Kuzaliwa Kwa Yesu

Siku zile Kaisari Augusto, mtawala wa milki ya Kirumi, aliamuru ya kwamba watu wote wa milki yake waandikishwe. Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza kufanyika nayo ilitokea wakati Kirenio alipokuwa liwali wa Siria. Watu wote walikwenda katika sehemu walikozaliwa ili waandikishwe huko. Yusufu alitoka mji wa Nazareti uliopo Galilaya akaenda mpaka Bethlehemu mji wa Daudi kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi. Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na mchumba wake Mariamu ambaye kwa wakati huu alikuwa mja mzito.

Walipokuwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu kujifungua uli fika, naye akamzaa mtoto wa kiume, kifungua mimba. Akamfunika kwa vinguo na kumlaza horini, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.

Wachungaji Wapata Habari

Usiku ule walikuwako wachungaji wakilinda kondoo zao nje ya mji. Ghafla malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Mungu ukawang’azia pande zote. Wakajawa na hofu kuu. 10 Lakini malaika akawatuliza akisema: “Msiogope! Nawaletea habari njema ya furaha kubwa, na habari hii ni kwa faida ya watu wote! 11 Kwa maana leo katika mji wa Bethlehemu, amezaliwa Mwokozi ambaye ndiye Kristo Bwana. 12 Na hivi ndivyo mtakavyomtambua: mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa vinguo na kulazwa horini.”

13 Mara jeshi kubwa la malaika wa mbinguni likatokea na pamoja wakamsifu Mungu wakiimba: 14 “Atukuzwe Mungu juu mbin guni, na duniani iwepo amani kwa watu ambao amependezwa nao.”

15 Malaika hao waliporudi mbinguni wale wachungaji walish auriana: “Jamani, twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotokea, ambayo Bwana ametufahamisha.”

16 Kwa hiyo wakaenda haraka Bethlehemu, wakawakuta Mariamu na Yusufu; na yule mtoto mchanga alikuwa amelala mahali pa kulia ng’ombe. 17 Walipomwona mtoto, wakawaeleza yale waliyokuwa wameambiwa. 18 Na wote waliosikia habari hizi wakastaajabia yale waliyoambiwa na wachungaji. 19 Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake, akayafikiria mara kwa mara.

20 Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kum sifu kwa yale waliyoyasikia na kuyaona.

21 Hata baada ya siku nane, ilipotimia siku ya kumtahiri mtoto, aliitwa Yesu; jina alilopewa na malaika kabla hata haja chukuliwa mimba.

Yesu Apelekwa Hekaluni

22 Baada ya kutimia kwa muda wa utakaso wa Yusufu na Mar iamu, kwa mujibu wa sheria ya Musa, walimpeleka mtoto Yerusalemu, wakamtoa kwa Bwana 23 kama ilivyotakiwa na sheria ya Bwana -“Kila mtoto wa kiume wa kwanza atakabidhiwa kwa Bwana.” 24 Pia walitoa sadaka, kama ilivyotakiwa na sheria ya Bwana: “Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.” 25 Na alikuwepo huko Yerusalemu mzee mmoja jina lake Simeoni ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Siku zote alikuwa akitarajia ukombozi wa Israeli na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Pia Roho Mtaka tifu alikuwa amemhakikishia kuwa hangekufa kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Kwa hiyo, akiwa ameongozwa na Roho Mtaka tifu, Simeoni alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Yesu ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 Simeoni alimpokea mtoto mikononi mwake akamshukuru Mungu akisema: 29 “Sasa Bwana, niruhusu mimi mtumishi wako niende kwa amani kama ulivyoniahidi, 30 kwa sababu macho yangu yameuona wokovu 31 ulioandaa mbele ya watu wote, 32 nuru itakayowaangazia watu wa mataifa na kuleta utukufu kwa watu wako Israeli.” 33 Wazazi wa mtoto walistaajabu kwa yale yaliyokuwa yakisemwa kumhusu mtoto wao. 34 Simeoni akawabariki. Kisha akamwambia Mariamu, mama yake, “Mtoto huyu amechaguliwa na Mungu kwa makusudi ya kuanga mizwa na kuokolewa kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ya onyo kutoka kwa Mungu ambayo watu wengi wataikataa 35 ili kudhi hirisha mawazo yao ya ndani. Na uchungu kama kisu kikali utaku choma moyoni.” 36-37 ,Tena, alikuwepo Hekaluni nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti wa Fanueli, wa kabila la Asheri. Nabii Ana alikuwa mjane wa miaka themanini na minne naye alikuwa ameolewa kwa miaka saba tu mumewe akafariki. Yeye aliishi humo Hekaluni daima, akimwabudu Mungu na kuomba na kufunga.

