Mpango Wa Kumwua Yesu

26 Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, “Mnafahamu kwamba sikukuu ya Pasaka inaanza baada ya siku mbili na mimi Mwana wa Adamu nitasalitiwa na kusulubiwa.”

Wakati huo makuhani wakuu na wazee walifanya mkutano katika ukumbi wa kuhani mkuu, jina lake, Kayafa. Wakashauriana jinsi ya kumkamata Yesu na kumwua kwa siri. Wakasema, “Lakini tusi fanye haya wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.”

Yesu Anapakwa Mafuta Bethania

Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, mwa namke mmoja alimjia akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya thamani kubwa; akammiminia Yesu manukato hayo kichwani akiwa ame kaa mezani. Lakini wanafunzi wake walipoona hayo waliudhika, wakasema, “Kwa nini kupoteza manukato bure? Haya yangaliuzwa kwa bei kubwa na fedha hizo wakapewa maskini.”

10 Yesu alifahamu mawazo yao kwa hiyo akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mama? Amenifanyia jambo zuri sana. 11 Maskini mnao siku zote lakini hamtakuwa nami siku zote. 12 Aliponimimi nia haya manukato alikuwa akiandaa mwili wangu kwa mazishi. 13 Ninawaambia kweli, mahali po pote Habari Njema itakapohubi riwa ulimwenguni, jambo hili alilofanya litatajwa, kwa ukumbusho wake.”

Yuda Akubali Kumsaliti Yesu

14 Kisha mmojawapo wa wale wanafunzi kumi na wawili aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa kuhani mkuu akamwambia, “Mtanilipa kiasi gani nikimtoa kwenu?” 15 Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. 16 Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti Yesu.

Matayarisho Ya Pasaka

17 Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate isiotiwa chachu wale wanafunzi walikuja kwa Yesu wakamwuliza, “Ungependa tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”

18 Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini mkamwambie, ‘Bwana anasema hivi: saa yangu imekaribia, napenda kula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu nyumbani kwako.’ ” 19 Wanafunzi waka fanya kama Yesu alivyowaambia, wakaandaa Pasaka.

20 Ilipofika jioni, Yesu aliketi mezani pamoja na wanafunzi wake. 21 Walipokuwa wakila akawaambia, “Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti.” 22 Wakasikitika sana, wakaanza kumwul iza mmoja mmoja, “Ni mimi, Bwana?” 23 Yesu akawaambia, “Yule aliyechovya mkono wake katika bakuli pamoja nami, ndiye ata kayenisaliti. 24 Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama ilivy oandikwa katika Maandiko, lakini ole wake mtu yule atakayenisal iti. Ingalikuwa nafuu kwake kama hakuzaliwa!”

25 Kisha Yuda, yule ambaye alimsaliti akasema, “Ni mimi, Bwana?” Yesu akamjibu, “Umetamka mwenyewe.”

Bwana?” Yesu akamjibu, “Umetamka mwenyewe.”

26 Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, “Chukueni mle; huu ni mwili wangu.” 27 Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa akisema, “Kunyweni nyote katika kikombe hiki. 28 Hii ni damu yangu ya agano ambayo inamwagika kwa ajili ya wengi ili wasame hewe dhambi. 29 Ninawahakikishia kuwa sitakunywa tena maji ya mzabibu mpaka siku nitakapoyanywa pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu.”

Baba yangu.”

30 Walipokwisha kuimba wimbo walikwenda kwenye mlima wa Mizeituni.

Yesu Amwambia Petro Atamkana

31 Kisha Yesu akawaambia, “Usiku wa leo kila mmoja wenu atanikimbia kwa maana Maandiko yanasema, ‘Nitampiga mchungaji, na kondoo wote wa kundi lake watatawanyika.’ 32 Lakini baada ya kufufuka, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

33 Petro akasema, “Hata kama wote watakuacha, mimi sitaku acha.”

34 Yesu akamjibu, “Ninakuambia kweli, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” 35 Lakini Petro akasema, “Hata kama itabidi nife pamoja na wewe, sitakukana.” Na wana funzi wote wakasema hivyo hivyo.

