Kutoka kwa Mzee. Kwa mama mteule pamoja na watoto wake niwapendao katika kweli. Wala si mimi tu niwapendaye bali wote wanaoifahamu kweli; kwa sababu ya ile kweli ikaayo ndani yetu na ambayo itakuwa nasi hadi milele.

Neema, huruma, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wake zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.

Kweli Na Upendo

Nimefurahi sana kuona kwamba baadhi ya watoto wako wanadumu katika kweli, kama Baba alivyotuamuru. Na sasa, mama mpendwa, sikuandikii amri mpya, bali ile ile ambayo tumekuwa nayo kutoka mwanzo: kwamba tupendane. Na upendo ni huu: kwamba tuishi kwa kuzifuata amri za Mungu. Na kama mlivyosikia tangu mwanzo, amri yake ni kwamba muishi maisha ya upendo.

Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, watu wasiokiri ya kwamba Kristo alikuja kama mwanadamu. Mtu kama huyo ni mdanganyifu na mpinga-Kristo. Jihadharini msije mkapoteza yale mliyoyafanyia kazi, bali mpewe thawabu kamili.

Mtu ye yote anayevuka mpaka wa mafundisho ya Kristo, na kuyaacha, huyo hana Mungu. Na mtu anayedumu katika mafundisho ya Kristo, huyo anaye Baba na Mwana pia. 10 Mtu ye yote akija kwenu bila kuwaletea mafundisho haya, msimkaribishe nyumbani kwenu, wala msimsalimu. 11 Kwa maana mtu anayemsalimu anashiriki kazi zake za uovu.

12 Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sipendi kutumia kara tasi na wino. Badala yake ninatarajia kuwatembelea na kuongea nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu ikamilike.

Salamu kutoka kwa mzee.[a]

Kwa mwanamke[b] aliyechaguliwa na Mungu na kwa wanawe.

Kweli kabisa, ninawapenda ninyi nyote. Na sio mimi peke yangu. Bali wote wanaoifahamu kweli[c] wanawapenda vile vile. Tunawapenda kwa sababu ya kweli, ile kweli iliyomo ndani yetu. Kweli inayoendelea kuwemo ndani yetu milele yote.

Neema, rehema, na amani itakuwa pamoja nasi kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa mwanaye, Yesu Kristo, kwa kadri tuishivyo katika kweli na upendo.

Nilikuwa na furaha sana baada ya kufahamu habari za baadhi ya watoto wako. Nina furaha kuwa wanaifuata njia ya kweli, kama vile baba alivyo tuamuru. Na sasa, mwanamke mwema, nina ombi hili: na tupendane sisi kwa sisi. Hii si amri mpya. Ni amri ile ile tuliyo kuwa nayo tangu mwanzo. Na hii ndiyo maana ya kupenda: kuishi kulingana na amri zake. Na amri ya Mungu ni hii: Kwamba muishi maisha ya upendo. Mliisikia amri hii toka mwanzo.

Walimu wengi wa uongo wamo duniani sasa. Wana kataa kusema Yesu ni Masihi aliyekuja duniani na kufanyika mwanadamu. Kila anayekataa kuikubali kweli hii ni mwalimu wa uongo na adui wa Kristo. Muwe waangalifu! Msiipoteze thawabu tuliyokwisha[d] kuitendea kazi. Mhakikishe mnaipokea thawabu kamili.

Kila mmoja aendelee kuyashika mafundisho aliyefundishwa juu Kristo tu. Yeyote atakayeyabadili mafundisho hayo hana Mungu. Kila anayeendelea kuyafuata mafundisho ya Kristo[e] anao wote Baba na Mwanaye. 10 Msiwakubali wale wanaowaijia lakini hawawaletei mafundisho haya. Msiwakaribishe katika nyumba zenu. Msiwape salamu zenu. 11 Kama mkiwakaribisha na kuwasalimu, mnawasaidia katika kazi zao za uovu.

12 Nina mengi ya kuwaambia. Lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kuwatembelea. Kisha tunaweza kujumuika pamoja na kuzungumza uso kwa uso. Ndipo furaha yetu itakamilika. 13 Watoto wa dada[f] yako aliyechaguliwa na Mungu wamekutumia upendo wao.

Footnotes

  1. 1:1 mzee Huyu huenda alikuwa ni Mtume Yohana. “Mzee” ina maana ya mtu aliye mtu mzima au kiongozi maalumu katika kanisa (kama vile katika Tit 1:5).
  2. 1:1 mwanamke Inaweza kumaanisha mama. Au, katika barua hii, yaweza kumaanisha kanisa. Kama ni kanisa, basi watoto wake, wanaweza kuwa ndiyo wanakanisa. Pia katika mstari wa 5.
  3. 1:1 kweli Kweli au “habari njema” za Yesu Kristo zinazo waunganisha waamini wote pamoja.
  4. 1:8 tuliyokwisha Nakala zingine za Kiyunani zina “mliyoyatenda”.
  5. 1:9 mafundisho ya Kristo Hii ilihusu mafundisho juu ya Kristo kama alikuwa mwanadamu na pia Mungu na pia mafundisho ambayo Kristo mwenyewe aliyafundisha.
  6. 1:13 dada Dada wa mwanamke “mwanamke” katika mstari wa 1. Huyu aweza kuwa mwanamke mwingine au kanisa lingine.