38 Wakati huo huo, Ana alikuja mbele akamshukuru Mungu na kueleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wakitarajia ukombozi wa Yerusalemu. 39 Yusufu na Mariamu walipokamilisha mambo yote yaliyotakiwa na sheria ya Mungu, walirudi nyumbani kwao Nazareti katika Wilaya ya Galilaya. 40 Yesu aliendelea kukua, akawa kijana mwenye nguvu na hekima, akijaa baraka za

Mtoto Yesu Adhihirisha Hekima Yake

41 kila mwaka wazazi wake walikwenda Yerusalemu kushiriki katika siku kuu ya Pasaka. 42 Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama desturi ilivyokuwa. 43 Sikukuu ilipokwisha walianza safari ya kurudi nyumbani. Yesu akabaki Yerusalemu pasipo wazazi wake kujua. 44 Wao walidhani yupo nao kwenye msafara kwa hiyo wakaenda mwendo wa siku nzima. Walipotambua kwamba hawakuwa naye, walianza kumtafuta kati ya jamaa na marafiki. 45 Hawakumpata, kwa hiyo wakarudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu wakamkuta Hek aluni ameketi kati ya walimu wa sheria, akiwasikiliza na kuwau liza maswali. 47 Wote waliomsikia walistaajabishwa na uwezo wake mkubwa wa kuelewa na majibu aliyoyatoa.

48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Mama yake akamwul iza: “Mwanangu, mbona umetufanyia hivi? Baba yako na mimi tume hangaika kukutafuta kila mahali kwa wasiwasi mkubwa.” 49 Lakini yeye akajibu: “Kwa nini mlihangaika kunitafuta? Hamkujua ninge kuwa hapa Hekaluni kwenye nyumba ya Baba yangu? 50 Lakini wao hawakuelewa maana ya jibu lake.

51 Akarudi pamoja na wazazi wake hadi Nazareti. Akawa aki watii, na mama yake akayaweka moyoni mambo haya yote. 52 Basi Yesu akaendelea kuongezeka katika kimo na hekima, akipendwa na

Kuzaliwa kwa Yesu

(Mt 1:18-25)

Ulikuwa wakati ambapo amri ilitolewa na Kaisari Augusto kwamba watu wote wanaoishi katika utawala wote wa Rumi[a] wahesabiwe na kuorodheshwa[b] katika kumbukumbu za serikali. Orodha hii ilikuwa ya kwanza tangu Kirenio alipokuwa gavana wa Shamu. Kila mtu alikwenda katika mji aliozaliwa ili akahesabiwe na kuingizwa katika orodha hiyo.

Hivyo Yusufu alitoka Nazareti, mji uliokuwa katika jimbo la Galilaya na kwenda katika mji wa Bethlehemu uliokuwa katika jimbo la Uyahudi. Pia, mji huu ulijulikana kama mji wa Daudi. Yusufu alikwenda Bethlehemu kwa sababu alikuwa mzaliwa wa ukoo wa Daudi. Yusufu alijiandikisha akiwa pamoja na Mariamu kwani alikuwa tayari amemchumbia ili amwoe. Na Mariamu alikuwa mjamzito. Yusufu na Mariamu walipokuwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu kujifungua ulifika. Akamzaa mwanawe wa kwanza. Akamvingirishia nguo vizuri, kisha akamlaza katika hori la kulishia mifugo.[c] Walimweka humo kwa sababu chumba cha wageni kilikuwa kimejaa.

