Kifo Cha Yesu Msalabani

33 Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu. 34 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” 35 Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, “Mnamsikia? Anamwita

Eliya!”

36 Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!”

37 Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.

39 Yule askari aliyekuwa amesimama mbele ya msalaba alipoona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

40 Walikuwapo pia wanawake walio kuwa wakiangalia mambo haya kwa mbali. Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na pia Salome . 41 Hawa walifuatana na Yesu alipokuwa Galilaya na kumhudumia. Pia walikuwapo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja naye Yerusalemu.

Read full chapter