Gethsemane

36 Kisha Yesu akaenda nao mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane. Akawaambia, “Kaeni hapa, mimi ninakwenda mbele zaidi kuomba.” 37 Akamchukua Petro, pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kufadhaika na kuhuzunika. 38 Kisha Yesu akawaambia, “Moyo wangu umejaa majonzi karibu ya kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami.”

39 Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, “Baba yangu, kama inawezekana, niondolee kikombe hiki cha mateso, lakini si kama nipendavyo bali kama upendavyo wewe.”

40 Akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamwul iza Petro, “Hamkuweza kukesha nami hata kwa saa moja? 41 Kesheni muombe, msije mkaingia katika majaribu. Kwa maana roho i radhi lakini mwili ni dhaifu.” 42 Akaenda tena mara ya pili, akaomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kion dolewe pasipo mimi kukinywea, mapenzi yako yafanyike.” 43 Ali porudi tena aliwakuta wamelala kwa maana macho yao yalikuwa mazito. 44 Kwa hiyo akawaacha akaenda tena mara ya tatu, akaomba vile vile.

45 Kisha akarudi kwa wale wanafunzi akawaambia, “Bado mme lala na kupumzika? Angalieni, saa imefika ambapo mimi Mwana wa Adamu sina budi kukabidhiwa mikononi mwa wenye dhambi. 46 Amkeni, twendeni! Yule anayenisaliti atafika sasa hivi!”

Yesu Akamatwa

47 Alipokuwa anazungumza, Yuda, mmojawapo wa wale kumi na wawili, akafika,akifuatana na umati wa watu wenye mapanga na mar ungu. Walikuwa wametumwa na makuhani wakuu na wazee wa watu.

48 Yuda alikuwa amepatana na hao watu kuwa, ‘Nitakayembusu ndiye, mkamateni.’ 49 Basi alipofika, alimwendea Yesu moja kwa moja, akamsalimia, “Salaam, Rabi!” Akambusu. 50 Yesu akamjibu, “Rafiki, umekuja kufanya nini hapa?” Basi wale watu wakasogea, wakamkamata Yesu. 51 Ndipo mmojawapo wa wafuasi wa Yesu ali poona hivyo, akachukua panga lake, akampiga nalo mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 52 Yesu akamwambia, “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote watumiao upanga watakufa kwa upanga. 53 Unadhani siwezi kumwomba Baba yangu aniletee mara moja majeshi kumi na mbili ya malaika? 54 Lakini nikifanya hivyo yatatimiaje Maandiko yale yasemayo kwamba mambo haya lazima yato kee?”

55 Wakati huo Yesu akawaambia ule umati, “Mmekuja kunika mata kama mnyang’anyi kwa mapanga na marungu? Mbona siku zote nilikaa Hekaluni na kufundisha lakini hamkunikamata? 56 Lakini haya yametokea ili Maandiko ya manabii yatiimie.” Ndipo wana funzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.

Yesu Ashtakiwa Mbele Ya Baraza

57 Wale waliomkamata Yesu wakampeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu, ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekutanika.

58 Lakini Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa kuhani mkuu akaingia ndani pamoja na walinzi aone litakalotokea. 59 Basi makuhani wakuu na baraza zima wakatafuta ushahidi wa uongo ili wamwue Yesu, 60 lakini hawakupata, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza. Hatimaye wakajitokeza watu wawili, 61 wakasema: “Huyu mtu alisema, ‘Nina uwezo wa kuvunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena katika muda wa siku tatu .’ ”

62 Kisha kuhani mkuu akasimama, akamwambia Yesu, “Huna jibu? Husikii huo ushahidi waliotoa watu hao?” 63 Lakini Yesu hakusema neno. Basi kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha kwa jina la Mungu aliye hai, tuambie kama wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu.”

Mungu.”

