Upendo Na Utii

Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda dhambi, tunaye mtetezi wetu kwa Baba, yaani Yesu Kristo mwenye haki. Kristo ndiye sadaka iliyotolewa kwa ajili ya dhambi zetu, na wala si dhambi zetu sisi tu, bali pia dhambi za ulimwengu wote.

Na tunaweza kuwa na hakika kwamba tunamjua Kristo ikiwa tunatii amri zake. Mtu ye yote akisema, “Ninamjua’ Lakini mtu ye yote anayetii neno lake, huyo ndiye ambaye upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kwa kweli. Hivi ndivyo tunavy ojua kuwa tumo ndani ya Kristo. Mtu anayesema anadumu ndani ya Kristo anapaswa kuishi kama Yesu Kristo mwenyewe alivyoishi.

Wapendwa, siwaandikii amri mpya bali amri ile ambayo mme kuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilok wisha kusikia. Lakini hata hivyo amri hii ninayowaandikieni ni mpya; ambayo ukweli wake unaonekana kwake na kwenu, kwa sababu giza linatoweka na nuru ya kweli imekwishaanza kuangaza. Mtu anayesema kwamba anaishi nuruni, naye anamchukia ndugu yake, bado yumo gizani. 10 Anayempenda ndugu yake anaishi katika nuru na wala hana kitu cha kumfanya ajikwae. 11 Lakini anayemchukia ndugu yake anaishi gizani na anatembea gizani, wala hajui aen dako, kwa sababu giza limempofusha macho.

Kwa Watoto, Baba Na Vijana

12 Ninawaandikieni ninyi watoto, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. 13 Ninawaandikieni ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliyekuwapo tangu mwanzo. Ninawaandikieni ninyi vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Ninawandikieni ninyi watoto, kwa kuwa mmemjua Baba. 14 Ninawaan dikieni ninyi akina baba, kwa kuwa mmemjua yeye aliyekuwapo tangu mwanzo. Ninawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mna nguvu na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

Msipende Dunia

15 Msiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani. Kama mtu akiipenda dunia, hawezi kumpenda Baba. 16 Maana vitu vyote vil ivyomo duniani, yaani, tamaa za mwili, tamaa ya vitu vinavyoone kana kwa macho, na kiburi kiletwacho na mali, vyote hivi havitoki kwa Baba bali hutoka ulimwenguni. 17 Nayo dunia inapita na tamaa zake zote zinapita, lakini mtu anayetimiza mapenzi ya Mungu huishi milele.

Onyo Kuhusu Adui Wa Kristo

18 Watoto wapendwa, huu ni wakati wa mwisho. Na kama mlivy okwisha kusikia kwamba yule mpinga-Kristo anakuja, hata sasa wapinga-Kristo wengi wamekwisha kuja. Kwa hiyo tunajua kuwa huu ni wakati wa mwisho. 19 Watu hao walitoka kati yetu, lakini hawakuwa wa kundi letu. Kama wangekuwa wa kundi letu, wangeende lea kuishi pamoja nasi; lakini waliondoka ili iwe wazi kuwa hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kundi letu.

20 Lakini ninyi mmemiminiwa Roho Mtakatifu na nyote mnaijua kweli. 21 Siwaandikii hivi kwa kuwa hamuijui kweli bali kwa sababu mnaijua na kwa kuwa hakuna uongo utokao katika kweli. 22 Je, mwongo ni nani? Mwongo ni yule anayekana kwamba Yesu si Kristo. Mtu huyo ndiye mpinga-Kristo, anayemkana Baba na Mwana. 23 Mtu anayemkana Mwana hawezi kumjua Baba; mtu anayemkiri Mwana anamjua na Baba pia.

24 Hakikisheni kwamba ujumbe mliosikia tangu mwanzo unadumu mioyoni mwenu. Ujumbe huo ukikaa mioyoni mwenu, ninyi pia mtadumu ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 25 Na yeye ametuahidi uzima wa milele.

26 Ninawaandikia mambo haya kuhusu wale wanaojaribu kuwapo tosha. 27 Lakini yule Roho Mtakatifu mliyempokea anakaa ndani yenu wala hamhitaji mtu kuwafundisha. Lakini kama vile huyo Roho Mtakatifu anavyowafundisha mambo yote, naye ni wa kweli wala si wa uongo; kama alivyowafundisha, dumuni ndani yake.

Watoto Wa Mungu

28 Na sasa, wanangu, kaeni siku zote ndani yake, kusudi ata kapotokea tuwe na ujasiri na wala tusijitenge naye kwa kuona aibu atakapokuja.

29 Kama mnajua kwamba yeye ni wa haki, basi mnajua kwamba kila atendaye haki amezaliwa naye.

Yesu ni Msaidizi Wetu

Wapendwa wanangu, ninawaandikieni waraka huu ili kwamba msitende dhambi. Ila kama yeyote akitenda dhambi, tunaye Yesu Kristo wa kutusaidia. Yeye daima alitenda haki, kwa hiyo anaweza kututetea mbele za Mungu Baba. Yesu ndiye njia ambapo dhambi zetu zinaondolewa. Naye haziondoi dhambi zetu tu bali anaziondoa dhambi za watu wote.

Kama tukitii mambo ambayo Mungu ametuamuru kuyafanya, tunapata uhakika ya kuwa tunamjua. Kama tukisema kuwa tunamjua Mungu lakini hatuzitii amri zake, tunasema uongo. Kweli haimo ndani mwetu. Lakini tunapotii mafundisho ya Mungu, kwa hakika upendo wake unakamilika ndani yetu. Hivyo ndivyo tunavyojua kuwa tunaishi ndani yake. Kama tukisema kuwa tunaishi ndani ya Mungu, ni lazima tuishi kwa namna ambvyo Yesu aliishi.

