sasa. Lakini Mungu hakumpa urithi wo wote katika nchi hii, hakumpa hata mita moja ya ardhi. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Ibrahimu hakuwa na mtoto. Mungu alimwambia maneno haya, ‘Wazao wako wataishi ugenini, ambapo watafanywa kuwa watumwa na kutendewa maovu kwa kipindi cha miaka mia nne. Lakini nitalihukumu taifa ambalo watalitumikia, na baada ya haya watatoka katika nchi hiyo ili waje kuniabudu mahali hapa.’

“Mungu akampa Ibrahimu agano la tohara. Basi Ibrahimu akawa baba wa Isaka; naye akamtahiri Isaka siku ya nane baada ya kuzaliwa kwake. Isaka akawa baba wa Yakobo, naye Yakobo akawa baba wa babu zetu kumi na wawili. Hawa babu zetu walimwonea Yusufu ndugu yao wivu, wakamwuza utumwani Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye. 10 Akamwokoa katika mateso yote yaliyom pata, na akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, Mfalme wa Misri, ambaye alimfanya waziri mkuu wa nchi nzima na mtawala wa nyumba ya mfalme.

11 “Kukawa na njaa na dhiki kubwa nchi yote ya Misri na Kanaani, na babu zetu wakawa hawana chakula. 12 Lakini Yakobo aliposikia kwamba kule Misri kulikuwa na nafaka, aliwatuma wanawe, wakaenda huko kwa mara yao ya kwanza. 13 Nao walipotumwa mara ya pili, Yusufu alijitambulisha kwa ndugu zake, na akawatam bulisha ndugu zake kwa Farao. 14 Yusufu akatuma Yakobo baba yake aletwe Misri pamoja na ukoo mzima, wakiwa ni watu sabini na watano; na 15 Yakobo akaenda Misri. Naye akafa huko, yeye na wanawe, yaani babu zetu, 16 na miili yao ikachukuliwa na kuzikwa huko Shekemu katika kaburi ambalo Ibrahimu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori. 17 Ulipokaribia wakati Mungu aliopanga kutimiza ahadi yake, kwa Ibrahimu, idadi ya watu iliongezeka sana huko Misri. 18 Ndipo akatokea mfalme mpya wa Misri ambaye hakumfahamu wala kumtambua Yusufu. 19 Huyu mfalme aliwafanyia hila watu wa taifa letu na akawalazimisha babu zetu wawatupe watoto wao wachanga ili wafe.

20 “Musa alizaliwa wakati huo, naye alikuwa mtoto mzuri sana machoni pa Mungu. Akalelewa na wazazi wake kwa muda wa miezi mitatu. 21 Waliposhindwa kumficha zaidi, wakamweka nje na binti Farao akamchukua akamtunza kama mtoto wake mwenyewe. 22 Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri akawa mtu shujaa kwa maneno na matendo yake. 23 Musa alipokuwa na umri wa miaka arobaini akawa na hamu ya kuwatembelea ndugu zake Waisraeli. 24 Alipoona mmoja wao akionewa na Mmisri, akamwua yule Mmisri kulipiza kisasi. 25 Alidhani kuwa ndugu zake wangeelewa kwamba Mungu ali kuwa akiwaokoa kwa msaada wake, lakini wao hawakuelewa. 26 Kwa hiyo siku ya pili alipoona Waisraeli wanagombana alijaribu kuwa patanisha, akawaambia, ‘Jamani, ninyi ni ndugu. Mbona mnaoneana wenyewe kwa wenyewe?’ 27 Lakini yule aliyekuwa akimwonea mwen zake akamsukumia Musa kando, akamwuliza, ‘Ni nani aliyekuweka uwe mtawala na mwamuzi kati yetu? 28 Je, unataka kuniua kama ulivy omwua yule Mmisri jana?’ 29 Musa aliposikia maneno haya alikim bia akatoka Misri akaenda kuishi kama mkimbizi sehemu za Midiani. Huko akawa baba wa watoto wawili wa kiume. 30 “Baada ya miaka arobaini, malaika wa Mungu akamtokea jangwani karibu na Mlima Sinai katika kichaka kilichokuwa kina waka moto. 31 Musa alishangazwa na kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto; na aliposogea karibu ili aone vizuri, akasikia sauti ya Bwana ikisema, 32 ‘Mimi ni Mungu wa baba zako; Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka na wa Yakobo.’ Musa alitetemeka kwa hofu akaogopa kutazama.

