Mashtaka Ya Wayahudi Juu Ya Paulo

24 Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania akafika pamoja na baadhi ya wazee na wakili mmoja aitwaye Tertulo. Wakatoa mashtaka yao juu ya Paulo mbele ya Gavana. Na Paulo alipoitwa, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akasema, “Mtukufu Feliksi, kutokana na uongozi wako wa busara tumekuwa na amani ya kudumu na tunatambua ya kuwa mabadiliko mengi muhimu yaliyotokea katika taifa letu yameletwa na uwezo wako wa kuona mbele. Wakati wote na kila mahali tunapokea mambo haya yote kwa shukrani za dhati. Lakini nisije nikakuchosha, nakuomba kwa hisani yako utusikilize kwa muda mfupi. Tumemwona mtu huyu kuwa ni mfanya fujo ambaye ana chochea maasi kati ya Wayahudi dunia nzima. Yeye ni kiongozi wa dhehebu la Wanazareti. Tena alijaribu kulichafua Hekalu letu lakini tulimkamata [tukataka kumhukumu kwa mujibu wa sheria zetu, lakini jemadari Lisia alikuja akamchukua kutoka kwetu kwa kutu mia nguvu akaamuru wanaomshtaki walete mashtaka yao mbele yako]. Wewe mwenyewe ukimwuliza maswali utathibitisha ukweli wa mashtaka yote tunayoleta mbele yako kumhusu yeye.” Wayahudi wakamwunga mkono wakithibitisha kwamba mashtaka yote yalikuwa ya kweli.

Paulo Ajitetea Mbele Ya Feliksi

10 Gavana Feliksi alipomruhusu Paulo ajitetee, yeye alisema, “Najua kwamba wewe umekuwa hakimu katika taifa hili kwa miaka mingi kwa hiyo natoa utetezi wangu bila wasi wasi. 11 Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipokwenda Yerusalemu kuabudu. 12 Hawa wanaonish taki hawakunikuta nikibishana na mtu ye yote au nikianzisha fujo katika Hekalu au katika sinagogi au mahali pengine po pote mjini. 13 Wala hawawezi kabisa kuthibitisha mambo haya wanayon ishtaki. 14 Lakini nakiri mbele yako kuwa mimi namwabudu Mungu wa baba zetu kwa kufuata ile ‘Njia’ ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kilichoandikwa katika Sheria ya Musa na Mana bii 15 na ninalo tumaini kwa Mungu ambalo hata na wao wanaliku bali, kwamba kutakuwa na ufufuo wa wote, walio na haki na wasio na haki. 16 Kwa hiyo ninafanya kila jitihada kuishi nikiwa na dhamiri safi mbele za Mungu na mbele za wanadamu. 17 Basi, baada ya kuwa nje ya Yerusalemu kwa miaka kadhaa nilikuja mjini kuwale tea watu wa taifa langu sadaka kwa ajili ya maskini na kutoa dha bihu. 18 Nilikuwa nimeshatakaswa waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya, na hapakuwa na umati wa watu wala fujo yo yote. 19 Lakini kulikuwa na Wayahudi kutoka Asia, nadhani nao walista hili wawepo hapa mbele yako ili watoe mashtaka yao kama wanalo lo lote la kunishtaki. 20 La sivyo, watu hawa waseme ni kosa gani walilogundua nimefanya niliposhtakiwa mbele ya Baraza, 21 isipo kuwa lile jambo nililotangaza wazi wazi nilipojitetea mbele yao, kwamba, ‘Mimi nimeshtakiwa mbele yenu leo kuhusu ufufuo wa wafu.’

22 Ndipo Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia, akaamua kuahirishwa kwa kesi, akasema, “Mara jemadari Lisia atakapofika nitatoa hukumu yangu juu ya kesi hii.” 23 Akaamuru askari amweke Paulo kizuizini chini ya ulinzi lakini awe na uhuru kiasi, na marafiki zake wasizuiwe kumhudumia. 24 Baada ya siku chache Feliksi akaja na mkewe Drusila ambaye alikuwa Myahudi. Akatuma Paulo aitwe, wakamsikiliza akizungumza juu ya kumwamini Kristo Yesu. 25 Na Paulo alipokuwa akiwaeleza juu ya kuwa na kiasi na juu ya hukumu ya mwisho, Feliksi aliin giwa na hofu akasema, “Tafadhali sasa nenda, nitakuita tena nikipata nafasi.” 26 Wakati huo huo Feliksi alitazamia kwamba Paulo angempatia hongo, kwa hiyo akawa anamwita mara kwa mara kuzungumza naye. 27 Lakini baada ya miaka miwili kupita, Porkio Festo akachukua nafasi ya Feliksi kama Gavana; na kwa sababu Feliksi alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, akamwacha Paulo gere zani.

Baadhi ya Wayahudi Wamshitaki Paulo

24 Siku tano baadaye Anania, kuhani mkuu, alikwenda mjini Kaisaria. Aliwachukua pamoja naye baadhi ya viongozi wa wazee wa Kiyahudi na mwanasheria aitwaye Tertulo. Walikwenda Kaisaria kutoa ushahidi dhidi ya Paulo mbele ya gavana. 2-3 Paulo aliitwa kwenye mkutano, na Tertulo akaanza kueleza mashitaka.

