Anania Na Safira

Pia mtu mmoja jina lake Anania na mkewe Safira waliuza mali yao. Lakini Anania, kwa makubaliano na mkewe akaficha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobakia kwa mitume.

Petro akamwambia, “Anania, mbona shetani ametawala moyo wako kiasi cha kukubali kumdanganya Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata? Kabla hujauza hilo shamba lilikuwa mali yako. Na hata baada ya kuliuza , fedha ulizopata zilikuwa zako. Kwa nini basi umeamua moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Ujue hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.”

Ujue hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.”

Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini akafa. Na wote waliosikia maneno haya wakajawa na hofu. Vijana wakaingia wakaufunga mwili wake wakamchukua nje kumzika.

Na baada ya muda wa saa tatu mkewe Anania akaingia, naye hakuwa na habari ya mambo yaliyotokea. Petro akamwuliza, “Niambie, je? Mliuza shamba lenu kwa kiasi hiki?” Akajibu, “Ndio, tuliuza kwa kiasi hicho.”

Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje wewe na mumeo mkaamua kumjaribu Roho Mtakatifu wa Bwana? Tazama, vijana waliomzika mumeo wako mlangoni nao watakuchukua nje.”

10 Na mara akaanguka chini akafa. Wale vijana walipoingia wakamwona kuwa amekufa, wakamchukua wakamzika karibu na mumewe. 11 Waamini wote na watu wote waliosikia habari hizi wakajawa na hofu kuu.

Mitume Wafanya Miujiza Mingi Na Maajabu

12 Mitume walifanya miujiza mingi na ishara za ajabu. Na waamini wote walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Sulemani. 13 Hakuna mtu mwingine aliyethubutu kujiunga nao lakini watu wote waliwaheshimu sana. 14 Hata hivyo watu wengi zaidi, wanaume kwa wanawake walikuwa wakiongezeka katika kundi la waliomwamini Bwana. 15 Hata walikuwa wakiwabeba wagonjwa wakawalaza kwenye mikeka barabarani ili Petro alipokuwa akipita kivuli chake kiwa guse angalau baadhi yao, wapone. 16 Pia watu walikusanyika kutoka katika miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu wakileta wagonjwa na watu waliopagawa na pepo wachafu, hao wote wakapo nywa.

Mitume Washitakiwa

17 Kuhani mkuu na wale waliomuunga mkono, yaani Masadukayo, walijawa na wivu, 18 wakawakamata mitume na kuwatia gerezani.

19 Lakini usiku ule malaika wa Bwana akaja akawafungulia milango ya gereza akawatoa nje akawaambia, 20 “Nendeni mkasi mame Hekaluni mkawaambie watu habari za maisha haya mapya!”

21 Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaanza kufundisha watu. Kuhani Mkuu alipowasili pamoja na wenzake wakaitisha mkutano wa baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani. 22 Lakini wale maafisa wal iotumwa walipoingia gerezani hawakuwakuta wale mitume mle. Kwa hiyo wakarudi kutoa ripoti kwa baraza. 23 Wakasema, “Tumekuta milango ya jela imefungwa sawasawa, na maaskari wa gereza wamesi mama nje ya milango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu ye yote ndani.”

24 Mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Hekalu na makuhani wakuu waliposikia ripoti hiyo wakashangaa sana wasijue mambo haya yan geishia wapi. 25 Ndipo mtu mmoja akaja akawaambia, “Wale watu mliowatia gerezani wako Hekaluni wakiwafundisha watu.”

26 Ndipo yule mkuu wa kikosi cha walinzi wa Hekalu na wale maofisa wakaenda wakawaleta mitume lakini hawakuwadhuru kwa sababu waliogopa wangelipigwa mawe na watu. 27 Baada ya kuwaleta wakawaweka mbele ya baraza. Kuhani mkuu akaanza kuwahoji,

28 “Tuliwakanya msifundishe kwa jina la huyu mtu, lakini ninyi mmeeneza mafundisho yenu Yerusalemu yote, na tena mmeamua kuwa sisi tuna hatia juu ya kifo chake.”

29 Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu na sio wanadamu. 30 Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu ambaye ninyi mlimwua kwa kumtundika kwenye msalaba. 31 Mungu alimwinua, akamweka mkono wake wa kuume awe Mtawala na Mwokozi ili awape wana wa Israeli toba na msamaha wa dhambi. 32 Nasi tu mashahidi wa mambo haya pamoja na Roho Mtakatifu aliyetolewa na Mungu kwa watu wanaomtii.”

Mungu kwa watu wanaomtii.”

33 Wajumbe wa baraza la wazee waliposikia haya walijawa na ghadhabu, wakataka kuwaua wale mitume. 34 Lakini mmoja wao, Far isayo aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa sheria aliyeh eshimiwa na watu wote, akasimama akaamuru wale mitume watolewe nje kwa muda.

