Malaika Amtoa Petro Gerezani

12 Wakati huu mfalme Herode aliwatesa vikali baadhi ya waamini katika kanisa. Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. Alipoona kuwa kitendo hicho kimewapendeza Wayahudi, akaamuru Petro akamatwe. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate isiyotiwa chachu. Baada ya kumkamata Petro walimweka jela chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, kila kikundi kikiwa na askari wanne. Herode alikuwa amepanga kumtoa Petro mbele ya Wayahudi baada ya Pasaka. Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani; lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii. Usiku ule ambao Herode alikuwa ameamua kumtoa kwa watu, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa kwa minyororo miwili, na askari wengine walikuwa wakilinda nje ya lango la gereza. Mara malaika wa Bwana akatokea, na mwanga ukamulika ndani ya chumba. Yule malaika akampiga Petro ubavuni akamwamsha, akisema, “Haraka! Amka!” Na mara ile minyororo ikaanguka toka mikononi mwa Petro. Yule malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, “Vaa koti lako unifuate.” Petro alitoka mle gere zani akifuatana na malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitokea yalikuwa kweli. Alidhani alikuwa katika ndoto. 10 Wal ipita kituo cha askari wa kwanza, na kituo cha askari wa pili, ndipo wakafika katika lango la chuma la kutokea kuelekea mjini. Lango likafunguka lenyewe, wakatoka nje wakaelekea katika bara bara mojawapo . Mara yule malaika akamwacha Petro. 11 Ndipo Petro alipopata fahamu sawa sawa, akasema, “Sasa nina hakika ya kuwa Bwana amemtuma malaika wake aniokoe kutoka kwa Herode na maovu yote ambayo Wayahudi walikuwa wamekusudia kunitendea.”

12 Baada ya kutambua alipokuwa, Petro alikwenda nyumbani kwa Maria, mama yake Yohana Marko, ambako waamini wengi walikuwa wamekutana kwa maombi. 13 Petro alipobisha hodi mlangoni, mfany akazi msichana aitwaye Roda, akaja kumfungulia.

Lakini ali potambua sauti ya Petro, alirudi mbio kwa furaha kuwaambia wen gine kuwa Petro yuko nje, hata akasahau kumfungulia . 15 Wakam wambia yule msichana, “Una kichaa!” Lakini yeye alisisitiza kwamba ilikuwa ni kweli amesikia sauti ya Petro. Wakasema, “Ni malaika wake.” 16 Wakati huo Petro aliendelea kugonga mlangoni; nao walipofungua mlango wakamwona Petro, walistaajabu sana. 17 Lakini yeye aliwaashiria wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa jela. Akawaambia, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Akaondoka akaenda sehemu nyingine. 18 Kulipopam bazuka kukawa na hekaheka huko gerezani. Askari wakawa wanauli zana kuhusu yaliyompata Petro. 19 Herode akaamuru msako ufanyike lakini waliposhindwa kumpata Petro, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri hao askari wauawe. Basi Herode akatoka Yudea akaenda Kaisaria, akakaa huko.

Kifo Cha Herode

20 Herode alikuwa amekasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Watu wa miji hiyo miwili wakaungana pamoja wakapeleka wajumbe wakaonane na Herode. Wajumbe hao wakapata kibali cha Blasto, mtumishi mwaminifu wa Mfalme Herode, ili waonane na mfalme kutaka amani kwa kuwa miji hiyo ilipata chakula chake kutoka katika milki ya mfalme. 21 Siku ya hao wajumbe kumwona mfalme ilipofika, Herode alivaa mavazi rasmi ya kifalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi akaanza kutoa hotuba. 22 Alipokuwa akihutubu watu walimshangilia, wakapiga kelele wakisema, “Hii ni sauti ya Mungu! Sio sauti ya mwanadamu!” 23 Mara malaika wa Bwana akampiga Herode; akaliwa na funza akafa kwa sababu hakumpa Mungu utukufu. 24 Lakini neno la Mungu liliendelea kuenea na waamini wakaongezeka sana. 25 Barnaba na Sauli walipomaliza kazi yao walirudi Yerusalemu wakiwa pamoja na Yohana Marko.

Matatizo Mengi kwa waamini

12 Katika wakati huu huu, Mfalme Herode akaanza kuwatesa baadhi ya waamini waliokuwa sehemu ya kanisa. Aliamuru Yakobo aliyekuwa kaka yake Yohana, auawe kwa upanga. Herode alipoona kuwa Wayahudi wamelifurahia jambo hili, aliamua kumkamata Petro pia. Hii lilitokea katika kipindi cha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Alimkamata Petro na kumfunga gerezani, ambako alilindwa na kundi la askari kumi na sita.[a] Herode alipanga kumleta Petro mbele ya watu ili ahukumiwe, lakini alisubiri mpaka baada ya sikukuu ya Pasaka. Hivyo Petro aliwekwa gerezani lakini kanisa lilikuwa likiomba kwa Mungu bila kuacha kwa ajili yake.