64 Yesu akajibu, “Umetamka mwenyewe. Lakini nina waambieni nyote kwamba baada ya hapa, mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wa Mungu mwenye uweza na akija juu ya mawingu ya mbin guni.”

65 Aliposikia maneno hayo, kuhani mkuu alirarua mavazi yake akasema, “Amekufuru! Tunahitaji ushahidi gani zaidi? Si mmemsi kia akikufuru? 66 Mnaamuaje?” Wakajibu, “Anastahili kufa!”

67 Kisha wakamtemea mate usoni; wengine wakampiga ngumi na makofi, 68 wakasema, “Hebu toa unabii wewe Kristo! Ni nani ame kupiga?”

69 Wakati huo Petro alikuwa amekaa uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.” 70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui usemalo.”

71 Kisha alipotoka nje, mlangoni mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwapo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 72 Akakana tena kwa kiapo akisema, “Simfa hamu mtu huyo!” 73 Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesi mama pale walimwendea Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao kwa maana namna yako ya kusema ni kama yao.” 74 Ndipo Petro akalaani na kuapa, akawaambia, “Simfahamu mtu huyo!” Wakati huo huo jogoo akawika. 75 Na Petro akakumbuka Yesu alivyomwambia, “Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu.” Akaenda nje, akalia kwa uchungu.

Mpango wa Kumwua Yesu

(Mk 14:1-2; Lk 22:1-2; Yh 11:45-53)

26 Yesu alipomaliza akasema haya yote, akawaambia wafuasi wake, “Mnajua kuwa kesho kutwa ni Pasaka. Siku hiyo Mwana wa Adamu atakabidhiwa kwa maadui zake ili auawe msalabani.”

Ndipo viongozi wa makuhani na wazee walikutana katika nyumba ya Kayafa kuhani mkuu. Katika mkutano huo walitafuta njia ya kumkamata na kumwua Yesu kwa siri pasipo mtu yeyote kujua. Wakasema, “Hatuwezi kumkamata Yesu wakati wa sherehe ya Pasaka. Hatutaki watu wakasirike na kusababisha vurugu.”

Mwanamke Ampa Yesu Heshima

(Mk 14:3-9; Yh 12:1-8)

Yesu alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simoni aliyekuwa na ugonjwa mbaya sana wa ngozi. Mwanamke alimwendea, akiwa na chupa yenye manukato ya thamani kubwa. Yesu akiwa anakula, mwanamke huyo akamwagia manukato hayo kichwani.

Wanafunzi walipomwona mwanamke akifanya hivi walimkasirikia. Walisema, “Kwa nini kuharibu manukato hayo? Yangeuzwa na pesa nyingi ingepatikana, na pesa hiyo wangepewa maskini.”

10 Lakini Yesu alijua kilichokuwa kinaendelea. Akasema, “Kwa nini mnamsumbua mwanamke huyu? Amenifanyia jambo zuri sana. 11 Mtaendelea kuishi na maskini siku zote.[a] Lakini ninyi hamtakuwa nami siku zote. 12 Mwanamke huyu amenimwagia manukato. Amefanya hivi kuniandaa kwa ajili ya mazishi baada ya kufa. 13 Habari Njema itahubiriwa kwa watu wote ulimwenguni. Na ninaweza kuwathibitishia kuwa kila mahali ambako Habari Njema zitahubiriwa, jambo alilofanya mwanamke huyu litahubiriwa pia, na watu watamkumbuka.”

Yuda Akubali Kuwasaidia Adui wa Yesu

(Mk 14:10-11; Lk 22:3-6)

14 Ndipo Yuda Iskariote, mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu alikwenda kuzungumza na wakuu wa makuhani. 15 Akasema, “Nikimkabidhi Yesu kwenu, mtanilipa nini?” Makuhani walimpa sarafu thelathini za fedha. 16 Kuanzia siku hiyo, Yuda alianza kutafuta muda mzuri wa kumsaliti Yesu.

