Mafundisho Kutoka Historia Ya Wayahudi

10 Nataka mkumbuke ndugu zangu, kwamba baba zetu wote wali kuwa wakiongozwa na wingu, na wote walipita katikati ya bahari ya Shamu. Wote walibatizwa kama wafuasi wa Musa katika lile wingu na ndani ya ile bahari. Wote walikula kile chakula cha kiroho, na wote walikunywa kile kinywaji cha kiroho. Kwa maana waliku nywa kutoka katika ule mwamba wa kiroho uliofuatana nao; na mwamba huo ulikuwa ni Kristo. Hata hivyo Mungu hakupendezwa na wengi wao, kwa hiyo maiti zao zilitapakaa jangwani.

Basi mambo haya ni onyo kwetu, tusitamani uovu kama wao walivyofanya. Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyofa nya. Kama Maandiko yasemavyo, “Watu walikaa chini wakala na kunywa, kisha wakainuka kucheza.” Wala tusifanye uasherati kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu elfu ishirini na tatu kwa siku moja. Pia tusimjaribu Bwana, kama wengine walivyofa nya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10 Msilalamike, kama wengine walivyofanya, wakaangamizwa na malaika wa kifo.

11 Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wen gine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia.

12 Kwa hiyo mtu anayejidhania kwamba anasimama, awe na tahadhari asije akaanguka. 13 Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; hata- ruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu. Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.

14 Kwa hiyo rafiki zangu, msishiriki katika ibada za sanamu. 15 Nasema nanyi kama na watu wenye ufahamu. Amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo. 16 Je? Kikombe cha baraka ambacho tuna kibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Na mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa kuna mkate mmoja, sisi tulio wengi, tu mwili mmoja, kwa kuwa tunashiriki mkate mmoja. 18 Fikirini kuhusu Waisraeli, je, Wanaokula kilichotolewa sadaka hawashiriki katika madhabahu? 19 Je, nikisema hivyo nina taka kusema kwamba sadaka iliyotolewa kwa sanamu au kwamba sanamu ina maana yo yote? 20 La, sivyo. Lakini sadaka inayotolewa kwa sanamu inatolewa kwa mashetani, na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi muwe na ushirika na mashetani. 21 Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na kunywa katika kikombe cha mashetani pia. Hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya mashe tani. 22 Je, tunataka kujaribu kumfanya Bwana awe na wivu? Je, sisi tuna nguvu kuliko yeye?

Uhuru Wa Mwamini

23 Vitu vyote vinaruhusiwa, lakini si vitu vyote vina faida. ‘Vitu vyote ni halali,’ lakini si vyote vinajenga. 24 Mtu asita fute yale yanayomfaa yeye peke yake, bali atafute yale yanayomfaa jirani yake.

25 Kuleni cho chote kinachouzwa katika masoko ya nyama bila kuuliza maswali kuhusu dhamiri. 26 Kwa maana, ‘Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.’ 27 Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kitakachokuwa mezani bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri. 28 Lakini kama ukiam biwa, “Hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu,” basi kwa ajili ya huyo aliyekuambia juu ya hicho chakula, na kwa ajili ya dhamiri, usile. 29 Namaanisha dhamiri ya huyo aliyekuambia, si kwa ajili ya dhamiri yako. Lakini kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 30 Kama nakula kwa shukrani, kwa nini nashutu miwa kwa kile ambacho ninatoa shukrani?

31 Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au ni kunywa, fanyeni mambo yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 32 Msiwe kik wazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki, au kwa kanisa la Mungu; 33 kama mimi ninavyojaribu kumridhisha kila mtu katika kila kitu ninachofanya. Kwa maana sitafuti kujiridhisha mwenyewe bali nata futa faida ya walio wengi, ili waweze kuokolewa.

Tahadhari Kutokana na Yaliyotokea Zamani

10 Ndugu zangu, sitaki mshindwe kutambua umuhimu wa kile kilichowatokea baba zetu waliokuwa na Musa. Walifunikwa na wingu,[a] na walipita katika bahari. Walibatizwa[b] wote katika Musa katika wingu na katika bahari. Wote walikula chakula kilichotolewa na Roho wa Mungu, na wote walikunywa kinywaji kinachotolewa na Roho wa Mungu. Kinywaji walichokunywa kilitoka katika mwamba wa roho uliokuwa pamoja nao, na mwamba huo ni Kristo. Lakini Mungu hakupendezwa na wengi wao, na hivyo waliangamizwa jangwani.

Mambo haya yaliyotokea ni tahadhali kwa ajili yetu. Mifano hii itufanye tuache kutamani maovu kama baadhi yao walivyofanya. Msiabudu sanamu kama ambavyo baadhi yao walifanya. Na kama Maandiko yanavyosema, “Waliketi chini kula na kunywa kisha wakasimama kucheza.”(A) Tusifanye dhambi ya uzinzi kama baadhi yao walivyofanya na watu ishirini na tatu elfu miongoni mwao wakafa. Tusimjaribu Kristo[c] kama vile baadhi yao walivyofanya. Kwa sababu hiyo, waliuawa na nyoka. 10 Na msinung'unike kama baadhi yao walivyofanya na wakauawa na malaika anayeangamiza.

