Mwenendo Wa Mkristo

13 Endeleeni kupendana kama ndugu. Msiache kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivyo watu wengine waliwakaribisha mal aika pasipo kujua. Wakumbukeni waliofungwa gerezani kama vile mmefungwa pamoja nao; pia wakumbukeni wanaoteswa, kwa kuwa na ninyi bado mnaishi katika mwili.

Ndoa iheshimiwe na watu wote, na wenye ndoa wawe waaminifu kwa wenzi wao ; maana Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati.

Maisha yenu yasitawaliwe na tamaa ya kupenda fedha, na mridhike na mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita kupungukia kamwe wala sitakuacha.” Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri, “Bwana ni msaada wangu, sitaogopa kitu, mwanadamu anaweza kunifanya nini?”

Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Tafakarini jinsi walivyoishi na matokeo ya mwenendo wao, mkaige imani yao. Yesu Kristo ni yule yule, jana, leo na hata milele. Msipotoshwe na mafundisho ya kigeni ya namna mbalimbali. Ni vema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, na wala si kwa kutii mash arti kuhusu vyakula, ambavyo havina faida kwa wanaovila. 10 Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema ya kuabudia hawana haki ya kula vitu vilivyowekwa juu yake.

11 Nyama za hao wanyama ambao damu yao huletwa na kuhani mkuu katika Patakatifu pa Patakatifu kama dhabihu ya dhambi, huchomwa nje ya kambi. 12 Kwa hiyo Yesu naye aliteswa nje ya mlango wa mji ili awatakase watu kwa damu yake. 13 Kwa hiyo tum wendee nje ya kambi, tukashiriki aibu aliyostahimili. 14 Maana hapa hatuna mji wa kudumu, bali tunautafuta ule mji ujao.

15 Basi, kwa njia ya Yesu, tuendelee kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani, matunda ya midomo ya watu wanaokiri jina lake. 16 Msiache kutenda mema na kushirikiana mlivyo navyo, kwa maana sadaka kama hizi ndizo zinazompendeza Mungu.

17 Watiini viongozi wenu na kufanya wanavyowaagiza. Wao wanachunga roho zenu, kama watu ambao watatoa ripoti ya huduma yao. Watiini kusudi wafanye kazi yao kwa furaha, na wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.

18 Tuombeeni, kwa maana tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi na tunapenda kufanya yaliyo sawa daima. 19 Ninawasihi zaidi mniombee ili nirudishwe kwenu upesi zaidi.

Sala

20 Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, 21 awape ninyi kila kitu chema, ili mpate kutimiza mapenzi yake akifanya ndani yenu lile linalopendeza machoni pake, kwa njia ya Yesu Kristo; yeye apewe utukufu milele na milele.

Maneno Ya Mwisho

22 Basi, ndugu zangu, nawasihi mpokee vema maonyo haya, maana nimewaandikia kwa ufupi.

23 Napenda kuwafahamisha kwamba ndugu yetu Timotheo amefun guliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja naye kuwaona.

24 Wasalimuni viongozi wenu wote pamoja na watu wote wa Mungu. Salamu zenu kutoka kwa ndugu wa Italia.