Yesu alipomaliza kuwaambia watu mambo haya alikwenda Kaper naumu. Huko mtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi ambaye bwana wake alimpenda, alikuwa mgonjwa sana, karibu ya kufa. Jemadari huyo aliposikia habari za Yesu aliwatuma wazee wa Kiyahudi wakam wombe aje kumponya mtumishi wake. Wale wazee walipofika kwa Yesu walimsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, “Mtu huyu anastahili msaada wako kwani yeye analipenda taifa letu, tena ametujengea sinagogi.”

Hivyo Yesu akaongozana nao. Hata alipoikaribia nyumba yake, yule jemadari aliwatuma rafiki zake, kumwambia Yesu, “Bwana, usijisumbue kuingia nyumbani kwangu. Sistahili heshima kubwa kiasi hicho, wala sikuona ninastahili mimi kuja kukuona binafsi. Sema neno moja tu na mtumishi wangu atapona. Katika nafasi yangu ya kazi nina wakubwa wangu na wapo askari wengine chini ya mamlaka yangu. Nikitoa amri kwa askari, ‘Nenda!’ huenda; nikimwambia mwingine, ‘Njoo!’ huja; na nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hiki,’ hufanya.” Yesu aliposikia maneno haya alishangaa sana. Akawageukia wale watu walioongozana naye aka waambia, “Hata katika Israeli yote sijakutana na mtu mwenye imani kama hii.” 10 Na wale waliotumwa kwa Yesu waliporudi nyumbani kwa yule jemadari walikuta yule mtumishi amepona kabisa.

Yesu Amfufua Mtoto Wa Mjane

11 Baada ya siku hiyo, Yesu alikwenda mji mmoja uitwao Naini. Wanafunzi wake na umati wa watu waliongozana naye. 12 Alipokaribia njia ya kuingia mjini alikutana na watu wal iobeba maiti wakitoka nje ya mji. Marehemu alikuwa mtoto wa kiume wa pekee wa mama mmoja mjane na umati wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mama. 13 Bwana Yesu alipomwona yule mjane moyo wake ulijaa huruma, akamwambia, “Usilie.” 14 Kisha akalisoge lea lile jeneza akaligusa na wale waliolibeba wakasimama. Ndipo akasema: “Kijana nakuambia, amka!” 15 Yule aliyekuwa marehemu akaamka, akakaa na akaanza kusema! Yesu akamkabidhi kwa mama yake.

16 Watu wote wakajawa na hofu. Wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kutuokoa sisi watu wake.” 17 Habari hizi za mambo aliyofanya Yesu zikaenea Uyahudi nzima na sehemu za jirani.

Hakuna Aliye Mkuu Kuliko Yohana

18 Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walipomweleza Yohana habari hizi zote aliwaita wawili kati yao 19 akawatuma wakamwulize Bwana Yesu, “Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?”

201 Walipofika kwa Yesu wakamwambia, “Yohana Mbatizaji ametutuma tukuulize, ‘Wewe ndiye yule ajaye au tumtazamie mwin gine?”’

21 Wakati huo huo, Yesu aliwaponya wengi waliokuwa na magonjwa, maumivu na pepo wachafu. Pia akawawezesha vipofu wengi kuona. 22 Ndipo akawajibu wale wanafunzi waliotumwa, “Nendeni mkamwambie Yohana yote mliyoyaona na kusikia: vipofu wanapata kuona, vilema wanatembea, wenye ukoma wanapona, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanasikia Habari Njema. 23 Amebari kiwa mtu asiyepoteza imani yake kwangu.” 24 Wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuwaeleza watu juu ya Yohana: “Hivi mlipokwenda nyikani mlikwenda kuona nini? Nyasi zikipeperushwa na upepo? 25 Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa nguo za fahari? Sidhani! Watu wanaovaa nguo za fahari na kuishi maisha ya anasa hukaa katika majumba makubwa. 26 Sasa mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kuona nabii? Naam! Tena aliye mkuu kuliko nabii. 27 Huyu Yohana ndiye anayezungumzwa katika Maandiko yase mayo: ‘Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie, ili akuandalie njia.’ 28 Nawaambia, kati ya binadamu wote, hakuna aliye mkuu kumzidi Yohana. Hata hivyo aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana. 29 Watu wote waliosikia maneno hayo, ikiwa ni pamoja na watoza ushuru, walimtukuza Mungu kwa kuwa wao waliukubali ubatizo wa Yohana. 30 Bali Mafarisayo na wanasheria walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokukubali kubatizwa na Yohana. 31 Yesu akawau liza, “Niseme nini juu ya watu wa kizazi hiki? Niwafananishe na nini? 32 Wao wamefanana na watoto waliokaa sokoni wakijibizana na wenzao wakisema: ‘Tuliwaimbia nyimbo za shangwe, hamkucheza. Tuliwaimbia nyimbo za msiba, hamkuomboleza.’ 33 Yohana Mbatizaji alikuwa akifunga na hakuonja divai maishani mwake, ninyi mkasema, ‘Ana wazimu!’ 34 Lakini mimi nakula na kunywa, nanyi mnasema: ‘Mtazameni mlafi na mlevi! Rafiki wa watoza kodi na wenye dhambi.’ 35 Lakini hekima ya Mungu inadhihirishwa kuwa kweli na wote wanaoipokea.”