33 “Mungu akamwambia, ‘Vua viatu vyako kwa maana hapo uli posimama ni mahali patakatifu. 34 Nimeona mateso ya watu wangu walioko Misri, na nimesikia kilio chao, nami nimeshuka ili niwaokoe. Basi sasa nitakutuma Misri.’ 35 Huyu Musa ndiye wali yemkataa wakisema, ‘Ni nani aliyekufanya uwe mtawala na mwamuzi wetu?’ Mungu alimtuma kama mtawala na mkombozi kwa njia ya yule malaika aliyemtokea katika kile kichaka. 36 Aliwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, baada ya kufanya maajabu na ishara nyingi huko Misri na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini.

37 “Huyu Musa ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, ‘Mungu atawateulia nabii kutoka miongoni mwa ndugu zenu kama alivyoni teua mimi.’ 38 Huyu Musa alikuwa katika kusanyiko la wana wa Israeli jangwani pamoja na baba zetu na yule malaika aliyezun gumza naye kwenye Mlima wa Sinai; akapokea maneno yaliyo hai ili atupatie.

39 “Lakini baba zetu walikataa kumtii Musa, wakamsusia, na mioyoni mwao wakarudi Misri. 40 Wakamwambia Haruni, ‘Tufanyie miungu watakaotuongoza; kwa maana huyu Musa aliyetutoa Misri hat ujui yaliyompata.’ 41 Siku hizo wakatengeneza kinyago mfano wa ndama, wakakitolea sadaka za kuteketezwa, kisha wakafanya sherehe kushangilia kitu walichotengeneza kwa mikono yao wenyewe. 42 Ndipo Mungu akaondoka kati yao, akawaacha waabudu sayari za angani kama miungu yao: jua, mwezi na nyota. Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii, ‘ Je, nyumba ya Israeli, mlinitolea sadaka za wanyama wa kuteketezwa kwa miaka arobaini jangwani? La! 43 Tazama mlibeba hema ya Moleki, na sanamu ya nyota wa Refani, miungu mliyotengeneza ili muiabudu. Kwa hiyo nitawapeleka utum wani, mbali kuliko Babiloni.’

44 “Baba zetu walikuwa na ile hema ya ushuhuda pamoja nao jangwani. Nayo ilikuwa imetengenezwa kama malaika alivyomwelekeza Musa itengenezwe; na kwa mshono ambao Musa alikuwa ameonyeshwa. 45 Nao baba zetu wakaileta hiyo hema wakiongozwa na Yoshua wali poiteka nchi kutoka kwa yale mataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbele yao. Na hivi ndivyo ilivyokuwa mpaka wakati wa mfalme Daudi 46 ambaye alipendwa na Mungu, naye akaomba apewe ruhusa amjengee Mungu wa Yakobo makao. 47 Lakini mfalme Sulemani ndiye aliyem jengea Mungu nyumba. 48 Hata hivyo Mungu aliye Mkuu sana hakai kwenye nyumba iliyojengwa kwa mikono na binadamu. Kama nabii alivyosema, 49 ‘Mbingu ni kiti changu cha Enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu: mtanijengea nyumba ya namna gani? Auliza Bwana. Au mahali pangu pa kupumzikia ni wapi? 50 Je, si mimi niliyeumba vitu vyote hivi?’

51 “Ninyi watu wenye shingo ngumu! Wenye mioyo ya kipagani! Mmekuwa viziwi kwa neno la Mungu wala hamchoki kumpinga Roho Mta katifu! Kama walivyofanya baba zetu nanyi leo mnafanya vivyo hivyo. 52 Je, kuna nabii hata mmoja ambaye baba zetu hawa kumtesa? Waliwaua hata wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki, ambaye ninyi mmemsaliti kisha mkamwua. 53 Ninyi mlizipokea sheria za Mungu zilizoletwa kwenu na malaika lakini hamkuzitii.”

Stefano Auawa Kwa Kupigwa Mawe

54 Basi wale viongozi waliposikia maneno haya walijawa na hasira, wakasaga meno yao kwa ghadhabu. 55 Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, alitazama mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, akamwona Yesu amesimama upande wa kulia wa Mungu.” 56 Akasema, “Tazameni! Naona mbingu zimefunguka na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kulia wa Mungu.”

Adamu amesimama upande wa kulia wa Mungu.”

57 Wao wakapiga makelele, wakaziba masikio yao wasimsikie, wakamrukia kwa pamoja. 58 Wakamtupa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Na mashahidi walioteuliwa walimwachia kijana mmoja aitwae Sauli mavazi yao. 59 Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, Bwana Yesu, pokea roho yangu!” 60 Akapiga magoti akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema haya, akafa.

