Add parallel Print Page Options

15 Kila mtu alitarajia kuja kwa Masihi,[a] na walijiuliza wakisema, “Labda Yohana ndiye Masihi.”

16 Yohana aliwajibu watu wote, akasema, “Ninawabatiza ninyi katika maji, lakini yupo mwingine ajaye baada yangu, mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, huyo atafanya mengi zaidi yangu. Nami niliye mtumwa wa chini kabisa sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Yeye huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 17 Yuko tayari sasa kuja kusafisha nafaka. Atatenganisha nafaka nzuri na makapi, na kuiweka katika ghala yake kisha ataichoma ile isiyofaa katika moto usiozimika.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:15 Masihi Ni neno la Kiebrania lililo na maana sawa na Kristo kwa Lugha ya Kiyunani (Kigiriki), maana yake ni Mpakwa Mafuta.

15 Siku hizo watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wakijiuliza mioyoni mwao kama Yohana ndiye Kristo.

16 Yohana aliwajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini anayekuja ni mkuu kuliko mimi, sistahili hata kuwa mtumwa wake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

17 “Yuko tayari na pepeto lake mkononi, tayari kusafisha mahali pake pa kukusanyia mazao. Nafaka safi ataiweka ghalani lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.”

Read full chapter