Askari Mwaminifu Wa Kristo Yesu

Basi, wewe mwanangu, uwe imara katika neema iliyomo ndani ya Kristo Yesu. Na mambo ambayo ulinisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu ambao wataweza kuwa fundisha watu wengine pia. Vumilia mateso pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu. Hakuna askari ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kiraia kwa sababu nia yake ni kumrid hisha yule aliyemwandika kuwa askari. Hali kadhalika mwanar iadha hawezi kupewa tuzo kama hakufuata masharti. Mkulima mwe nye bidii ndiye anayestahili kupata fungu la kwanza la mavuno. Yatafakari haya ninayokuambia, kwa maana Mungu atakupa ufahamu katika mambo yote.

Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, aliyez aliwa katika ukoo wa Daudi. Hii ndio Injili yangu ninayoihubiri. Nami ninateseka kwa sababu ya Injili hii nikivaa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu halikufungwa minyororo. 10 Kwa hiyo ninavumilia taabu zote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi na wao pia wapokee wokovu uliomo ndani ya Kristo Yesu pamoja na utukufu wake wa milele.

11 Neno hili ni kweli kabisa: kwamba kama tumekufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia. 12 Kama tukivumilia, tutatawala pamoja naye pia; kama tukimkana, naye pia atatukana. 13 Tusipo kuwa waaminifu, yeye huendelea kuwa mwaminifu kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.

Mfanyakazi Mwenye Kibali Mbele Za Mungu

14 Wakumbushe mambo haya na uwaamuru mbele za Bwana waache kubishana juu ya maneno. Hii haiwasaidii cho chote bali huwaanga miza wanaowasikiliza. 15 Jitahidi kujidhihirisha mbele za Mungu kama mtu aliyepata kibali chake, mfanyakazi asiyekuwa na sababu yo yote ya kuona aibu, ambaye hulitumia neno la kweli kwa usa hihi. 16 Jiepushe na maneno ya kipuuzi, yasiyo ya kimungu, kwa maana hayo huwavuta watu mbali na Mungu zaidi na zaidi. 17 Mafundisho yao yataendelea kuenea kama donda ndugu. Kati yao wamo Himenayo na Fileto 18 ambao wametanga tanga na kuiacha kweli wakisema kwamba ufufuo umekwishapita. Wanapotosha imani ya baadhi ya watu. 19 Lakini msingi thabiti wa Mungu umesimama imara ukiwa na muhuri wenye maneno haya: “Bwana anawajua walio wake,” na tena, “Kila anayelitaja jina la Bwana aache uovu.”

20 Katika nyumba ya kifahari kuna vyombo vya dhahabu na fedha na pia vimo vyombo vya mbao na vya udongo. Baadhi ya vyombo ni vya heshima lakini vingine sio. 21 Kama mtu akijitakasa na kujitenga na visivyo vya heshima atakuwa chombo cha kutumika kwa shughuli za kifahari; chombo kilichotakaswa kimfaacho Bwana wa nyumba, ambacho ni tayari kwa matumizi yote yaliyo mema. 22 Basi, kimbia tamaa za ujana, na utafute kupata haki, imani, upendo na amani pamoja na wote wamwitao Bwana kwa moyo safi.

23 Usijishughulishe na mabishano yasiyo na maana na ya kipumbavu kwa kuwa unajua ya kwamba hayo huleta ugomvi. 24 Na tena mtumishi wa Bwana hapaswi kuwa mgomvi. Anapaswa kuwa mpole kwa kila mtu na mwalimu mwenye uwezo, na mvumilivu. 25 Anapaswa kuwaonya wale wanaompinga kwa upole, kwa matumaini kwamba Mungu anaweza kuwajalia watubu na kuifahamu kweli; 26 fahamu zao ziwarudie tena, watoke katika mtego wa shetani ambaye amewafunga wafanye kama apendavyo.

