Imani Ndani Ya Kristo

Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo, ni mtoto wa Mungu; na kila ampendaye mzazi wa mtoto, humpenda pia na mtoto wa mzazi huyo. Na hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu: tukimpenda Mungu na kuzitii amri zake. Kwa maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na amri zake hazitule mei. Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu ameushinda ulimwengu. Nasi tumeushinda ulimwengu kwa imani yetu. Ni nani basi aushin daye ulimwengu isipokuwa yeye aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

Mashahidi Wa Yesu Kristo

Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji na damu; si kwa maji peke yake, bali kwa maji na damu. Roho mwenyewe ndiye anayemshu hudia kwa maana Roho ni kweli. Wapo mashahidi watatu: Roho, maji na damu; na hawa watatu wanakubaliana. Kama tunakubali ushahidi wa wanadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; kwa sababu huu ni ushahidi wa Mungu ambao ameutoa kumhusu Mwanae. 10 Mtu anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushuhuda huo ndani yake. Mtu asiyemwamini Mungu, amemfanya Mungu kuwa ni mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda alioutoa Mungu kuhusu Mwanae. 11 Na ushuhuda wenyewe ndio huu: Mungu ametupatia uzima wa milele, na uzima huu umo kwa Mwanae. 12 Aliye naye Mwana anao uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana uzima.

Uzima Wa Milele

13 Ninawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu kusudi mjue kuwa mnao uzima wa milele. 14 Na sisi tunao ujasiri huu mbele za Mungu kwamba, tukiomba cho chote sawa na mapenzi yake, atatusikia. 15 Na tukijua kwamba anatusikia kwa lo lote tunaloomba basi tuna hakika kwamba tumekwisha pata yale tuliyomwomba.

Umuhimu Wa Kuonyana

16 Mtu akimwona ndugu yake akitenda dhambi isiyompeleka kwe nye kifo, amwombee kwa Mungu, naye Mungu atampatia uzima. Ninasema kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi ambayo humpeleka mtu kwenye kifo. Sisemi kwamba ana paswa kuomba kuhusu hiyo. 17 Matendo yote yasiyo ya haki ni dhambi na kuna dhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo.

18 Tunafahamu kuwa kila aliyezaliwa na Mungu haendelei kutenda dhambi; kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda na yule mwovu hawezi kumgusa. 19 Tunajua kuwa sisi ni wa Mungu na kwamba ulim wengu wote unatawaliwa na yule mwovu. 20 Tunajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupa ufahamu ili tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.

Watoto wa Mungu Ushindeni Ulimwengu

Watu wanao amini kuwa Yesu ni Masihi ni wana wa Mungu. Na kila ampendae Baba pia anawapenda watoto wa Baba. Twatambuaje kuwa tunawapenda watoto wa Mungu? Twatambua kwa sababu tunampenda Mungu na tunazitii amri zake. Kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na amri za Mungu si ngumu kwetu, kwa sababu kila ambae ni mwana wa Mungu ana uwezo wa kushinda dhidi ya ulimwengu. Ni imani yetu iliyoshinda vita dhidi ya ulimwengu. Hivyo ni nani anayeushinda ulimwengu? Ni wale tu wanaoamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu.

Mungu alituambia kwa Habari ya Mwanae

Yesu Kristo ndiye aliyekuja. Alikuja kwa maji na damu.[a] Hakuja kwa maji peke yake. Lahasha, Yesu alikuja kwa vyote maji na damu. Na Roho atuambia kuwa hili ni kweli. Roho ndiye Kweli. Kwa hiyo kuna mashahidi watatu wanao tuambia habari za Yesu: Roho, Maji, na Damu. Mashuhuda hawa watatu wanakubaliana.

Tunawaamini watu wanaposema jambo llililo kweli. Lakini kile anachosema Mungu ni muhimu zaidi. Na Hivi ndivyo Mungu alivyotuambia: Alituambia ukweli kuhusu Mwanaye. 10 Kila amwaminiye Mwana wa Mungu anayo kweli ambayo Mungu alituambia. Lakini watu wasiomwamini Mungu wanamfanya Mungu kuwa mwongo, kwa sababu hawaamini kile ambacho Mungu ametueleza kuhusu mwanaye. 11 Hiki ndicho ambacho Mungu alitueleza: Mungu ametupatia uzima wa milele, na uzima huu umo katika wanawake. 12 Yeyote aliye na mwana anao uzima wa milele, lakini asiye na mwana wa mungu hana huo uzima wa milele.

Tunao uzima wa Milele Sasa

13 Ninawaandikia barua hii ninyi mnaomwamini Mwana wa Mungu ili mjue ya kwamba sasa mnao uzima wa milele. 14 Tunaweza kwenda kwa Mungu tukiwa na ujasiri huo. Hii ina maana kuwa tunapomwomba Mungu mambo (na mambo hayo yakakubaliana na matakwa yake kwetu), Mungu huyajali yale tunayosema. 15 Hutusikiliza kila wakati tunapomwomba. Hivyo tunatambua kuwa yeye hutupa kila tunachomwomba.

16 Utakapomwona muumini mwenzio akitenda dhambi (Dhambi isiyomwongoza kwenye mauti), unapaswa kumwombea. Kisha Mungu atampa uzima. Ipo aina ya dhambi inayomwongoza mtu hadi mauti ya milele. Sina maana ya kusema unapaswa kuombea aina hiyo ya dhambi. 17 Daima kutenda yasiyo haki ni dhambi. Lakini ipo dhambi isiyomwongoza mtu katika mauti ya milele.

18 Tunajua kwamba wale waliofanyika watoto wa Mungu hawaendelei kutenda dhambi. Mwana wa Mungu anawahifadhi salama.[b] Yule Mwovu hawezi kuwagusa. 19 Tunajua kwamba sisi ni wa Mungu, Lakini yule Mwovu anautawala ulimwengu wote. 20 Nasi tunajua kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupa uelewa. Hivyo sasa tunaweza kumjua yeye aliye kweli, na tunaishi katika Mungu huyo wa kweli. Nasi tumo ndani ya mwanaye, Yesu Kristo. Yeye ndiye Mungu wa kweli, naye ndiye uzima wa milele. 21 Kwa hiyo, watoto wapendwa, mjiepushe na miungu wa uongo.

Footnotes

  1. 5:6 maji na damu Inaweza kumaanisha Maji ya ubatizo wa Yesu Kristo, na damu aliyo imwaga pale msalabani.
  2. 5:18 Mwana … salama Kwa maana ya kawaida, “Yeye aliye aliyezaliwa kutokana na Mungu hutunzwa” au “anajitunza”.