Karamu ya Pasaka

(Mk 14:12-21; Lk 22:7-14,21-23; Yh 13:21-30)

17 Ilipofika siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wafuasi wake walimjia Yesu na kumwambia, “Tutaandaa kila kitu kwa ajili yako ili ule mlo wa Pasaka. Unataka tuandae wapi mlo wa Pasaka?”

18 Yesu akajibu, “Nendeni mjini kwa mtu ninayemfahamu. Mwambieni kuwa Mwalimu anasema, ‘Muda uliowekwa kwa ajili yangu umekaribia sana. Mimi na wafuasi wangu tutakula mlo wa Pasaka katika nyumba yako.’” 19 Walitii na kufanya kama Yesu alivyowaambia. Waliandaa mlo wa Pasaka.

20 Jioni ilipowadia, Yesu alikuwa ameketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 21 Walipokuwa wakila Yesu akasema, “Niaminini, ninapowaambia kuwa mmoja wenu ninyi kumi na wawili atanikabidhi kwa maadui zangu.”

22 Wanafunzi walisikitika sana waliposikia hili. Kila mmoja akasema, “Bwana, hakika si mimi!”

23 Yesu akajibu, “Yeye aliyechovya mkate wake katika kikombe kile kile nilichochovya mimi ndiye atakayenisaliti. 24 Mwana wa Adamu atakiendea kifo chake kama Maandiko yanavyosema. Lakini ole wake mtu yule anayemsaliti Mwana wa Adamu ili auawe. Ni bora mtu huyo asingezaliwa.”

25 Ndipo Yuda, ambaye ndiye angemsaliti, akamwambia Yesu, “Mwalimu, hakika si mimi unayemzungumzia, ama ndiye?”

Yesu akamjibu, “hicho ndicho unachosema.”

Chakula cha Bwana

(Mk 14:22-26; Lk 22:15-20; 1 Kor 11:23-25)

26 Walipokuwa wakila, Yesu alichukua baadhi ya mikate na akamshukuru Mungu. Alimega baadhi ya vipande, akawapa wafuasi wake na akasema, “Chukueni mkate huu na mle. Ni mwili wangu.”

27 Kisha akachukua kikombe chenye divai, akamshukuru Mungu na akawapa. Akasema, “Kila mmoja wenu anywe divai iliyo katika kikombe hiki. 28 Divai hii ni damu yangu, itakayomwagika ili kusamehe dhambi za watu wengi na kuanza Agano Jipya ambalo Mungu analifanya na watu wake. 29 Ninataka mjue kuwa, hii ni mara ya mwisho nitakunywa divai mpaka siku ile nitakapokunywa divai mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”

30 Waliimba wimbo kwa pamoja kisha wakaenda kwenye Mlima wa Mizeituni.

Yesu Asema Wafuasi Wake Watamwacha

(Mk 14:27-31; Lk 22:31-34; Yh 13:36-38)

31 Yesu akawaambia wafuasi wake, “Usiku wa leo ninyi nyote mtapoteza imani yangu kwangu. Maandiko yanasema,

‘Nitamwua mchungaji,
    na kondoo watatawanyika.’(A)

32 Lakini baada ya kuuawa, nitafufuka Kisha nitakwenda Galilaya. Nitakuwa huko kabla ninyi hamjaenda huko.”

33 Petro akajibu, “Wafuasi wengine wote wanaweza kupoteza imani juu yako. Lakini imani yangu haitatetereka.”

34 Yesu akajibu, “Ukweli ni huu, usiku wa leo utasema haunifahamu. Utanikana mara tatu kabla jogoo hajawika.”

35 Lakini Petro akajibu, “Sitasema kwamba sikufahamu! Mimi hata nitakufa pamoja nawe!” Na wafuasi wengine wote wakasema kitu hicho hicho.

Yesu Aomba Akiwa Peke Yake

(Mk 14:32-42; Lk 22:39-46)

36 Kisha Yesu akaondoka pamoja na wafuasi wake na kwenda mahali panapoitwa Gethsemane. Akawaambia, “Kaeni hapa wakati ninakwenda mahali pale kuomba.” 37 Alimwambia Petro na wana wawili wa Zebedayo waende pamoja naye. Kisha akaanza kuhuzunika na kuhangaika. 38 Yesu akamwambia Petro na wana wa Zebedayo, “Moyo wangu ni mzito na wenye huzuni hata kujisikia kana kwamba huzuni hiyo itaniua. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami.”