Hotuba ya Stefano

Kuhani mkuu akamwambia Stefano, “Mambo haya ndivyo yalivyo?” Stefano akajibu, “Ndugu zangu na baba zangu Wayahudi, nisikilizeni! Mungu wetu mkuu na mwenye utukufu alimtokea Ibrahimu, baba yetu, alipokuwa Mesopotamia. Kabla hajahamia Harani. Mungu alimwambia, ‘Ondoka katika nchi yako na watu wako, kisha uende katika nchi nitakayokuonesha.’(A)

Hivyo Ibrahimu akaondoka katika nchi ya Ukaldayo[a] na kwenda kuishi Harani. Baada ya baba yake kufa, Mungu akamleta katika nchi hii, mahali mnapoishi sasa. Lakini Mungu hakumpa Ibrahimu sehemu yoyote ya ardhi hii, hata eneo dogo lenye ukubwa wa unyayo wake. Lakini Mungu aliahidi kuwa atampa Ibrahimu nchi hii yeye na watoto wake hapo baadaye. Hii ilikuwa kabla Ibrahimu hajapata watoto.

Mungu alimwambia: ‘Wazao wako wataishi katika nchi nyingine. Watakuwa wageni. Watu wa huku watawafanya kuwa watumwa na kuwatendea vibaya kwa miaka mia nne. Lakini nitaliadhibu taifa lililowafanya watumwa.’(B) Pia, Mungu alisema, ‘Baada ya mambo hayo kutokea, watu wako watatoka katika nchi hiyo. Kisha wataniabudu mahali hapa.’(C)

Mungu aliweka agano na Ibrahimu; alama ya agano hili ilikuwa tohara. Na Ibrahimu alipopata mwana, alimtahiri siku ya nane baada ya kuzaliwa. Jina la mwanaye lilikuwa Isaka. Pia, Isaka alimtahiri mwanaye Yakobo. Na Yakobo alifanya vivyo hivyo kwa wanaye, ambao ndiyo baba wakuu kumi na mbili wa watu wetu.

Baba zetu hawa walimwonea wivu Yusufu ndugu yao na wakamwuza ili awe mtumwa Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye, 10 akamwokoa kutoka katika matatizo yake yote. Wakati huo Farao alikuwa mfalme wa Misri. Alimpenda na akamheshimu Yusufu kwa sababu ya hekima ambayo Mungu alimpa. Farao alimfanya Yusufu kuwa gavana wa Misri na msimamizi wa watu wote na kila kitu katika kasri lake. 11 Lakini nchi yote ya Misri na Kanaani zikakosa mvua na mazao ya chakula hayakuweza kuota. Watu waliteseka sana na watu wetu hawakuweza kupata chakula chochote.

12 Lakini Yakobo aliposikia kulikuwa chakula Misri aliwatuma mababa zetu huko. Hii ilikuwa safari yao ya kwanza kwenda Misri. 13 Kisha walikwenda safari ya pili. Safari hii Yusufu akawaeleza ndugu zake yeye ni nani. Ndipo Farao akatambua kuhusu familia ya Yusufu. 14 Kisha Yusufu aliwatuma kaka zake wamwambie Yakobo, baba yake, ahamie Misri. Aliwaalika pia ndugu zake wote, jumla yao wote walikuwa watu sabini na tano. 15 Hivyo Yakobo alitelemka kwenda Misri. Yeye na baba zetu waliishi huko mpaka walipokufa. 16 Baadaye, miili yao ilihamishiwa Shekemu, ambako iliwekwa katika kaburi ambalo Ibrahimu alilinunua kwa fedha kutoka kwa wana wa Hamori.

17 Watu wetu walipokuwa Misri idadi yao iliongezeka. Watu wetu walikuwa wengi mno huko. Ahadi ambayo Mungu aliiweka kwa Ibrahimu ilikuwa karibu kutimia. 18 Ndipo mfalme mwingine akaanza kutawala Misri, ambaye hakujua lolote kuhusu Yusufu. 19 Mfalme huyu aliwahadaa watu wetu. Akawatendea vibaya sana, akawalazimisha wawaache watoto wao nje ili wafe.