Tertulo alisema, “Mheshimiwa Feliki, kwa muda mrefu watu wetu wamefurahia amani kwa sababu yako, na mambo mengi mabaya katika nchi yetu yanarekebishwa kutokana na msaada wako wa hekima. Kwa hili sisi sote tunaendelea kushukuru. Lakini sitaki kuchukua muda wako mwingi. Hivyo nitasema maneno machache. Tafadhali uwe mvumilivu. Mtu huyu ni mkorofi. Anasababisha vurugu kwa Wayahudi kila mahali ulimwenguni. Ni kiongozi wa kundi la Wanazorayo. 6-8 Pia, alikuwa anajaribu kulinajisi Hekalu, lakini tulimsimamisha.[a] Unaweza kuamua ikiwa haya yote ni kweli. Mwulize maswali wewe mwenyewe.” Wayahudi wengine wakakubali na kusema ndivyo ilivyo.

Paulo Ajitetea Mbele ya Feliki

10 Gavana alifanya ishara ili Paulo aanze kuzungumza. Hivyo Paulo alijibu, “Gavana Feliki, ninafahamu kuwa umekuwa jaji wa nchi hii kwa muda mrefu. Hivyo ninafurahi kujitetea mimi mwenyewe mbele yako. 11 Nilikwenda kuabudu Yerusalemu siku kumi na mbili tu zilizopita. Unaweza kutambua wewe mwenyewe kuwa hii ni kweli. 12 Wayahudi hawa wanaonishitaki, hawakuniona nikibishana na mtu yeyote wala kukusanya kundi la watu Hekaluni. Na sikuwa nabishana au kufanya vurugu kwenye masinagogi au mahali popote katika mji. 13 Watu hawa hawawezi kuthibitisha mambo wanayoyasema dhidi yangu sasa.

14 Lakini nitakuambia hili: Ninamuabudu Mungu, Mungu yule yule aliyeabudiwa na baba zetu, na kama mfuasi wa Njia, ambayo wayahudi hawa wanasema si njia sahihi. Na ninaamini kila kitu kinachofundishwa katika Sheria ya Musa na yote yaliyoandikwa katika vitabu vya manabii. 15 Nina tumaini katika Mungu kama walilonalo Wayahudi hawa, kwamba watu wote, wema na wabaya, watafufuliwa kutoka kwa wafu. 16 Hii ndiyo sababu daima nimejaribu kufanya kile ninachoamini kuwa sahihi mbele za Mungu na kila mtu.

17-18 Nimekuwa mbali na Yerusalemu kwa miaka mingi. Nilikwenda kule nikiwa na fedha za kuwasaidia watu wangu. Pia nilikuwa na sadaka za kutoa Hekaluni. Nilipokuwa nafanya hivyo, baadhi ya Wayahudi waliponiona pale. Nilikuwa nimemaliza ibada ya utakaso.[b] Sikufanya vurugu yoyote, na hakuna watu waliokuwa wamekusanyika kunizunguka. 19 Lakini baadhi ya Wayahudi kutoka Asia walikuwa pale. Walipaswa kuwa hapa mbele yako wakinishtaki ikiwa wana ushahidi kuwa nilifanya kitu chochote kibaya. 20 Waulize watu hawa ikiwa waliona kosa lolote kwangu niliposimama mbele ya mkutano wa baraza kuu mjini Yerusalemu. 21 Jibu pekee watakaloweza kukujibu ni hili: Kwamba nilipokuwa mbele zao nilipaza sauti na kusema, ‘Mnanishitaki leo kwa sababu ninaamini watu watafufuka kutoka kwa wafu!’”

22 Feliki tayari alikuwa anaelewa mengi kuhusu Njia. Akasimamisha kesi na kusema, “Kamanda Lisiasi atakapokuja hapa, nitaamua nini cha kufanya.” 23 Feliki alimwambia ofisa wa jeshi kumlinda Paulo lakini wampe uhuru kiasi na wawaruhusu rafiki zake wamletee chochote atakachohitaji.

Paulo Azungumza na Feliki na Mkewe

24 Baada ya siku chache, Feliki alikuja na mke wake Drusila, aliyekuwa Myahudi. Feliki akaagiza Paulo apelekwe kwake. Alimsikiliza Paulo akiongea kuhusu kumwamini Yesu Kristo. 25 Lakini Feliki aliogopa Paulo alipoongelea kuhusu vitu kama kutenda haki, kuwa na kiasi, na hukumu itakayokuja baadaye. Akasema, “Unaweza kwenda sasa. Nitakapokuwa na muda mwingi, nitakuita.” 26 Lakini Feliki alikuwa na sababu nyingine ya kuzungumza na Paulo. Alitegemea Paulo angempa rushwa, hivyo alimwita Paulo mara nyingi na kuzungumza naye.

27 Lakini baada ya miaka miwili, Porkio Festo akawa gavana. Hivyo Feliki hakuwa gavana tena. Lakini alimwacha Paulo gerezani ili kuwaridhisha Wayahudi.

Footnotes

  1. 24:6-8 Nakala zingine za Kiyunani zimeongeza mstari 6a-8b: “Na tulitaka kumhukumu kwa kutumia sheria zetu wenyewe. Lakini ofisa Lisiasi alikuja na kutumia nguvu kubwa kumchukua kutoka kwetu. Na Lisiasi aliamuru wale wanaotaka kumshitakija waje kwako.”
  2. 24:17-18 ibada ya utakaso Vitu muhimu ambavyo Wayahudi walifanya ili kuikamilisha nadhiri ya mnadhiri. Tazama Mnadhiri katika Orodha ya Maneno.