Add parallel Print Page Options

Yesu Amponya Asiyeona

(Mt 20:29-34; Lk 18:35-43)

46 Kisha wakafika Yeriko. Yesu alipokuwa akiondoka mjini na wanafunzi wake pamoja na umati wa watu, Bartimayo mwana wa Timayo, ombaomba asiyeona, alikuwa amekaa kando ya barabara. 47 Aliposikia kwamba huyo alikuwa ni Yesu wa Nazareti, alianza kupiga kelele na kusema, “Yesu Mwana wa Daudi, unihurumie!”

48 Na watu wengi walimkemea na kumwambia anyamaze kimya. Lakini yeye alipiga kelele kwa sauti kubwa zaidi na kusema, “Mwana wa Daudi, unihurumie!”

49 Kwa hiyo Yesu akasimama na kusema, “Hebu mwiteni.”

Nao wakamwita yule mtu asiyeona na kumweleza, “Jipe moyo mkuu! Inuka! Yesu anakuita.” 50 Naye akalitupa joho lake, akaruka juu, na akamwendea Yesu.

51 Naye Yesu akamwambia, “Unataka nikufanyie nini?”

Yule mtu asiyeona akamwambia, “Mwalimu, nataka kuona tena.”

52 Hivyo Yesu akamwambia, “Nenda! Imani yako imekuponya.”[a] Na mara akaweza kuona tena, na akamfuata Yesu barabarani.

Read full chapter

Footnotes

  1. 10:52 imekuponya Kiyunani kinatumia neno hilo hilo kuwa na maana ya neno kuponya na kumaanisha kuokoa.