Yesu Alituagiza Kuwapenda Wengine

Wapendwa rafiki zangu, siwaandiki ninyi amri mpya. Ni amri ile ile ambayo mmekuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ni fundisho lile lile ambalo mmekwishalisikia. Lakini kile ninachokiandika pia ni amri mpya. Ni kweli; Mnaweza kuiona kweli ndani ya Yesu na ndani yenu ninyi wenyewe. Giza linatoweka, na nuru ya kweli tayari inang'aa.

Mtu anaweza kusema, “Niko nuruni,” lakini ikiwa anamchukia ndugu yeyote katika familia ya Mungu, basi angali bado katika giza. 10 Wao wanaowapenda ndugu wanaishi katika nuru, na hakuna kitu ndani yao cha kuwafanya watende mabaya. 11 Lakini yeyote anayemchukia nduguye wa kike au wa kiume yuko gizani. Anaishi katika giza. Hajui anakoenda, kwa sababu giza limemfanya asiweze kuona.

12 Ninawaandikia, ninyi watoto wapendwa,
    kwa sababu dhambi zenu zimesamehewa kwa njia ya Kristo.
13 Ninawaandikia, ninyi akina baba,
    kwa sababu mnamjua yeye aliyekuwepo tangu mwanzo.
Ninawaandikia, ninyi vijana,
    kwa sababu mmemshinda yule mwovu.
14 Ninawaandikia ninyi watoto,
    kwa sababu mnamjua Baba.
Ninawaandikia ninyi, akina baba,
    kwa sababu mnamfahamu yeye aliyekuwepo tangu mwanzo.
Ninawaandikia ninyi, vijana,
    kwa sababu mna nguvu.
Mafundisho ya Neno la Mungu yimo ndani yenu,
    na mmemshinda yule mwovu.

15 Msiipende dunia hii ya uovu wala mambo yaliyomo ndani yake. Kama mkiipenda dunia, upendo wa baba haumo ndani yenu. 16 Yote yaliyomo katika dunia: yaani, tamaa halisi za kibinadamu, tamaa kwa yale mabaya tunayoyaona, na kiburi cha vitu tulivyonavyo. Lakini hakuna hata mojawapo ya haya litokalo kwa Baba. Yote yanatoka katika dunia. 17 Dunia inapita, na mambo yote ambayo watu wanayataka kutoka katika dunia nayo yanapita. Lakini yeyote atendaye mambo ambayo Mungu anayataka ataishi milele.

Msiwafuate Maadui wa Kristo

18 Wapendwa wanangu, mwisho umekaribia! Mmesikia kuwa adui wa Kristo anakuja. Na sasa maadui wengi wa Kristo tayari wapo hapa. Hivyo tunajua kwamba mwisho umekaribia. 19 Maadui hawa walikuwa miongoni mwetu, lakini walituacha. Hawakuwa wenzetu hasa. Kama wangelikuwa kweli wenzetu, wangebaki pamoja nasi. Lakini walituacha. Hii inaonesha kuwa hakuna hata mmoja wao aliyekuwa kwa hakika mwenzetu.

20 Mnayo karama[a] aliyowapa Yeye Aliye Mtakatifu.[b] Hivyo nyote mnaijua kweli. 21 Mnadhani ninawaandikia waraka huu kwa sababu hamuijui kweli? Hapana! Ninawaandikia kwa sababu mnaijua kweli. Na mnajua kuwa hakuna uongo utokao katika kweli.

22 Ni nani basi aliye mwongo? Ni yeye anayesema kuwa Yesu siyo Kristo. Yeyote anayesema hivyo ni adui wa Kristo. Yeye huyo asiyemwamini Baba wala Mwana. 23 Yeyote asiyemwamini Mwana hana Baba, ila yeye anayemkubali Mwana anaye Baba pia.

24 Mnapaswa kuendelea kuyafuata mafundisho mliyoyasikia tangu mwanzo. Kama mkifanya hivyo, mtakuwa siku zote katika Mwana na katika Baba. 25 Na hili ndilo ambalo Mwana ameliahidi kwetu sisi, uzima wa milele.

26 Ninawaandikia barua hii juu ya wale ambao wanataka kuwapotosha katika njia isiyo sahihi. 27 Kristo aliwapa karama maalumu.[c] Nanyi bado mngali na karama hiyo ndani yenu. Hivyo hamumhitaji yeyote kuwafundisha. Karama aliyowapa inawafundisha juu ya kila jambo. Ni karama ya kweli, si ya uongo. Hivyo endeleeni kuishi katika Kristo, kama karama yake ilivyowafundisha.

28 Ndiyo, wanangu wapendwa, ishini ndani yake. Kama tukifanya hivyo, hatutakuwa na hofu siku kristo atakapo kuja tena. Hatutahitaji kujificha na kuwa na aibu ajapo. 29 Mnajua ya kwamba daima Kristo alifanya yaliyo ya haki. Vivyo hivyo mnajua pia ya kwamba wote watendao haki ni watoto wa Mungu.

Footnotes

  1. 2:20 karama Kwa maana ya kawaida, “upako”. Hili linaweza kumaanisha Roho Mtakatifu. Au Mafundisho au Kweli kama ilivyo katika mstari wa 24. Pia katika mstari wa 27.
  2. 2:20 Mtakatifu Mungu au Kristo.
  3. 2:27 karama maalumu Kwa ufasaha “upako”.