35 Ndipo alipowaambia wajumbe wa baraza, “Wazee wa Israeli, fikirini kwa uangalifu mtakalowatendea watu hawa! 36 Kumbukeni kuwa sio zamani sana tangu alipotokea mtu aliyeitwa Theuda ambaye alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi mia nne wal ioambatana naye. Lakini aliuawa na wafuasi wake wote wakatawany ika, kazi yake ikawa bure. 37 “Baada yake alitokea Yuda Mgali laya wakati ule wa sensa, akapata wafuasi wengi; lakini naye akauawa nalo kundi lake likatawanyika.

38 “Kwa hiyo, kwa kesi hii nawashauri waacheni watu hawa wala msiwatendee lo lote, kwa maana kama mpango wao na kazi yao ni mambo ya wanadamu hayatafika po pote; 39 lakini ikiwa ni kazi ya Mungu hamtaweza kuwazuia. Badala yake huenda mkajikuta mnam pinga Mungu!”

40 Wakapokea ushauri wa Gamalieli; wakawaita mitume ndani na baada ya kuwachapa viboko wakawaamuru wasifundishe kwa jina la Yesu. Wakawaachia waende zao. 41 Wale mitume walitoka barazani wamejaa furaha kwa sababu Mungu aliwapa heshima ya kupata aibu ya kuchapwa viboko kwa ajili ya jina la Yesu. 42 Na kila siku Hek aluni na nyumbani walizidi kuhubiri na kufundisha bila kukoma, juu ya Habari Njema kwamba Yesu ndiye Kristo.

Anania na Safira

Alikuwepo mtu aliyeitwa Anania na mke wake aliyeitwa Safira. Anania aliuza shamba lake, lakini aliwapa mitume sehemu tu ya pesa alizopata baada ya kuuza shamba lake. Kwa siri alibakiza kiasi cha pesa kwa ajili yake mwenyewe. Mke wake alilijua hili na akalikubali.

Petro akasema, “Anania, kwa nini umemruhusu Shetani aitawale akili yako kwa wazo la namna hii? Umebakiza sehemu ya pesa kwa ajili yako mwenyewe na kumdanganya Roho Mtakatifu! Je, kabla ya kuuza shamba, halikuwa lako? Na hata baada ya kuliuza, ungeweza kutumia pesa kwa namna yoyote unayotaka. Imekuwaje hata ufikirie kufanya jambo hili? Hukutudanganya sisi bali Mungu!”

5-6 Anania aliposikia hili, alianguka chini na kufa. Baadhi ya vijana wakaja na kuufunga mwili wake. Wakautoa nje na kuuzika. Kila mtu aliyelisikia hili aliingiwa hofu.

Baada ya kama saa tatu baadaye, mkewe naye alifika. Safira hakujua kilichompata mumewe. Petro akamwambia, “Niambie mlipata pesa kiasi gani baada ya kuuza shamba lenu. Kilikuwa kiasi hiki?”

Safira akajibu, “Ndiyo, hicho ndicho tulichopata baada ya kuuza shamba.”

Petro akamwambia, “Kwa nini wewe na mume wako mlikubaliana kumjaribu Roho wa Bwana? Sikiliza! Unasikia vishindo hivyo vya miguu? Watu waliomzika mume wako, wako mlangoni. Watakuchukua nje kwa njia hiyo hiyo.” 10 Safira akaanguka miguuni kwa Petro na kufa papo hapo. Vijana wakaingia, walipomwona amekwisha kufa, walimchukua na kumzika kando ya mume wake. 11 Kanisa lote na watu wote waliosikia kuhusu hili waliingiwa hofu.

Uthibitisho kutoka kwa Mungu

12 Mitume walipewa nguvu ya kufanya ishara nyingi za miujiza na maajabu katikati ya watu. Walikuwa wanakutanika pamoja mara kwa mara katika eneo la Hekalu lililoitwa Ukumbi wa Sulemani. 13 Hakuna mtu yeyote ambaye hakuwa mwamini alikaa na kushirikiana nao, lakini kila mtu alisema mambo mazuri juu yao. 14 Watu wengi zaidi na zaidi walimwamini Bwana; na watu wengi, wanaume kwa wanawake waliongezwa katika kundi la waamini. 15 Hivyo watu waliwatoa wagonjwa majumbani na kuwaweka mitaani katika vitanda vidogo na mikeka. Walitumaini kuwa ikiwa Petro atapita karibu yao na kivuli chake kikawaangukia watapona. 16 Watu walikuja kutoka katika miji kuzunguka Yerusalemu. Waliwaleta wagonjwa au waliosumbuliwa na pepo wachafu. Wote waliponywa.

