Kuhusu Ndoa

Na sasa kuhusu mambo mliyoniandikia. Ni vizuri mtu asioe. Lakini kwa kuwa dhambi ya zinaa imeenea, kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.

Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe; na hali kadhal ika mke kwa mumewe. Kwa maana mke hatawali mwili wake mwe nyewe, bali mume wake ndiye autawalaye. Vivyo hivyo, mume hata wali mwili wake mwenyewe, bali mkewe ndiye anayeutawala. Msiny imane, isipokuwa kama mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda mfupi ili muwe na nafasi nzuri ya maombi. Lakini baada ya muda huo rudianeni tena shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kushindwa kujizuia. Nasema haya kama ushauri, na si sheria. Ningalipenda wote wawe kama mimi nilivyo. Lakini kila mtu amepewa karama yake kutoka kwa Mungu, mmoja ana karama hii na mwingine ana karama ile.

Na sasa nasema kwa wale wasioolewa na kwa wajane. Ingekuwa vizuri kama wangeendelea kuishi bila kuoa au kuolewa kama mimi. Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe. Ni afadhali kuoa kuliko kuwaka kwa tamaa.

10 Kwa wale waliooana ninayo amri, si amri yangu ila ni ya Bwana. Mke asimwache mumewe. 11 Lakini kama akimwacha, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Na mume asimpe mkewe talaka.

12 Lakini kwa wengine nasema, si Bwana ila ni mimi: kama ndugu ana mke asiyeamini, na huyo mke amekubali kuishi pamoja naye, basi asimpe talaka. 13 Na kama mwanamke mwamini ameolewa na mwanaume asiyeamini, na huyo mwanaume amekubali kuishi naye, basi huyo mwanamke asimpe talaka. 14 Kwa maana huyo mwanaume asiyeamini anatakaswa kwa ajili ya mkewe naye mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa ajili ya mumewe anayeamini. Kama isingalikuwa hivyo watoto wao wangalikuwa si safi, lakini ilivyo sasa wao ni watakatifu. 15 Lakini kama yule asiyeamini akitaka kuachana na mwenzake anayeamini, basi na iwe hivyo. Katika hali hiyo mke au mume ambaye ni mwamini hafungwi. Kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani. 16 Wewe mke, unajuaje kama hutamwokoa mumeo? Wewe mume unajuaje kama hutamwokoa mkeo?

Kuishi Kama Mlivyoitwa

17 Kila mtu aishi maisha aliyopangiwa na Bwana, na ambayo ameitiwa na Mungu. Hii ndio amri ninayotoa kwa makanisa yote.

18 Kama mtu alikuwa ametahiriwa alipoitwa, basi asijaribu kuondoa alama za kutahiriwa kwake. Na kama mtu alikuwa hajatahi riwa alipoitwa, basi, asitafute kutahiriwa. 19 Kwa kuwa kutahi riwa au kutotahiriwa si kitu. Jambo lililo muhimu ni kutii amri za Mungu . 20 Kila mtu abaki katika nafasi ambayo alikuwa nayo alipoitwa kuamini. 21 Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Lakini kama unaweza kuwa huru, utumie nafasi hiyo. 22 Kwa maana aliyeitwa kwa Bwana akiwa mtumwa ni mtu huru wa Bwana. Hali kadhalika mtu aliyekuwa huru alipoitwa ni mtumwa wa Kristo. 23 Mmenunuliwa kwa gharama; msikubali kuwa watumwa wa watu. 24 Kwa hiyo ndugu zangu, kila mmoja wenu akae na Mungu katika nafasi aliyokuwa nayo alipoitwa.

Kwa Hali Ya Sasa, Afadhali Kutokuoa

25 Sasa, kuhusu wale walio bikira. Sina amri yo yote kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa ushauri kama mtu aliyemwaminifu kwa rehema ya Bwana.

26 Kwa sababu ya dhiki iliyopo, nadhani itakuwa vyema mki baki kama mlivyo. 27 Je, umeoa? Basi usitake talaka. Kama hujaoa usitafute mke. 28 Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa hajatenda dhambi. Lakini wanaooa watakabil iana na matatizo mengi katika maisha haya, nami ningependa myaep uke kwa kubaki mlivyo.

29 Nikisema hivyo ndugu zangu, nina maana kwamba muda uliobaki ni mfupi. Tangu sasa waliooa waishi kama hawakuoa; 30 na wana oomboleza kama hawaoombolezi; wenye furaha kama hawana furaha; wanaonunua kama walivyonunua si mali yao; 31 na wanaoshughulika na vitu vya dunia hii, kama hawahusiki navyo. Kwa maana dunia hii kama tunavyoiona sasa inatoweka.