39 Kisha Yesu akaenda mbele kidogo. Akainama hadi chini uso wake ukiigusa nchi akiomba na akasema, “Baba yangu, ikiwezekana, usifanye nikinywee kikombe hiki cha mateso.[b] Lakini fanya lile ulitakalo na si lile ninalolitaka mimi.” 40 Kisha akarudi walipokuwa wafuasi wake na akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Je hamkuwa na uwezo wa kukesha pamoja nami hata kwa saa moja? 41 Amkeni kesheni na kuomba ili muyashinde majaribu. Roho zenu zinataka kufanya mambo sahihi, lakini miili yenu ni dhaifu.”

42 Kisha Yesu akaenda mara ya pili na akaomba akisema, “Baba yangu, ikiwa ni lazima nikinywee kikombe hiki na haiwezekani nikakwepa, basi mapenzi yako na yatimizwe.”

43 Kisha akarudi na kwenda walipokuwa wafuasi wake, akawakuta wamelala tena. Hawakuweza kukesha. 44 Hivyo akawaacha akaenda tena kuomba. Mara hii ya tatu alipokuwa anaomba akasema kama alivyosema hapo mwanzo.

45 Kisha Yesu akawarudia wafuasi wake na akasema, “Bado mnalala na kupumzika? Wakati wa Mwana wa Adamu kukabidhiwa kwa wenye dhambi umewadia. 46 Simameni! Tuondoke. Tazama yeye atakayenikabidhi anakuja.”

Yesu Akamatwa

(Mk 14:43-50; Lk 22:47-53; Yh 18:3-12)

47 Yesu alipokuwa anazungumza, Yuda mmoja wa wanafunzi wake kumi na mbili alifika akiwa na kundi kubwa la watu, waliokuwa wamebeba majambia na marungu. Walikuwa wametumwa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 48 Yuda aliyekuwa amkabidhi Yesu kwao, alipanga kufanya kitu cha kuwajulisha yupi kati ya wafuasi alikuwa Yesu. Alisema, “Mtu nitakayembusu ndiye mtakayemkamata.” 49 Hivyo Yuda alikwenda kwa Yesu na kumwambia, “Salamu, Mwalimu!” Kisha akambusu.

50 Yesu akajibu, “Rafiki yangu, fanya ulilokuja kufanya.”

Kisha wale watu wakaja na kumkamata Yesu. 51 Jambo hili lilipotokea, mmoja wa wafuasi wa Yesu alichukua jambia lake na kumkata sikio mtumishi wa kuhani mkuu.

52 Yesu akamwambia, “Rudisha jambia lako mahali pake. Atumiaye jambia atauawa kwa jambia. 53 Hakika unajua kuwa ningemwomba Baba yangu yeye angenipa zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika. 54 Lakini hilo lisingekubaliana na yale Maandiko, yanayosema hivi ndivyo ilivyopasa itokee.”

55 Kisha Yesu akaliambia kundi, “Kwa nini mnakuja kunikamata mkiwa na mikuki na marungu kama vile mimi ni mhalifu? Nimekuwa nakaa eneo la Hekalu nikifundisha kila siku. Kwa nini hamkunikamata kule? 56 Lakini mambo haya yote yametokea ili kutimiza Maandiko yaliyoandikwa na manabii.” Ndipo wafuasi wake wote wakamwacha na kukimbia.

Yesu Akiwa Mbele ya Viongozi wa Kidini

(Mk 14:53-65; Lk 22:54-55,63-71; Yh 18:13-14,19-24)

57 Wale waliomkamata Yesu wakampeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu. Walimu wa Sheria na viongozi wazee wa Kiyahudi walikuwa wamekusanyika huko. 58 Petro alimfuata Yesu lakini alikuwa mbali kidogo. Alimfuata mpaka katika ua wa nyumba ya kuhani mkuu. Petro alienda uani na akakaa pamoja na walinzi. Alitaka kuona nini kingetokea.