11 Mambo yaliyowapata wale watu ni mifano na yaliandikwa ili kututahadharisha sisi tunaoishi nyakati hizi za mwisho. 12 Hivyo kila anayedhani kuwa yuko imara katika imani yake, basi awe mwangalifu asianguke. 13 Majaribu mliyonayo ni yale yale waliyonayo watu wote. Lakini Mungu ni mwaminifu maana hataacha mjaribiwe kwa kiwango msichoweza kustahimili. Mnapojaribiwa, Mungu atawapa mlango wa kutoka katika jaribu hilo. Ndipo mtaweza kustahimili.

14 Hivyo rafiki zangu wapenzi, zikimbieni ibada za sanamu. 15 Ninyi ni watu wenye akili. Upimeni ukweli wa haya ninayosema sasa. 16 Kikombe cha baraka[d] tunachokitolea shukrani ni ushirika wa sadaka ya damu ya Kristo, sawa? Na mkate ule tunaomega, ni ushirika wa mwili wa Kristo, sawa? 17 Kuna mkate mmoja, nasi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa tunashiriki katika mkate huo mmoja.

18 Na fikirini kuhusu Waisraeli wanavyofanya. Wanapokula sadaka, wanaunganishwa pamoja kwa kugawana kile kilichotolewa kwenye madhabahu. 19 Je, ninataka kuthibitisha kitu gani? Je, ninasema kwamba nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu ni hakika najisi kwa kiasi fulani? Je, ninasema kwamba sanamu ni mungu wa kweli? Hapana. 20 Lakini ninasema kuwa chakula kinapotolewa sadaka kwa sanamu, ni sadaka kwa mashetani, siyo kwa Mungu. Nami sitaki ninyi muungane na hao wengine katika kuyaabudu mashetani. 21 Hamwezi kukinywea kikombe cha Bwana na kisha mkakinywea kiombe kinachotukuza mashetani. Hamwezi kushiriki kula chakula na kunywa pamoja kwenye meza ya Bwana kisha mkaenda kushiriki kula chakula na kunywa pamoja kwenye meza inayotukuza mashetani. 22 Kufanya hivyo kunamtia wivu Bwana.[e] Je, mnafikiri tunaweza kujaribu kumfanya Bwana apate wivu? Mnadhani tuna nguvu kuliko yeye?

Utumieni Uhuru Wenu Kumtukuza Mungu

23 Mnasema “Vitu vyote vimeruhusiwa.” Lakini si vitu vyote vinafaa. “Vitu vyote vimeruhusiwa.” Lakini vitu vingine havisaidii katika kuliimarisha kanisa. 24 Jitahidi kuwafanyia mema wengine badala ya kufanya mema kwa ajili yako wewe wenyewe.

25 Kuleni chakula chochote kinachouzwa sokoni. Msiulize maswali ili kutafuta kujua kama ni sahihi ama la kwako kukila. 26 Mnaweza kula chakula hicho, “Kwa sababu dunia na kila kitu kilichomo ndani yake ni vya Bwana.”(B)

27 Asiye mwamini anaweza kuwaalika kula chakula. Ikiwa mtakwenda, basi mle chochote kitakachowekwa mbele yenu. Msiulize ulize maswali. 28 Lakini mtu akiwaambia, “Chakula hicho kilitolewa sadaka katika hekalu la miungu,” basi msile. Kwa sababu kinaweza kumwathiri mtu na uhusiano wake na Mungu. 29 Na hapa sizungumzii kuhusu uhusiano wenu na Mungu, bali uhusiano wa mtu yule aliyewaambia na Mungu. Kwa nini uhuru wangu mwenyewe uhukumiwe na mawazo ya mtu mwingine? 30 Ikiwa mimi nitakula chakula nikiwa na shukrani, kwa nini basi nisikosolewa kwa sababu ya kitu ambacho kwa hicho ninamshukuru Mungu?

31 Ninachosema ni kwamba: ukila, au ukinywa, au ukifanya jambo lolote, lifanye kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 32 Kamwe usifanye jambo lolote litakalowafanya watu wengine kutenda mabaya, iwe ni Wayahudi, wasio Wayahudi au mtu yeyote katika kanisa la Mungu. 33 Ninafanya vivyo hivyo. Ninajitahidi kwa njia yeyote ile kumpendeza kila mtu. Mimi sijaribu kutenda yaliyo mema kwangu. Ninajaribu kutenda yale yaliyo na manufaa kwa watu wengine ili waweze kuokoka.

Footnotes

  1. 10:1 wingu Wingu lililowaongoza na kuwalinda watu wa Israeli katika safari yao kutoka Misri, wakavuka Bahari ya Shamu, na wakiwa jangwani. Tazama Kut 13:20-22; 14:19-20.
  2. 10:2 Walibatizwa Tazama Batiza katika Orodha ya Maneno. Hapa, Paulo anamaanisha kuwa kilichofanyika kwa Wayahudi walipokuwa na Musa kinaweza kulinganishwa na ubatizo wa waamini katika Kristo.
  3. 10:9 Kristo Nakala zingine za Kiyunani zimeongeza, “Bwana”.
  4. 10:16 Kikombe cha baraka Kikombe cha divai ambacho waamini katika Kristo humshukuru Mungu katika Mlo wa Bwana (Meza ya Bwana au sakramenti).
  5. 10:22 kunamtia wivu Bwana Tazama Kum 32:16-17.