Wachungaji wa Mifugo Wajulishwa Kuhusu Yesu

Usiku ule, baadhi ya wachungaji walikuwa mashambani nje ya mji wa Bethlehemu wakilinda kondoo zao. Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukaangaza kuwazunguka, wakaogopa sana. 10 Malaika akawaambia, “Msiogope, kwa kuwa nimewaletea habari njema zitakazowafurahisha watu wa Mungu wote. 11 Kwa sababu leo katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo,[d] Bwana. 12 Na hivi ndivyo mtakavyomtambua: Mtamkuta mtoto mchanga amevingirishiwa nguo na amelala katika hori la kulishia mifugo.”

13 Kisha malaika pamoja na jeshi kubwa la mbinguni wakaanza kumsifu Mungu, wakisema:

14 “Atukuzwe Mungu juu mbinguni,
    na amani iwepo duniani
    kwa watu wote wanaompendeza.”

15 Malaika walipoondoka kurudi mbinguni, wale wachungaji wakaambiana wakisema, “Twendeni Bethlehemu, tukalione jambo hili lililotokea, ambalo Bwana ametujulisha.”

16 Wakaenda haraka, wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala katika hori la kulishia mifugo. 17 Wachungaji walipomwona huyo mtoto, walisimulia kile walichoambiwa na malaika kuhusu mtoto. 18 Kila aliyesikia maelezo ya wachungaji, alishangaa. 19 Mariamu aliendelea kuyatafakari mambo haya, na kuyaweka moyoni. 20 Wachungaji waliirudia mifugo yao, wakawa wanamsifu na kumshukuru Mungu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona. Ilikuwa kama walivyoambiwa na malaika.

21 Ilipofika siku ya nane mtoto alitahiriwa, akaitwa Yesu. Hili ndilo jina alilopewa na malaika kabla mama yake hajaibeba mimba yake.

Yesu Atambulishwa Hekaluni

22 Muda wa kutakaswa ulimalizika, kama ilivyotakiwa na Sheria ya Musa baada ya mtoto kuzaliwa.[e] Baada ya hapo walimpeleka Yesu Yerusalemu na kumweka mbele za Bwana. 23 Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana: Mzaliwa wa kwanza akiwa mtoto wa kiume, atolewe wakfu kwa ajili ya Bwana.[f] 24 Pia Mariamu na Yusufu walikwenda Yerusalemu kutoa dhabihu kama Sheria ya Bwana inavyosema kuwa, “Ni lazima utoe dhabihu ya jozi moja ya hua[g] au makinda mawili wa njiwa.”

Simeoni Amwona Yesu

25 Alikuwepo mtu mmoja aliyeishi katika mji wa Yerusalemu, mtu huyu aliitwa Simeoni. Alikuwa mtu mwema na mcha Mungu na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. Alikuwa akiusubiri wakati ambao Mungu angeisaidia Israeli. 26 Roho Mtakatifu alimwambia kwamba asingekufa kabla ya kumwona Masihi kutoka kwa Bwana. 27 Roho Mtakatifu alimwongoza mpaka Hekaluni. Hivyo, alikuwemo Hekaluni wakati Mariamu na Yusufu walipomleta mtoto Yesu ili wamfanyie kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Kiyahudi. 28 Simeoni alimbeba mtoto Yesu mikononi mwake, akamshukuru Mungu na kusema,

29 “Sasa, Bwana, niruhusu mimi mtumishi wako nife kwa amani
    kwa kuwa umeitimiza ahadi yako kwangu.
30 Nimeona kwa macho yangu namna utakavyowaokoa watu wako.
31     Sasa watu wote wanaweza kuuona mpango wako.
32 Yeye ni mwanga wa kuionesha njia yako kwa mataifa mengine,
    na atawaletea heshima watu wako Israeli.”

33 Mariamu na Yusufu walishangazwa sana na maneno aliyosema Simeoni kuhusu Yesu. 34 Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu; “Wayahudi wengi wataanguka na wengi watainuka kwa sababu ya mtoto huyu. Atakuwa ishara kutoka kwa Mungu, lakini baadhi ya watu watamkataa. 35 Mawazo ya siri ya watu wengi yatajulikana. Na mambo yatakayotokea yatakuumiza, kama upanga unaokuchoma moyoni.”