20 Huu ni wakati ambapo Musa alizaliwa. Alikuwa mtoto mzuri sana, na kwa miezi mitatu wazazi wake walimtunza nyumbani. 21 Walipolazimishwa kumtoa nje, Binti wa Farao alimchukua. Alimkuza kama mwanaye wa kumzaa. 22 Musa alielimishwa kwa elimu bora ya Kimisri. Wamisri walimfundisha kila kitu walichojua. Alikuwa mwenye nguvu katika yote aliyosema na kutenda.

23 Musa alipokuwa na umri wa miaka kama arobaini, aliamua kuwatembelea watu wake mwenyewe, watu wa Israeli. 24 Aliona mmoja wao ananyanyaswa na Mmisri, hivyo akamtetea; Musa akampiga na kumwua Mmisri ili kulipiza kwa kumwumiza Mwisraeli. 25 Musa alidhani kwamba watu wake wangeelewa kuwa Mungu alikuwa anamtumia kuwaokoa. Lakini hawakuelewa.

26 Siku iliyofuata, Musa akawaona wawili wa watu wake wakipigana. Alijaribu kuwapatanisha kwa kuwaambia, ‘Ninyi ni ndugu! Kwa nini mnataka kuumizana?’ 27 Aliyekuwa akimwumiza mwenzake akamsukuma Musa na akamwambia, ‘Nani amekufanya wewe uwe mtawala na mwamuzi wetu? 28 Unataka kuniua kama ulivyomwua yule Mmisri jana?’(D) 29 Musa alipomsikia akisema hili, alikimbia Misri. Alikwenda kuishi Midiani kama mgeni. Katika kipindi alichoishi huko, alipata wana wawili.

30 Miaka arobaini baadaye, Musa alipokuwa jangwani karibu na Mlima Sinai, malaika alimtokea katika mwali wa moto uliokuwa unawaka katika kichaka. 31 Musa alipoliona hili, alishangaa. Alisogea ili kuangalia kwa karibu. Akasikia sauti; ilikuwa sauti ya Bwana. 32 Bwana alisema, ‘Mimi ni Mungu yule yule aliyeabudiwa na baba zako. Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.’(E) Musa akaanza kutetemeka kwa woga. Aliogopa kukitazama kichaka.

33 Kisha Bwana akamwambia, ‘Vua viatu vyako, kwa sababu mahali uliposimama ni ardhi takatifu. 34 Nimewaona watu wangu wanavyoteseka sana Misri. Nimesikia watu wangu wakilia na nimeshuka ili kuwaokoa. Njoo sasa, Musa, ninakutuma urudi Misri.’(F)

35 Huyu ni Musa ndiye aliyekataliwa na watu wake. Walisema, ‘Nani amekufanya uwe mtawala na mwamuzi wetu?’(G) Lakini ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mtawala na mwokozi. Mungu alimtuma pamoja na msaada wa malaika,[b] ambaye Musa alimwona katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto. 36 Hivyo Musa aliwaongoza watu kutoka Misri. Alitenda maajabu na ishara za miujiza Misri, katika bahari ya Shamu na jangwani kwa miaka arobaini.

37 Huyu ni Musa yule yule aliyewaambia maneno haya watu wa Israeli: ‘Mungu atakupa nabii. Nabii huyo atakuja kutoka miongoni mwa watu wako mwenyewe. Atakuwa kama mimi.’(H) 38 Musa huyo huyo alikuwa pamoja na kusanyiko la watu wa Mungu jangwani. Alikuwa na malaika aliyezungumza naye alipokuwa Mlima Sinai, na alikuwa pamoja na baba zetu. Alipokea maneno yaletayo uzima kutoka kwa Mungu, na Musa akatupa sisi Maneno hayo.

39 Lakini baba zetu hawakutaka kumtii Musa. Walimkataa, wakataka kurudi Misri. 40 Walimwambia Haruni, ‘Musa alituongoza kutoka katika nchi ya Misri. Lakini hatujui kilichompata. Hivyo tengeneza miungu ili iwe mbele yetu ituongoze.’(I) 41 Hivyo watu wakatengeneza kinyago kinachofanana na ndama. Kisha wakakitolea sadaka za kuteketezwa. Walifurahia kile walichotengeneza kwa mikono yao wenyewe. 42 Lakini Mungu akawaacha, nao wakaendelea kuabudu nyota na sayari.[c] Kitabu cha manabii[d] kinasema hivi:

‘Watu wa Israeli, hamkunipa dhabihu
    jangwani kwa miaka arobaini.
43 Mlibeba hema kwa ajili ya kumwabudia Moleki,
    na sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani.
Hizi zilikuwa sanamu mlizotengeneza ili mziabudu.
    Hivyo nitawahamishia mbali, kuvuka Babeli.’(J)

