Add parallel Print Page Options

Yesu Aonekana Akiwa na Musa na Eliya

(Mt 17:1-8; Mk 9:2-8)

28 Baada ya siku kama nane tangu Yesu aseme maneno haya, aliwachukua Petro, Yohana na Yakobo, akapanda mlimani kuomba. 29 Yesu alipokuwa akiomba, uso wake ulianza kubadilika. Nguo zake zikawa nyeupe, zikang'aa. 30 Kisha watu wawili walikuwa pale, wakiongea naye. Walikuwa Musa na Eliya; 31 Wao pia walionekana waking'aa na wenye utukufu. Walikuwa wanazungumza na Yesu kuhusu kifo chake kitakachotokea Yerusalemu. 32 Petro na wenzake walikuwa wanasinzia. Lakini waliamka na kuuona utukufu wa Yesu. Waliwaona pia watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 33 Musa na Eliya walipokuwa wanaondoka, Petro akasema, “Mkuu, ni vizuri tuko hapa. Tutajenga vibanda vitatu hapa, kimoja kwa ajili ya kukutukuza wewe, kingine kwa ajili kumtukuza Musa na kingine wa ajili ya kumtukuza Eliya.” Petro hakujua alichokuwa anasema.

34 Petro alipokuwa akisema mambo haya, wingu likaja, likawafunika wote. Petro, Yohana na Yakobo waliogopa walipofunikwa na wingu. 35 Sauti ikatoka katika wingu na kusema, “Huyu ni Mwanangu. Ndiye niliyemchagua. Mtiini yeye.”

36 Sauti hiyo ilipomalizika, Yesu peke yake ndiye alikuwa pale. Petro, Yohana na Yakobo hawakusema chochote. Na kwa muda mrefu baada ya hilo, hawakumwambia mtu yeyote yale waliyoyaona.

Read full chapter

Bwana Yesu Abadilika Sura

28 Yapata siku nane baada ya kusema hayo, Yesu alikwenda kusali mlimani pamoja na Petro, Yakobo na Yohana. 29 Alipokuwa akiomba, sura yake ili badilika, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta na kung’aa. 30 Ghafla wakawepo watu wawili wakaanza kuzungumza naye. Walikuwa ni Musa na Eliya! 31 Nao walionekana katika utukufu wakizungumza na Yesu kuhusu kifo chake ambacho kingetokea Yerusalemu.

32 Petro na wenzake ambao walikuwa wamelala usingizi mzito waliamka wakaona utukufu wa Yesu na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 33 Musa na Eliya walipoanza kuondoka, Petro akamwambia Yesu, “Bwana ni vizuri mno kwamba tuko hapa! Tutajenga vibanda vitatu - kimoja chako, kingine cha Musa na kin gine cha Eliya.” Lakini Petro hakujua anasema nini. 34 Petro alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu kubwa na kivuli chake kikawafunika, na wale wanafunzi wakashikwa na hofu lile wingu lilipowafikia. 35 Sauti ikatoka kwenye wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu niliyemchagua, msikilizeni yeye.” 36 Baada ya sauti hiyo kusema, alionekana Yesu peke yake. Wale wanafunzi wakakaa kimya na kwa wakati huo hawakumwambia mtu ye yote yale waliyoy aona.

Read full chapter