Ana Amwona Yesu

36 Alikuwapo nabii aliyeitwa Ana binti Fanueli, kutoka katika kabila la Asheri. Alikuwa mwanamke mzee sana. Aliishi na mume wake kwa miaka saba, 37 kabla ya mume wake kufa na kumwacha peke yake. Na sasa alikuwa na umri wa miaka themanini na nne. Ana alikuwa Hekaluni daima, hakutoka. Alimwabudu Mungu kwa kufunga na kuomba usiku na mchana.

38 Simeoni alipokuwa anazungumza na Yusufu na Mariamu, Ana alikwenda walipokuwa na akaanza kumsifu Mungu na kuwaambia kuhusu Yesu watu wote waliokuwa wanasubiri Mungu kuikomboa Yerusalemu.

Yusufu, Mariamu na Yesu Warudi Nyumbani

39 Yusufu na Mariamu walipotimiza mambo yote yanayotakiwa katika sheria ya Bwana, walirudi Galilaya, katika mji wao wa Nazareti. 40 Mtoto Yesu aliendelea kukua na kuwa kijana mwenye nguvu na aliyejaa hekima nyingi. Na Mungu alikuwa anambariki.

Yesu Akiwa Mvulana

41 Kila mwaka wazazi wa Yesu walikwenda Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka. 42 Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda kwenye sikukuu kama ilivyokuwa desturi ya Kiyahudi. 43 Sikukuu ilipokwisha, walirudi nyumbani, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kutambua. 44 Walianza kumtafuta kwa jamaa na rafiki zao baada ya kusafiri kutwa nzima, wakidhani kuwa alikuwa pamoja nao katika msafara. 45 Walipomkosa, walirudi Yerusalemu kumtafuta.

46 Ikawa baada ya siku tatu wakamkuta Hekaluni, amekaa katikati ya walimu wa dini, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Na wote waliomsikiliza walishangazwa sana kwa ufahamu wake na majibu yake ya busara. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa pia, ndipo mama yake akamwambia, “Mwanangu, kwa nini umefanya hivi? Mimi na baba yako tulikuwa na wasiwasi sana, na tumekuwa tukikutafuta.”

49 Yesu akawaambia, “Kwa nini mlikuwa mnanitafuta? Mnapaswa kujua kuwa inanilazimu kuwemo nyumbani mwa Baba yangu?” 50 Lakini wao hawakuelewa alichowaambia.

51 Yesu alirudi pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii. Mama yake aliendelea kuyaweka mambo haya yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Footnotes

  1. 2:1 Rumi Au “dola ya ulimwengu ya Rumi”.
  2. 2:1 wahesabiwe na kuorodheshwa Yaani, “Sensa”, lengo hasa ilikuwa waorodheshwe katika kumbukumbu za serikali kwa ajili ya kulipa kodi.
  3. 2:7 hori la kulishia mifugo Sehemu au chombo cha kulishia mifugo. Pia katika mstari wa 12 na 16.
  4. 2:11 Kristo Kwa maana ya kawaida “Kristo”, ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania “Masihi” linalomaanisha “Mpakwa Mafuta”, ambapo katika Agano la Kale linawakilisha sherehe ya kupakwa mafuta (Kuwekwa Wakfu) mfalme mpya. Pia linamaanisha Mfalme Mteule. Tazama Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno. Pia katika mstari wa 26 na katika kitabu chote hiki.
  5. 2:22 baada ya mtoto kuzaliwa Sheria ya Musa iliagiza kuwa ifikapo siku 40 baada mwanamke wa Kiyahudi kuzaa mtoto, yule mtoto anapaswa kutakaswa kwa sherehe maalumu Hekaluni. Tazama Law 12:2-8.
  6. 2:23 wakfu kwa ajili ya Bwana Tazama Kut 13:2,12.
  7. 2:24 hua Hua (au tetere) ni njiwa wa porini, ni wadogo kuliko wale wanaofugwa na huruka kwa mwendo kasi. Imenukuliwa kutoka Law 12:8.