Mwanamke Aliyempaka Yesu Manukato

36 Farisayo mmoja alimwalika Yesu nyumbani kwake kwa chak ula. Naye akaenda akakaa ale chakula. 37 Katika mji ule palikuwa na mwanamke mmoja kahaba. Naye aliposikia kuwa Yesu atakula nyum bani kwa yule Farisayo, alichukua chupa ya alabasta iliyojaa man ukato 38 akaenda, akakaa nyuma ya Yesu, karibu na miguu yake. Kisha akaanza kulia, machozi yake yakidondokea miguuni mwa Yesu, akayafuta kwa nywele zake. Huku akimbusu miguu na kuimiminia yale manukato.

39 Yule Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Huyu mtu hawezi kuwa ni nabii. Kama ange kuwa nabii angetambua kuwa huyu mwanamke ni kahaba.” 40 Kisha Yesu akijua mawazo ya yule Farisayo akamwambia, “Simoni, kuna jambo nataka kukuambia.” Simoni akajibu “Sema, mwalimu.” 41 “Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: mmoja shillingi elfu tano na mwingine shillingi mia tano. 42 Wote wawili wakashindwa kulipa madeni yao, kwa hiyo akaamua kuwasamehe. Unadhani kati yao, ni yupi aliyempenda zaidi yule aliyewasamehe?” 43 Simoni akajibu, “Nadhani ni yule aliyesame hewa deni kubwa zaidi.” Yesu akamwambia, “Umejibu sawa.” 44 Ndipo akamgeukia yule mwanamke akamwambia Simoni, “Unamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako hukunipa maji ya kunawa miguu, lakini huyu ameniosha miguu kwa machozi yake na kunifuta kwa nywele zake. 45 Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke amekuwa akiibusu miguu yangu tangu niingie hapa. 46 Hukunipaka mafuta kichwani kama ilivyo desturi lakini huyu mwanamke ameipaka miguu yangu manukato. 47 Kwa hiyo nakuambia, upendo mkubwa aliouonyesha huyu mama unathibitisha kuwa dhambi zake ambazo ni nyingi zimesamehewa. Lakini ye yote asamehewaye kidogo, huonyesha upendo kidogo.”

48 Akamwambia yule mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.” 49 Ndipo wale wageni wengine waliokuwepo wakaanza kuulizana, “Hivi huyu ni nani, hata aweze kusamehe dhambi?” 50 Yesu akam wambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”

Yesu Amponya Mtumishi wa Afisa wa Jeshi

(Mt 8:5-13; Yh 4:43-54)

Yesu alipomaliza kuwaambia watu mambo yote aliyotaka kuwaambia, alikwenda mjini Kapernaumu. Afisa wa jeshi katika mji wa Kapernaumu alikuwa na mtumishi aliyekuwa wa muhimu sana kwake. Mtumishi huyu alikuwa mgonjwa sana karibu ya kufa. Afisa huyu aliposikia kuhusu Yesu, aliwatuma baadhi ya viongozi wa wazee wa Kiyahudi kwa Yesu. Aliwataka wamwombe Yesu aende kumponya mtumishi wake. Wazee walikwenda kwa Yesu, wakamsihi amsaidie afisa. Walisema, “Mtu huyu anastahili msaada wako, Kwa sababu anawapenda watu wetu na ametujengea sinagogi.”

