Add parallel Print Page Options

Dhambi na Msamaha

(Mt 18:6-7,21-22; Mk 9:42)

17 Yesu akawaambia wafuasi wake, “Mambo yanayosababisha watu kutenda dhambi yatatokea hakika. Lakini ole wake mtu anayesababisha hili litokee. Ingekuwa vizuri kwa mtu huyo kama jiwe la kusagia lingefungwa shingoni mwake, na akatupwa baharini, kuliko kusababisha mmojawapo wa wanyenyekevu hawa kutenda dhambi.

Read full chapter

17 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Majaribu yanayowafanya watu watende dhambi hayana budi kuwepo. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. Ingekuwa nafuu kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito shingoni na kuzamishwa baharini kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi.

Read full chapter