32 Ningependa msiwe na wasiwasi. Mwanamume ambaye hajaoa anajishughulisha na mambo ya Bwana, jinsi ya kumpendeza. 33 Lakini mwanamume aliyeoa anajishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi ya kumfurahisha mke wake. 34 Kwa sababu hiyo, ana vutwa huku na huko. Mwanamke asiyeolewa au msichana bikira anaj ishughulisha na kazi ya Bwana, jinsi ya kuwa mtakatifu kimwili na kiroho. Lakini mwanamke aliyeolewa anajishughulisha na mambo ya dunia, jinsi ya kumfurahisha mume wake. 35 Ninasema haya kwa faida yenu na sio kuwawekea vikwazo. Napenda muishi sawa na kumpa Bwana maisha yenu yote. 36 Kama mtu anafikiri kwamba mwenendo wake kwa mchumba wake si sawa, na hasa kama mchumba wake anaanza kuzeeka, na anaona anawajibika kumuoa, basi afanye anavyoona vyema; waoane, si dhambi. 37 Lakini kama mwanamume ameshaamua moyoni mwake kuto kuoa bila kulazimishwa na mtu; kama anaweza kujitawala kabisa, basi anafanya vyema kutokumuoa mchumba wake. 38 Kwa hiyo mwana mume anayeamua kumuoa mchumba wake anafanya vizuri, lakini yule anayeamua kutokumuoa anafanya vizuri zaidi.

39 Mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mume wake maadamu anaishi. Kama mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, ila iwe katika Bwana. 40 Lakini kwa upande wangu naona kuwa angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo.

Kuhusu Ndoa

Sasa nitazungumza kuhusu mambo yale mliyoniandikia. Mliuliza ikiwa ni bora mwanaume asimguse mwanamke kabisa. Lakini dhambi ya uzinzi ni ya hatari, hivyo kila mwanaume anapaswa kumfurahia mke wake, na kila mwanamke anapaswa kumfurahia mume wake. Mume anapaswa kumtosheleza mkewe, vivyo hivyo mke amtosheleze mume wake. Mke hana mamlaka kabisa juu ya mwili wake, bali mume ana mamlaka juu ya mwili wa mkewe. Mume hana mamlaka kabisa juu ya mwili wake, bali mke ana mamlaka juu ya mwili wa mumewe. Msinyimane miili yenu. Lakini mnaweza kukubaliana kutojamiiana kwa muda ili mtumie muda huo katika maombi. Kisha mkutane tena ili Shetani asiwajaribu kutokana na kushindwa kujizuia tamaa zenu. Ninasema hivi ili kuwaruhusu mtengane kwa muda tu. Lakini hii siyo amri. Mimi ningependa kila mtu angekuwa kama mimi nilivyo. Lakini Mungu amempa kila mtu uwezo tofauti. Huwafanya wengine kuwa hivi na wengine kuwa vile.

Sasa kwa ajili ya wale ambao hawajaoa ama hawajaolewa na kwa ajili ya wajane ninawaambia ya kwamba ni vizuri mkae bila kuoa au kuolewa kama mimi. Lakini ikiwa mtashindwa kudhibiti tamaa zenu, basi mwoe au muolewe. Ni vyema kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa.

10 Na sasa ninawaamuru wale walio katika ndoa. Si amri kutoka kwangu, lakini ndivyo Bwana aliamuru. Mke hapaswi kuondoka kwa mume wake. 11 Lakini ikiwa mke anaondoka, anapaswa kukaa bila kuolewa au arudi kwa mume wake. Na mume hapaswi kumtaliki mke wake.

12 Ushauri nilionao kwa wengine unatoka kwangu. Bwana hajatupa mafundisho mengine kuhusu hili. Ukiwa na mke asiyeamini, usimtaliki ikiwa yuko radhi kuendelea kuishi pamoja nawe. 13 Na kama una mume asiyeamini, usimtaliki ikiwa yuko radhi kuendelea kuishi pamoja nawe. 14 Mume asiyeamini ametengwa kwa ajili ya Bwana kupitia mke wake anayeamini. Na mke asiyeamini ametengwa kwa ajili ya Bwana kupitia mume wake anayeamini. Ikiwa hii si sahihi basi watoto wenu wasingefaa kwa ajili ya kumwabudu Mungu. Lakini sasa wametengwa kwa ajili yake.

15 Lakini mume au mke asiyemwamini akiamua kuondoka katika ndoa. Hili linapotokea, ndugu aliye katika Kristo anakuwa huru. Mungu aliwachagua ili muwe na maisha ya amani. 16 Inawezekana ninyi wake mtawaokoa waume zenu; nanyi waume mtawaokoa wake zenu kwani bado hamjui kitakachotokea baadaye.