Hivyo Yesu alikwenda nao. Alipoikaribia nyumba ya yule afisa, afisa aliwatuma rafiki zake kumwambia Yesu, “Bwana, huhitaji kufanya kitu chochote maalumu kwa ajili yangu. Sistahili wewe uingie nyumbani mwangu. Ndiyo maana sikuja mimi mwenyewe kwako. Unahitaji kutoa amri tu na mtumishi wangu atapona. Ninajua hii, kwa kuwa ninaelewa mamlaka. Kuna watu wenye mamlaka juu yangu, na nina askari walio chini ya mamlaka yangu. Nikimwambia askari mmoja ‘nenda’, huenda. Na nikimwambia mwingine ‘njoo’, huja. Pia nikimwambia mtumwa wangu ‘fanya hiki’, hunitii.”

Yesu aliposikia hayo alishangaa, akawageukia watu waliokuwa wanamfuata, akawaambia, “Ninawaambia, Sijawahi kuona imani kubwa namna hii hata katika Israeli.”

10 Kundi lililotumwa kwa Yesu waliporudi nyumbani, walimkuta yule mtumishi amepona.

Yesu Amfufua Kijana wa Mama Mjane

11 Siku iliyofuata Yesu na wafuasi wake walikwenda katika mji wa Naini. Kundi kubwa la watu walisafiri pamoja nao. 12 Yesu alipolikaribia lango la mji, aliona watu wamebeba maiti. Alikuwa ni mwana pekee wa mama mjane. Watu wengi kutoka mjini walifuatana na yule mama mjane. 13 Bwana alipomwona yule mama, alimwonea huruma na kumwambia, “Usilie.” 14 Akakaribia, akaligusa jeneza. Wanaume waliokuwa wamebeba jeneza wakasimama. Ndipo Yesu akamwambia kijana aliyekufa, “Kijana, nakuambia, inuka!” 15 Yule kijana, akaketi, akaanza kuongea. Yesu akamrudisha kwa mama yake.

16 Kila mtu aliingiwa hofu. Wakaanza kumsifu Mungu na kusema, “Nabii mkuu yuko hapa pamoja nasi!” na “Mungu amekuja kuwasaidia watu wake!”

17 Habari hii kuhusu Yesu ikaenea katika Uyahudi yote, na kila sehemu kuzunguka pale.

Yohana Atuma Watu Kumwuliza Yesu Swali

(Mt 11:2-19)

18 Wafuasi wa Yohana Mbatizaji walimweleza Yohana Mbatizaji kuhusu mambo haya yote. Naye aliwaita wanafunzi wake wawili. 19 Akawatuma waende na kumwuliza Yesu, “Wewe ndiye tuliyesikia anakuja, au tumsubiri mwingine?”

20 Wafuasi wa Yohana walipofika kwa Yesu, wakasema, “Yohana Mbatizaji ametutuma kwako tukuulize: ‘Wewe ndiye yule ajaye, au tumsubiri mwingine?’”

21 Wakati ule ule Yesu alikuwa amewaponya watu wengi madhaifu na magonjwa yao. Aliwaponya waliokuwa na pepo wabaya na kuwafanya wasiyeona wengi kuona. 22 Kisha aliwaambia wanafunzi wa Yohana, “Nendeni mkamweleze Yohana yale mliyoyaona na kuyasikia: wasiyeona wanaona, walemavu wa miguu wanatembea, wenye magonjwa mabaya ya ngozi wanatakasika, wasiyesikia wanasikia. Waliokufa wanafufuliwa na Habari Njema inahubiriwa kwa maskini. 23 Heri wale wasio na mashaka kunikubali mimi.”[a]

24 Baada ya wanafunzi wa Yohana kuondoka, Yesu akaanza kuwaambia watu kuhusu Yohana, “Mlitoka kwenda jangwani kuona nini? Mtu aliyekuwa dhaifu, kama unyasi unaotikiswa na upepo? 25 Mlitegemea kuona nini? Mtu aliyevaa mavazi mazuri? Hakika si hilo. Watu wanaovaa mavazi mazuri na kuishi kwa anasa wako katika majumba ya wafalme. 26 Sasa, mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Ndiyo, Yohana ni nabii. Lakini ninawaambia, Yohana ni zaidi ya nabii. 27 Andiko hili liliandikwa kuhusu Yohana:

‘Sikiliza! Nitamtuma mjumbe mbele yako.
    Yeye ataandaa njia kwa ajili yako.’(A)

28 Ninawaambia, hakuna aliyewahi kuzaliwa aliye mkuu kuliko Yohana. Lakini mwenye umuhimu mdogo, katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana.”

