Yesu Ajitambulisha Kwa Wanafunzi Saba

21 Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi: Simoni Petro, Tomaso aitwaye Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. Simoni Petro aka waambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini usiku ule hawakupata cho chote. Kulipopambazuka, Yesu alisimama ufukoni, lakini wale wana funzi hawakumtambua. Yesu akawaambia, “Wanangu, mmepata samaki wo wote?” Wakamjibu, “La.” Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kulia wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Walivyofa nya hivyo walipata samaki wengi mno hata wakashindwa kuingiza ule wavu uliojaa samaki katika mashua! Kisha yule mwanafunzi ali yependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Petro aliposikia haya akajifunga nguo yake, kwa kuwa alikuwa amevua wakati wakifa nya kazi, akajitosa baharini, akaogelea kuelekea ufukoni. Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja hivi.

Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate. 10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua.” 11 Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 12 Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua hakika ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akachu kua ile mikate na baadaye samaki, akawagawia. 14 Hii ilikuwa ni mara ya tatu Yesu kujitambulisha kwa wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu.

Yesu Amwuliza Petro Kama Anampenda

15 Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana kondoo wangu.” 16 Kwa mara nyingine Yesu akamwul iza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akajibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Akamwam bia, “Chunga kondoo wangu.” 17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwul iza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzu nika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, ‘Unanipenda?’ Akamjibu, “Bwana, wewe unajua kila kitu. Unajua ya kuwa naku penda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu. 18 Nakuambia wazi, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka; lakini ukiwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika nguo na kukupeleka usipotaka kwenda.” 19 Alisema haya ili kumfahamisha Petro jinsi atakavyokufa, na kwa kifo hicho Mungu atukuzwe. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate.” 20 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. Huyu mwanafunzi ndiye yule aliyekaa karibu kabisa na Yesu alipokula naye chakula cha mwisho akauliza, ‘Bwana, ni nani atakayekusaliti?’ 21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?” 22 Yesu akamjibu, “ Ikiwa nataka aishi mpaka nitakapo rudi, inakuhusu nini? Wewe nifuate!” 23 Kwa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea kati ya ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini?”

24 Huyu ndiye yule mwanafunzi ambaye anashuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushu huda wake ni wa kweli.