Petro Atolewa Nje ya Gereza

Wakati wa usiku kabla ya siku ambayo Herode alipanga kumhukumu mbele ya watu, Petro, akiwa amefungwa minyororo miwili, alikuwa amelala katikati ya askari wawili. Na askari waliokuwa nje ya mlango walikuwa wanalinda gereza. Ghafla malaika wa Bwana alikuwa amesimama pale, na chumba kilijaa mwanga. Malaika akamwamsha Petro kwa kumpiga upande, akasema, “Amka haraka!” Minyororo ikaanguka kutoka mikono mwa Petro. Malaika akasema, “Vaa nguo na viatu vyako.” Petro alifanya kama alivyoambiwa. Kisha malaika akasema, “Vaa koti lako na unifuate.”

Hivyo malaika akatoka nje na Petro alimfuata. Hakujua kama kweli malaika alikuwa anafanya hili. Alidhani alikuwa anaona maono. 10 Petro na malaika wakavuka lindo la kwanza na lindo la pili. Kisha walifika kwenye lango la chuma lililowatenganisha na mji. Lango likafunguka. Baada ya kuvuka lango na kutembea umbali wa kama mtaa mmoja, malaika akatoweka ghafla.

11 Ndipo Petro akatambua kuwa haikuwa ndoto. Akawaza moyoni akisema, “Sasa ninajua kwamba Bwana hakika alimtuma malaika wake kwangu. Ameniokoa kutoka kwa Herode na kutoka kwenye mabaya yote ambayo Wayahudi walidhani yatanipata.”

12 Petro alipotambua hili, alikwenda nyumbani kwa Mariamu, mama yake Yohana, aliyeitwa Marko. Watu wengi walikuwa wamekusanyika pale wakiomba. 13 Petro alibisha kwenye mlango wa nje. Mtumishi wa kike aliyeitwa Rhoda alikuja ili afungue mlango. 14 Alipoitambua sauti ya Petro, alifurahi sana hata akasahau kufungua mlango. Akakimbilia ndani na kuliambia kundi, “Petro yuko mlangoni!” 15 Waamini wakamwambia, “Wewe una kichaa!” Lakini alipoendelea kusema kwamba ni kweli Petro yuko mlangoni. Waamini walisema, “Lazima atakuwa malaika wa Petro.”

16 Lakini Petro aliendelea kubisha mlangoni. Waamini walipoufungua mlango na kumwona, wakashangaa. 17 Petro akawafanyia ishara kwa mkono wake kuwaambia wanyamaze. Akawaeleza namna Bwana alivyomtoa nje ya gereza. Akasema, “Mwambieni Yakobo na ndugu wengine kilichotokea.” Kisha akawaacha na kwenda sehemu nyingine.

18 Siku iliyofuata askari walichanganyikiwa. Walijiuliza nini kimempata Petro. 19 Herode alimtafuta kila mahali lakini hakumpata. Hivyo aliwahoji walinzi na kuamuru wauawe.

Kifo cha Herode Agripa

Baadaye, Herode alihama kutoka Uyahudi na kwenda katika mji wa Kaisaria na kukaa huko kwa muda. 20 Herode aliwakasirikia sana watu katika miji ya Tiro na Sidoni. Lakini miji hii ilihitaji chakula kutoka katika nchi yake, hivyo baadhi yao walimjia wakitaka amani naye. Waliweza kumshawishi Blasto mtumishi binafsi wa Mfalme ili awasaidie.

21 Herode alichagua siku maalumu ya kukutana nao. Siku hiyo alivaa vazi zuri la kifalme. Aliketi kwenye kiti chake cha enzi na kuwahutubia watu. 22 Watu wakapaza sauti zao na kusema, “Hii ni sauti ya mungu, siyo mwanadamu!” 23 Herode hakumpa Mungu utukufu. Hivyo malaika wa bwana akampiga kwa ugonjwa. Akaliwa na minyoo ndani na kufa.

24 Ujumbe wa Mungu ulikuwa unasambaa, ukiwafikia watu wengi zaidi.

25 Baada ya Barnaba na Sauli kumaliza kazi yao Yerusalemu, walirudi Antiokia, walimchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao.

Footnotes

  1. 12:4 kundi la askari kumi na sita Askari hawa walikuwa na zamu ya kulinda ya askari wanne wanne.