Askari Mwaminifu wa Kristo Yesu

Kwako wewe mwanangu, uwe hodari kwa njia ya neema inayopatikana kwa Kristo Yesu. Yachukue mambo uliyoyasikia kwangu mbele za mashahidi wengi, na yakabidhi kwa watu waaminifu ambao watakuwa na uwezo wa kuwafundisha wengine pia. Kama askari mwaminifu wa Kristo Yesu, jiunge nami katika mateso. Hakuna hata mmoja anayefanya kazi kama askari kisha akajishughulisha pia na mambo ya kiraia. Hii ni wa sababu anataka kumfurahisha kamanda wake. Na kama kuna mtu anayeshiriki katika mashindano ya riadha, hawezi kushinda taji endapo hatashindana kwa kufuata sheria. Mkulima mwenye juhudi anastahili kuwa wa kwanza kufurahia sehemu ya mavuno yake. Nakutaka wewe kuyafikiri ninayokuambia na Bwana atakupa uwezo wa kuyaelewa mambo haya yote.

Endelea kumkumbuka Yesu Kristo, aliyefufuka kutoka kwa wafu, na ni kutoka ukoo wa Daudi. Na huu ndiyo Habari Njema ninayoihubiri. Kwa sababu ya Habari Njema ninateseka, hadi hatua ya kufungwa kwa minyororo kama mhalifu. Lakini ujumbe wa Mungu haujafungwa. 10 Kwa hiyo nayavumilia yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili na wao waweze kuufikia wokovu unaopatikana katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.

11 Na hapa kuna usemi wa kuaminiwa:

Kama tumekufa pamoja naye,
    tutaweza kuishi naye pia.
12 Kama tutastahimili, tutaweza pia kumiliki pamoja naye.
    Kama tutamkana yeye, naye atatukana sisi.
13 Kama hatutakuwa waaminifu,
    yeye anabaki kuwa mwaminifu,
    kwa sababu hawezi kujikana mwenyewe.

Mtendakazi Ampendezaye Mungu

14 Endelea kuwakumbusha watu juu ya mambo haya. Waonye kwa mamlaka mbele za Mungu wasipigane juu ya maneno. Mapigano hayo hayana mambo mazuri, bali huwaharibu wanaoyasikiliza. 15 Jitahidi kujionesha mwenyewe kuwa umekubaliwa na Mungu, kama mtumishi asiye na kitu cho chote cha kumfadhaisha na anayeufanyia kazi ujumbe wa kweli ya Mungu katika njia sahihi.

16 Bali uyaepuke majadiliano ya kijinga ya kidunia, ambayo huwapeleka watu mbali na Mungu, 17 na mafundisho ya wale wanaoyachukua mafundisho hayo wanaenea kama saratani mwilini. Miongoni mwao wamo Himenayo na Fileto, 18 aliyeiasi na kuikosa kweli. Wanasema kuwa ufufuo kutoka kwa wafu kwa watu wote umekwisha kutokea, na wanageuza imani za watu wengine.

19 Hata hivyo, msingi ulio imara ambao Mungu aliuweka unasimama imara, na maneno haya yameandikwa juu yake: “Bwana anawajua wale walio wake,”(A) na “Kila anayesema kuwa ni wa Bwana aweze kuuacha ubaya.”

20 Ndani ya nyumba kubwa hakuna vyombo vya dhahabu na fedha pekee, bali hata vya udongo na mbao. Na vingine ni vya kutumika kwa matukio maalumu, na vingine ni kwa matumizi ya kawaida. 21 Hivyo mtu akitakaswa kutoka maovu yote, atakuwa mtakatifu na chombo maalumu cha kutumiwa na Bwana kilicho tayari kwa kila kazi njema.

22 Bali uzikimbie tamaa za ujana na kuyatafuta maisha ya haki, imani, upendo na amani, pamoja na wote wanaomwita Bwana kwa mioyo safi. 23 Nyakati zote ujiepushe na mabishano ya kijinga, kwa sababu unajua kuwa huleta mabishano makubwa. 24 Kwani mtumwa wa Bwana hapaswi kubishana, bali kuwa mkarimu kwa watu wote, mwenye ujuzi katika kufundisha na asiye mtukanaji. 25 Anapaswa kuwaelekeza wapinzani wake kwa upole katika tumaini kwamba Mungu anaweza kuwasaidia hao kutubu na kuujua ukweli, 26 na ili waweze kurudi katika fahamu zao na kuuepuka mtego wa adui, ambako wameshikiliwa kama mateka na Ibilisi na wamelazimishwa kuyafanya mapenzi yake.