Maonyo Ya Mwisho Na Salamu

13 Hii itakuwa ni safari yangu ya tatu kuja kwenu. “Shitaka lo lote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.” Niliwaonya wale waliotenda dhambi na wengine wote, na sasa nawaonya tena nikiwa siko nanyi kama nilivyowaonya wakati nili powatembelea mara ya pili, kwamba nikija tena sitawahurumia. Kwa kuwa mnataka kupata ushahidi kuwa Kristo anazungumza kupi tia kwangu, hiyo itakuwa ushahidi wangu. Yeye si mdhaifu anapow ashughulikia bali ni mwenye nguvu ndani yenu. Kwa maana alisu lubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Hali kadhalika sisi ni wadhaifu ndani yake, lakini kwa nguvu za Mungu tutaishi pamoja naye ili tuweze kuwahudumia.

Jichunguzeni mwone kama mnashika imani yenu. Jipimeni. Je, hamtambui ya kuwa Kristo yuko ndani yenu, au pengine mmeshindwa kufikia kipimo hicho? Natumaini mtagundua ya kuwa sisi hatu kushindwa kufikia kipimo hicho. Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda jambo lo lote ambalo ni kosa; si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaone kana kuwa tumeshindwa. Kwa maana hatuwezi kufanya lo lote kupinga kweli, bali kuithibitisha kweli. Tunafurahi wakati wo wote sisi tunapokuwa wadhaifu na ninyi mkawa wenye nguvu. Tuna choomba ni kwamba mpate kukomaa katika imani. 10 Nawaandikieni haya wakati nikiwa mbali ili nitakapokuja nisiwe na sababu ya kuwa mkali katika kutumia madaraka ambayo Bwana amenipa kuwa jenga, na sio kuwagandamiza. 11 Hatimaye ndugu zangu, kwaherini. Sahihisheni mwenendo wenu, pokeeni ushauri wangu; sikilizaneni ninyi kwa ninyi; kaeni kwa amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 12 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. 13 Watakatifu wote wanawasalimu.

Maonyo ya Mwisho na Salamu

13 Hii itakuwa ni safari yangu ya tatu kuwatembelea. Na mkumbuke, “Kila shitaka ni lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu wanaosema kuwa jambo hilo ni la kweli.”(A) Nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili, nilitoa maonyo kwa wale waliotenda dhambi. Sipo hapo sasa, ila natoa onyo lingine kwao na kwa yeyote aliyetenda dhambi: Nitakapo kuja tena kwenu, nitawaadhibu walio miongoni mwenu ambao bado wanatenda dhambi. Mnatafuta uthibitisho kuwa Kristo anasema kupitia mimi. Uthibitisho wangu ni kuwa yeye si dhaifu kuwashughulikia bali yeye anaonesha uweza wake miongoni mwenu. Ni kweli kuwa Kristo alikuwa dhaifu alipouawa msalabani, lakini yu hai kwa nguvu za Mungu. Ni kweli pia kwamba twashiriki unyonge wake, lakini kwa kushughulika nanyi, tutakuwa hai pamoja nae katika uweza wa Mungu.

Jiangalieni ninyi wenyewe. Mjipime ninyi wenyewe mkaone kama mngali mnaishi katika imani. Hamtambui kuwa Kristo Yesu yu ndani yenu? La mkishindwa jaribio hilo; ikiwa hamtakuwa mkiishi katika imani; basi Kristo hayumo ndani yenu. Lakini ni matumaini yangu kuwa mtagundua ya kwamba hatujashindwa jaribio hilo. Tunawaombea kwa Mungu msifanye lolote lililo baya. Tunachojali hapa si kwamba watu waone kuwa tumeshinda jaribio katika ile kazi tuliyofanya pamoja nanyi. Tunachokitaka zaidi ni ninyi kufanya lililo jema, hata ikiwa itaonekana kuwa tumeshindwa jaribio. Hatuwezi kufanya lolote lililo kinyume na kweli bali lile linalodumisha kweli. Tunafuraha kuonekana tu wadhaifu ikiwa ninyi mko imara. Na hili ndilo tunaloomba, kwamba maisha yenu yatakamilishwa katika haki tena. 10 Ninaandika haya kabla sijaja kwa kuwa niko mbali nanyi ili nijapo nisilazimike kutumia mamlaka kuwaadhibu. Bwana alinipa mamlaka hayo kuwaimarisha, na sio kuwaharibu.

11 Sasa, wapendwa dada zangu na kaka zangu mjazwe furaha. Jitahidini kutengeneza njia zenu, fanyeni nilichowaomba kufanya. Mpatane kila mmoja na mwenziwe, na ishini katika amani. Ndipo Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.

12 Msalimiane kwa salamu maalum ya watu wa Mungu.[a] Watakatifu wote wa Mungu hapa nao wanawasalimu.

13 Ninawaombea ili ninyi nyote mfurahie neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na Ushirika[b] wa Roho Mtakatifu.

Footnotes

  1. 13:12 salamu maalum ya watu wa Mungu Kwa maana ya kawaida, “busu takatifu”.
  2. 13:13 Ushirika Hii inaweza kumaanisha kushirikiana katika Roho Mtakatifu au kupenda kushirikishana mambo na kukaa katika umoja wa waamini kunakofanywa na Roho Mtakatifu.