Yesu Alisha Watu Elfu Tano

Baadaye, Yesu alivuka hadi ng’ambo ya pili ya ziwa la Gali laya, ambalo pia huitwa bahari ya Tiberia. Watu wengi walikuwa wakimfuata kwa sababu walikuwa wamemwona akiponya wagonjwa kwa njia za ajabu. Yesu alikwenda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka, ilikuwa imekaribia.

Yesu alipotazama aliona umati mkubwa wa watu wanamfuata. Akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ya kuwalisha watu hawa?” Alisema hivi kumjaribu Filipo maana yeye mwenyewe ali jua atakalofanya.

Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili, hazitoshi kununua mikate ya kuwapatia watu hawa japo kila mtu apate kipande kidogo.”

Mmoja wa wanafunzi wake, aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema, “Kuna mvulana mmoja ana mikate mitano na samaki wawili. Lakini hivi vitafaa nini kwa umati wote huu?”

10 Yesu akasema, “Waketisheni watu chini.” Zilikuwapo nyasi nyingi mahali hapo, kwa hiyo watu wapatao elfu tano wal iweza kukaa chini. 11 Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu, akawagawia wale watu waliokuwa wamekaa. Akawagawia pia na hao samaki wawili, kila mtu kiasi alichotaka. 12 Watu wote wali pokwisha kula kiasi cha kutosha, aliwaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vipande vilivyobaki, kisipotee kipande cho chote.” 13 Basi wakakusanya vipande vya ile mikate mitano, wakajaza vikapu kumi na viwili.

14 Watu walipoona muujiza huu alioufanya Yesu, wakasema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii tuliyekuwa tukimtazamia!”

Read full chapter