59 Viongozi wa makuhani na baraza kuu walijaribu kutafuta kosa ili waweze kumwua Yesu. Walijaribu kutafuta watu ili wadanganye kuwa Yesu alifanya kosa. 60 Watu wengi walikuja na akasema uongo kuhusu Yesu. Lakini baraza lilishindwa kupata ushahidi wa kuutumia ili kumwua. Ndipo watu wawili walikuja 61 na akasema, “Mtu huyu[c] alisema, ‘Ninaweza kuliharibu Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.’”

62 Kisha kuhani mkuu alisimama na kumwambia Yesu, “Huna neno lolote la kujitetea dhidi ya mashtaka haya juu yako? Wanasema kweli?” 63 Lakini Yesu hakusema neno lolote.

Kisha kuhani mkuu akamwambia Yesu, “Apa mbele za Mungu aliye hai kwamba utatuambia kweli. Je, wewe ni Masihi, Mwana wa Mungu?”

64 Yesu akajibu, “Unaweza akasema hivyo, Mimi ndiye. Lakini ninawaambia, kitambo kidogo mtamwona Mwana wa Adamu akiwa amekaa upande wa kuume wa Mungu, mwenye Nguvu. Na mtamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni.”

65 Kuhani mkuu aliposikia hili, alilarua vazi lake kwa hasira. Akasema, “Mtu huyu amemtukana Mungu! Hatuhitaji mashahidi zaidi. Ninyi nyote mmesikia matusi yake. 66 Mnasemaje?”

Viongozi wa Kiyahudi wakajibu, “Ana hatia, na ni lazima afe.”

67 Na baadhi ya waliokuwa pale wakamtemea mate Yesu usoni na kumpiga makonde na wengine walimpiga makofi. 68 Wakasema, “Tuonyeshe kuwa wewe ni nabii, Masihi! Nani amekupiga!”

Petro Amkana Yesu

(Mk 14:66-72; Lk 22:56-62; Yh 18:15-18,25-27)

69 Petro alipokuwa amekaa nje uani, msichana mtumishi akamwendea. Akasema, “Ulikuwa pamoja na Yesu, yule mtu kutoka Galilaya.”

70 Lakini Petro akamwambia kila mtu aliyekuwa pale kuwa si kweli. Akasema “Sijui unachosema.”

71 Kisha akaondoka uani. Akiwa kwenye lango msichana mtumishi akamwona na akawaambia watu waliokuwa pale, “Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti.”

72 Kwa mara nyingine tena Petro akasema hakuwa pamoja na Yesu. Akasema, “Ninaapa kwa Mungu, simfahamu mtu huyu!”

73 Baada ya muda mfupi baadaye, watu waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro na kumwambia, “Tunajua wewe ni mmoja wao. Hata namna unavyoongea inaonesha wazi kuwa ndivyo hivyo.”

74 Kisha Petro akaanza kujiapiza mwenyewe ikiwa anaongopa. Akasema, “Ninaapa kwa Mungu, simfahamu mtu huyu!” Mara alipomaliza akasema hili, jogoo akawika. 75 Kisha akakumbuka maneno alivyoambiwa na Yesu kuwa: “Kabla jogoo hajawika, utakuwa umenikana mara tatu.” Kisha Petro akatoka nje na kulia kwa uchungu sana.

Footnotes

  1. 26:11 Mtaendelea kuishi na maskini siku zote Tazama Kum 15:11.
  2. 26:39 kikombe Kikombe ni ishara ya mateso. Yesu alitumia dhana ya kukinywea kikombe akimaanisha kuyakubali mateso ambayo angeyapata katika matukio ya kutisha ambayo yangetokea muda mfupi ujao.
  3. 26:61 Mtu huyu Yaani, Yesu. Adui zake walikuwa wanakwepa kutamka jina lake.