Add parallel Print Page Options

Yesu Amponya Mgonjwa

(Mt 8:1-4; Mk 1:40-45)

12 Wakati mmoja Yesu alikuwa katika mji ambao mwanaume mmoja mgonjwa alikuwa anaishi. Mwanaume huyo alikuwa na ugonjwa mbaya sana wa ngozi mwili wake wote. Alipomwona Yesu, alimsujudia na kumsihi akisema, “Bwana, ikiwa unataka una uwezo wa kuniponya.”

13 Yesu akasema, “Hakika ninataka kukuponya, upone!” Kisha akamgusa, na ugonjwa ukatoweka papo hapo. 14 Yesu akamwambia, “Usimwambie mtu yeyote kilichotokea. Lakini nenda kwa kuhani akakuchunguze.[a] Na umtolee Mungu sadaka ambazo Musa aliamuru watu wanaoponywa watoe, ili iwe ushahidi kwa watu kwamba umepona.”

15 Lakini habari kuhusu Yesu zilizidi kuenea zaidi. Watu wengi walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. 16 Mara nyingi Yesu alikwenda sehemu zingine zisizokuwa na watu na akaomba huko.

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:14 kuhani akakuchunguze Sheria ya Musa ilisema ni lazima kuhani aamue ikiwa mtu aliyekuwa na ukoma amepona.