Mitume Wakamatwa

17 Kuhani mkuu na wafuasi wake wote wa karibu, kundi liitwalo Masadukayo wakaingiwa wivu sana. 18 Waliwakamata mitume na kuwafunga katika gereza la mji. 19 Lakini wakati wa usiku, malaika wa Bwana alifungua milango ya gereza. Malaika akawaongoza mitume nje ya gereza na kusema, 20 “Nendeni mkasimame katika eneo la Hekalu. Waelezeni watu kila kitu kuhusu maisha haya mapya.” 21 Mitume waliposikia hili, walifanya kama walivyoambiwa. Walikwenda katika eneo la Hekalu asubuhi na mapema jua lilipokuwa linachomoza na kuanza kuwafundisha watu.

Kuhani mkuu na wafuasi wake wakakusanyika na kuitisha mkutano wa Baraza kuu na wazee wa Kiyahudi. Wakawatuma baadhi ya watu gerezani ili wawalete mitume kwao. 22 Watu wale walipokwenda gerezani, hawakuwaona mitume. Hivyo walirudi na kuwaambia viongozi wa Kiyahudi kuhusu hili. 23 Walisema, “Gereza lilikuwa limefungwa na milango ilikuwa imefungwa. Walinzi walikuwa wamesimama milangoni. Lakini tulipofungua milango, gereza lilikuwa tupu!” 24 Mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani walipolisikia hili, walichanganyikiwa na kujiuliza maana yake ni nini.

25 Ndipo mtu mwingine akaja na kuwaambia, “Sikilizeni! Watu mliowafunga gerezani wamesimama katika eneo la Hekalu wanawafundisha watu!” 26 Mkuu wa walinzi na askari walinzi wa Hekalu walikwenda na kuwarudisha mitume. Lakini askari hawakutumia nguvu, kwa sababu waliwaogopa watu. Waliogopa watu wangewapiga kwa mawe mpaka wafe.

27 Askari waliwaleta mitume na kuwasimamisha mbele ya baraza. Kuhani mkuu akawauliza. 28 Akisema, “Tuliwaambia msifundishe tena kwa kutumia jina lile. Lakini tazameni mlichofanya! Mmeujaza mji wa Yerusalemu kwa mafundisho yenu. Na mnajaribu kutulaumu sisi kwa sababu ya kifo chake.”

29 Petro na mitume wengine wakajibu, “Ni lazima tumtii Mungu, siyo wanadamu! 30 Mlimwua Yesu kwa kumpigilia msalabani. Lakini Mungu, Mungu yule yule wa Baba zetu, alimfufua Yesu kutoka kwa wafu. 31 Yesu ndiye ambaye Mungu amemtukuza kwa kumpa nafasi upande wake wa kuume. Amemfanya kuwa Kiongozi na Mwokozi wetu. Mungu alifanya hivi ili kuwapa watu wote wa Israeli fursa ya kubadilika na kumgeukia Mungu ili dhambi zao zisamehewe. 32 Tuliona mambo haya yote yakitokea, na tunathibitisha kuwa ni ya kweli. Pia, Roho Mtakatifu anaonesha kuwa mambo haya ni ya kweli. Mungu amemtoa Roho huyu kwa ajili ya wote wanaomtii Yeye.”

33 Wajumbe wa Baraza waliposikia haya, walikasirika sana. Walianza kupanga namna ya kuwaua mitume. 34 Lakini mjumbe mmoja wa Baraza, Farisayo aliyeitwa Gamalieli, akasimama, alikuwa mwalimu wa sheria na watu wote walimheshimu. Aliwaambia wajumbe wawatoe nje mitume kwa dakika chache. 35 Kisha akawaambia, “Wanaume wa Israeli, iweni waangalifu kwa kile mnachopanga kuwatendea watu hawa. 36 Mnakumbuka Theuda alipotokea? Alijidai kuwa alikuwa mtu mkuu, na wanaume kama mia nne waliungana naye. Lakini aliuawa na wote waliomfuata walitawanyika. 37 Baadaye, wakati wa sensa, mtu mmoja aitwaye Yuda alikuja kutoka Galilaya. Watu wengi walijiunga kwenye kundi lake, lakini yeye pia aliuawa na wafuasi wake wote walitawanyika. 38 Na sasa ninawaambia, kaeni mbali na watu hawa. Waacheni. Ikiwa mpango wao ni kitu walichopanga wao wenyewe, utashindwa. 39 Lakini ikiwa ni mpango wa Mungu, hamtaweza kuwazuia. Mnaweza kuwa mnapigana kinyume na Mungu mwenyewe!”

Viongozi wa Kiyahudi wakakubaliana na kile alichosema Gamalieli. 40 Wakawaita mitume ndani tena. Wakawachapa viboko na kuwakanya waache kusema na watu kwa kutumia jina la Yesu. Kisha wakawaachia huru. 41 Mitume waliondoka kwenye mkutano wa Baraza, wakifurahi kwamba wamepewa heshima ya kudharauliwa kwa ajili ya Yesu. 42 Mitume hawakuacha kuwafundisha watu. Waliendelea kuzisema Habari Njema, kwamba Yesu ni Masihi. Walifanya hivi kila siku katika eneo la Hekalu na katika nyumba za watu.