Ishini Kama Mlivyokuwa Mungu Alivyowaita

17 Kila mmoja wenu anapaswa kuendelea kuishi katika namna ambayo Bwana Mungu amewapa, kuishi kama mlivyoishi Mungu alipowaita. Ninawaambia watu katika makanisa yote kufuata kanuni hii. 18 Mwanaume asibadili tohara yake ikiwa alikuwa ametahiriwa alipoitwa. Ikiwa hakuwa ametahiriwa alipoitwa, asitahiriwe. 19 Kutahiriwa au kutotahiriwa si muhimu. Kilicho muhimu ni kutii amri za Mungu. 20 Kila mmoja wenu awe katika hali aliyokuwa nayo Mungu alipomwita. 21 Usijisikie vibaya ikiwa ulipochaguliwa na Mungu ulikuwa mtumwa. Lakini ikiwa unaweza kujikomboa, basi fanya hivyo. 22 Kama ulikuwa mtumwa Bwana alipokuita, uko huru sasa katika Bwana. Wewe ni wa Bwana. Vivyo hivyo, kama ulikuwa huru ulipoitwa, wewe ni mtumwa wa Kristo sasa. 23 Mungu alilipa gharama kubwa kwa ajili yako, hivyo usiwe mtumwa kwa mtu yeyote tena. 24 Ndugu zangu, katika maisha yenu mapya pamoja na Mungu, kila mmoja wenu anapaswa kuendelea kuwa katika hali ya tohara kama alivyokuwa Mungu alipowaita.

Maswali Kuhusu Kuoa au Kuolewa

25 Sasa nitaandika kuhusu suala jingine mliloniandikia mkiuliza kuhusu watu ambao hawajaoa au kuolewa.[a] Sina amri kutoka kwa Bwana kuhusu hili, lakini haya ni maoni yangu. Na ninaweza kuaminiwa kwa sababu Bwana amenipa rehema. 26 Huu ni wakati mgumu. Hivyo nadhani ni vyema mtu akikaa kama alivyo. 27 Ikiwa umefungwa kwa mke, usijaribu kufunguliwa. Ikiwa hujaoa, usijaribu kuoa. 28 Lakini si dhambi ukiamua kuoa. Lakini waliooa watapata dhiki katika maisha haya, nami ninataka msiipitie dhiki hiyo.

29 Kaka zangu nina maana ya kuwa muda uliosalia ni mchache, wale waliooa waishi kama vile hawajaoa.[b] 30 Wale wanaolia wawe kama wasiolia, wenye furaha wawe kama hawana furaha na wale wanaonunua vitu wawe kama hawavimiliki vitu hivyo. 31 Vitumieni vitu vya ulimwengu pasipo kuviruhusu viwe vya muhimu kwenu. Hivi ndivyo mnapaswa kuishi, kwa sababu ulimwengu huu kwa namna ulivyo sasa, unapita.

32 Nataka msisumbuke. Mwanaume ambaye hajaoa hujishughulisha na kazi ya Bwana naye hujitahidi kumpendeza Bwana. 33 Lakini mwanaume aliyeoa hujishughulisha na mambo ya ulimwengu, ili ampendeze mke wake. 34 Ni lazima afikirie mambo mawili; kumpendeza mke wake na kumpendeza Bwana. Mwanamke ambaye hajaolewa au msichana ambaye hajawahi kuolewa hujishughulisha na kazi ya Bwana. Hutaka kuutoa mwili na roho yake kikamilifu kwa Bwana. Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya ulimwengu ili ampendeze mume wake. 35 Ninasema hili ili niwasaidie. Si kuwawekea vikwazo, lakini ninataka mwishi katika njia sahihi. Na ninataka mjitoe kikamilifu kwa Bwana pasipo kuchukuliwa katika mambo mengine.

36 Mwanaume anaweza kudhani kuwa hamtendei haki mchumba wake. Mchumba wake huyo anaweza kuwa ameshapita umri mzuri wa kuolewa.[c] Hivyo mwanaume anaweza kujisikia kuwa anapaswa kumwoa mchumba wake huyo. Basi na afanye anachotaka. Si dhambi kwao wakioana. 37 Lakini mwanaume mwingine anaweza kuwa na uhakika akilini mwake ya kuwa hakuna haja ya ndoa, hivyo yuko huru kufanya anachotaka. Ikiwa ameamua moyoni mwake kutomwoa mchumba wake, anafanya jambo sahihi. 38 Hivyo mwanaume anayemwoa mchumba wake anafanya jambo jema, na mwanaume asiyeoa anafanya vyema zaidi.

39 Mwanamke anapaswa kuishi na mume wake kipindi chote mumewe anapokuwa hai. Lakini mume akifa, mwanamke anakuwa huru kuolewa na mwanaume yeyote. Lakini mwanaume huyo lazima awe yule wa Bwana. 40 Ikiwa atabaki kuwa mjane, atakuwa na furaha sana. Haya ni maoni yangu, na ninaamini yanatoka kwa Roho wa Mungu.

Footnotes

  1. 7:25 ambao hawajaoa au kuolewa Kwa maana ya kawaida, “Mabikra au wanawali”.
  2. 7:29 wale waliooa waishi … hawajaoa Lugha ya Paulo ni ya mfano. Huenda ana maana ya kuwa waamini wayaone mahusiano yao katika maisha ya sasa kama ya muda tu na hivyo yana kikomo na hayadumu. Hivyo wasishikamane sana na mali na mahusiano ya sasa.
  3. 7:36 Mchumba wake … wa kuolewa Au “Mchumba wa kiume anaweza akashindwa kutawala tamaa zake.”