29 (Watu waliposikia hili, wote walikubali kuwa mafundisho ya Mungu yalikuwa mazuri. Hata watoza ushuru waliobatizwa na Yohana walikiri. 30 Lakini Mafarisayo na wanasheria walikataa kuukubali mpango wa Mungu kwa ajili yao; hawakumruhusu Yohana awabatize.)

31 “Niseme nini kuhusu watu wa wakati huu? Niwafananishe na nini? Wanafanana na nini? 32 Ni kama watoto waliokaa sokoni. Kundi moja la watoto likawaita watoto wengine na kusema,

‘Tuliwapigia filimbi
    lakini hamkucheza.
Tuliwaimba wimbo wa huzuni,
    lakini hamkulia.’

33 Yohana Mbatizaji alikuja na hakula chakula cha kawaida au kunywa divai. Nanyi mkasema, ‘Ana pepo ndani yake.’ 34 Mwana wa Adamu amekuja anakula na kunywa. Mnasema, ‘Mwangalieni anakula sana na kunywa sana divai. Ni rafiki wa watoza ushuru na watenda dhambi wengine.’ 35 Lakini hekima huoneshwa kuwa sahihi kwa wale wanaoikubali.”

Yesu na Mwanamke Mwenye Dhambi

36 Mmoja wa Mafarisayo alimwalika Yesu kula chakula nyumbani mwake. Yesu akaenda nyumbani kwa yule Farisayo, akaketi[b] katika nafasi yake sehemu ya kulia chakula.

37 Alikuwepo mwanamke mmoja katika mjini ule aliyekuwa na dhambi nyingi. Alipojua kuwa Yesu alikuwa anakula chakula nyumbani kwa Farisayo, alichukua chupa kubwa yenye manukato ya thamani sana. 38 Alisimama karibu na miguu ya Yesu akilia. Kisha alianza kuisafisha miguu ya Yesu kwa machozi yake na akaifuta kwa nywele zake, akaibusu mara nyingi na kuipaka manukato.

39 Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona hili, alijisemea moyoni mwake, “Mtu huyu angekuwa nabii, angetambua kuwa mwanamke huyu anayemgusa ni mwenye dhambi.”

40 Katika kujibu kile Farisayo alichokuwa akifikiri, Yesu akasema, “Simoni nina kitu cha kukwambia.”

Simoni akajibu, “Nieleze, Mwalimu.”

41 Yesu akasema, “Kulikuwa watu wawili. Wote wawili walikuwa wanadaiwa na mkopeshaji mmoja. Mmoja alidaiwa sarafu mia tano za fedha, na wa pili sarafu hamsini za fedha. 42 Watu wale hawakuwa na fedha, hivyo hawakuweza kulipa madeni yao. Lakini mkopeshaji aliwasamehe wote wawili. Kati ya wote wawili ni yupi atakayempenda mkopeshaji zaidi?”

43 Simoni akajibu, “Nafikiri ni yule aliyekuwa anadaiwa fedha nyingi.”

Yesu akamwambia, “Umejibu sawa.” 44 Kisha akamgeukia yule mwanamke na kumwambia Simoni, “Unamwona mwanamke huyu? Nilipoingia nyumbani mwako hukunipa maji ili ninawe miguu yangu. Lakini mwanamke huyu ameniosha miguu yangu kwa machozi yake na kuikausha kwa nywele zake. 45 Wewe hukunisalimu kwa busu, lakini amekuwa akinibusu miguu yangu tangu nilipoingia. 46 Hukuniheshimu kwa mafuta kwa ajili ya kichwa changu, lakini yeye amenipaka miguu yangu manukato yanayonukia vizuri. 47 Ninakwambia kuwa dhambi zake zilizo nyingi zimesamehewa. Hii ni wazi, kwa sababu ameonesha upendo mkubwa. Watu wanaosamehewa kidogo hupenda kidogo.”

48 Kisha akamwambia mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.”

49 Watu waliokaa naye sehemu ya chakula wakaanza kusema mioyoni mwao, “Mtu huyu anadhani yeye ni nani? Anawezaje kusamehe dhambi?”

50 Yesu akamwambia mwanamke, “Kwa sababu uliamini, umeokolewa kutoka katika dhambi zako. Nenda kwa amani.”

Footnotes

  1. 7:23 Heri … kunikubali mimi Au “Baraka kuu ni kwa wale wasio na mashaka kunikubali.”
  2. 7:36 akaketi Waliketi kwa kujilaza kidogo kuelekea katika meza ya chakula katika mzunguko, miguu yao ikiwa imenyooka kwa nyuma.