Ndugu zangu, mkimwona mtu amenaswa katika dhambi fulani, basi ninyi mnaoongozwa na Roho, mrejesheni mtu huyo kwa upole. Lakini mjihadhari, ili na ninyi msije mkajaribiwa. Chukulianeni mizigo yenu; na kwa njia hiyo mtaweza kutimiza sheria ya Kristo. Mtu akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe siyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe. Lakini, kila mtu apime mwenendo wake, ndipo anaweza kuwa na sababu ya kujisifu bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. Kwa maana, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe. Basi, mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake vitu vyote vilivyo vyema.

Msidanganyike, Mungu hadanganywi. Kwa maana kila mtu ata vuna kile alichopanda. Mtu apandaye katika tamaa za mwili, ata vuna kutoka katika mwili uharibifu; lakini yeye apandaye katika Roho, atavuna kutoka katika Roho uzima wa milele. Basi, tusi choke kutenda mema, kwa sababu kama hatukuchoka tutavuna kwa wakati wake. 10 Kwa hiyo basi, kadiri tunavyopata nafasi, tuwa tendee mema watu wote, na hasa wale tunaoshiriki imani moja.

Maonyo Ya Mwisho Na Salamu

11 Tazameni jinsi maandishi ya mkono wangu mwenyewe yalivyo makubwa. 12 Ni wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaowalazimisheni mtahiriwe; na wanafanya hivyo ili wao wenyewe wasije kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo. 13 Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawashiki sheria; lakini wanataka na ninyi mtahiriwe ili wapate kujivunia hiyo alama katika miili yenu. 14 Lakini mimi kamwe sitajivunia kitu cho chote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; kwa maana kwa njia ya msalaba, ulimwengu umesulubiwa kwangu, na mimi nimesulubiwa kwa ulimwengu. 15 Kwa maana, kutahiriwa au kutota hiriwa si kitu kwangu; kitu cha maana ni maisha ya watu kubadili ika kuwa mapya. 16 Amani na rehema ya Mungu ikae na wote wanao fuata kanuni hii, na kwa Israeli ya kweli ya Mungu.

17 Basi, tangu sasa mtu ye yote asije akanisumbua, kwa sababu ninazo alama za Yesu mwilini mwangu.