44 Baba zetu walikuwa na Hema Takatifu walipokuwa jangwani. Mungu alimwelekeza Musa jinsi ya kutengeneza hema hii. Aliitengeneza kwa kufuata ramani aliyoonyeshwa na Mungu. 45 Baadaye, Yoshua aliwaongoza baba zetu kuteka ardhi ya mataifa mengine. Watu wetu waliingia, na Mungu akawafukuza watu wengine. Watu wetu walipoingia katika ardhi hii mpya, waliibeba hema hii pamoja nao. Watu wetu waliipata hema hii kutoka kwa baba zao, na watu wetu waliitunza mpaka wakati wa Daudi. 46 Mungu alimpenda Daudi.[e] Na Daudi akamwomba Mungu amruhusu ajenge Hekalu kwa ajili ya watu wa Israeli[f] 47 Lakini Sulemani ndiye aliyemjengea Mungu Hekalu.

48 Lakini Mungu Aliye Juu sana hahitaji yumba zilizojengwa kwa mikono ya wanadamu ili aishi ndani yake. Nabii aliandika hivi:

49 ‘Bwana asema, Mbingu ni kiti changu cha enzi,
    na dunia ni sehemu ya kuweka miguu yangu.
Hivyo mnadhani mnaweza kunijengea nyumba?
    Je, ninahitaji mahali pa kupumzika?
50 Kumbukeni, niliumba vitu vyote hivi?’”(K)

51 Kisha Stefano akasema, “Enyi viongozi wa Kiyahudi mlio wakaidi! Mnakataa kumpa Mungu mioyo yenu na mnakataa hata kumsikiliza. Daima mko kinyume na Roho Mtakatifu. Baba zenu walikuwa vivyo hivyo, nanyi mko kama wao! 52 Walimtesa kila nabii aliyewahi kuishi. Waliwaua hata wale ambao zamani zilizopita walisema kwamba Mwenye Haki ilikuwa aje. Na sasa mmekuwa kinyume na Mwenye Haki na mmemwua. 53 Ninyi ndiyo mliipokea Sheria ya Mungu,[g] aliyoitoa kupitia malaika zake. Lakini hamtaki kuitii!”

Stefano Auawa

54 Waliokuwa kwenye mkutano wa baraza waliposikia maneno haya, walikasirika sana na wakamsagia meno Stefano kwa hasira. 55 Lakini Stefano, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alitazama juu mbinguni, na kuuona utukufu wa Mungu. Alimwona Yesu amesimama upande wa kulia wa Mungu. 56 Stefano akasema, “Tazama! Naona mbingu zimefunguka. Na ninamwona Mwana wa Adamu amesimama upande wa kulia wa Mungu.”

57 Kila mmoja pale akaanza kupiga kelele, wakaziba masikio yao kwa mikono yao. Wote kwa pamoja wakamvamia Stefano. 58 Wakamtoa nje ya mji na kuanza kumpiga kwa mawe. Mashahidi walioshuhudia uongo kinyume cha Stefano waliacha makoti yao kwa kijana aliyeitwa Sauli. 59 Walipokuwa wanampiga kwa mawe, Stefano aliomba, akisema, “Bwana Yesu, pokea roho yangu.” 60 Alianguka kwa magoti yake na kupaza sauti, akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii!” Haya yalikuwa maneno yake ya mwisho kabla ya kufa.

Footnotes

  1. 7:4 Ukaldayo Au “Babeli”, nchi iliyo kusini mwa Mesopotamia. Tazama mstari wa 2.
  2. 7:35 Hapa inamaanisha kuwa Musa aliambatana na nguvu za Mungu na ulinzi wa malaika.
  3. 7:42 nyota na sayari Ama jeshi lililoko angani. Nyakati za kale watu waliamini kuwa nyota na sayari zilikuwa miungu au malaika.
  4. 7:42 Kitabu cha manabii Hiki ni kitabu cha manabii wadogo kumi na mbili: Kuanzia Hosea mpaka Malaki.
  5. 7:46 Mungu alimpenda Daudi Au “alipendelewa na Mungu”.
  6. 7:46 watu wa Israeli Kwa maana ya kawaida, “nyumba ya Yakobo”. Nakala zingine za Kiyunani zina “Mungu wa Yakobo”.
  7. 7:53 Sheria ya Mungu Yaani Torati.