Ushuhuda Wa Paulo Kwa Wayahudi Wa Yerusalemu

22 “Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu.” Waliposikia akisema kwa lugha ya Kiebrania, wakatulia zaidi, naye akasema, “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kili kia, lakini nimekulia hapa Yerusalemu, nikiwa mwanafunzi wa Gamalieli. Nilielimishwa kwa kufuata utaratibu maalumu wa sheria za baba zetu, nikiwa na ari ya kumheshimu Mungu kama ninyi mlivyo siku hii ya leo. Niliwatesa wafuasi wa ‘Njia’ mpaka wakafa. Niliwakamata, waume kwa wake, nikawafunga na kuwaweka gerezani. Kuhani mkuu na baraza zima la wazee ni mashahidi wangu kuhusu jambo hili. Wao ndio walionipa barua za kupeleka kwa ndugu zao huko Dameski. Kwa hiyo nilikwenda kuwakamata wafuasi wa ‘Njia’ niwalete Yerusalemu kama wafungwa ili waadhibiwe. Nilipokuwa nimekaribia kufika Dameski, mnamo muda wa kama saa sita mchana, kulitokea mwanga mkali kutoka mbinguni ukaangaza pande zote kuni zunguka. Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, ‘Sauli! Sauli! Mbona unanitesa?’ Nikajibu, ‘Wewe ni nani Bwana?’ Naye akajibu, ‘Mimi ni Yesu wa Nazareti unayemtesa.’

“Wale watu niliokuwa nikisafiri nao waliona ule mwanga, lakini hawakuelewa ile sauti ya yule aliyekuwa akisema nami. 10 Nikauliza, ‘Nifanye nini Bwana?’ Naye Bwana akaniambia, ‘Inuka uingie Dameski na huko utaambiwa mambo yote uliyopangiwa kufanya.’ 11 Nilikuwa sioni kwa sababu ya ule mwanga mkali kwa hiyo wenzangu wakanishika mkono wakaniongoza na hivyo tukafika Dameski. 12 “Mtu mmoja aitwaye Anania, mtu wa dini, aliyeshika sana sheria zetu, na ambaye aliheshimiwa sana na Wayahudi wote wa Dameski, 13 alinijia akasimama karibu yangu akasema, ‘Ndugu Sauli, pokea tena uwezo wa kuona!’ Na wakati ule ule nikaweza kuona tena, nikamwona Anania. 14 Akasema, ‘Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe ufahamu mapenzi yake, umwone yeye Mwenye Haki na usikie akisema nawe kwa sauti yake mwenyewe. 15 Kwa kuwa utakuwa shahidi wake kwa watu wote uwaambie yote uliyoyaona na kuyasikia. 16 Sasa basi, mbona unakawia? Simama ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako kwa kuliitia jina lake.” ’

Wito Wa Paulo Kuwahubiri Mataifa

17 “Niliporudi Yerusalemu nikawa naomba Hekaluni 18 nilim wona katika ndoto akiniambia ‘Harakisha uondoke Yerusalemu upesi kwa sababu watu hawa hawatakubali ushuhuda wako juu yangu.’ 19 Nikajibu, ‘Bwana, wanajua jinsi nilivyokuwa nikienda katika masinagogi nikawafunga gerezani na kuwapiga wale waliokuamini wewe. 20 Na hata shahidi wako Stefano alipokuwa anauawa mimi nilikuwa nimesimama kando nikikubaliana na kitendo hicho na nikashika mavazi ya wale waliomwua. 21 Akaniambia, ‘Nenda, kwa maana nitakutuma mbali, kwa watu wa mataifa.”

22 Watu walimsikiliza Paulo mpaka hapo; kisha wakapaaza tena sauti zao wakasema, “Mwondosheni duniani! Mtu kama huyu hasta hili kuishi!” 23 Walipoendelea kupiga kelele na kupeperusha nguo zao na kutupa mavumbi juu hewani, 24 yule jemadari akaamuru wale askari wake wamwingize Paulo katika ngome na wamhoji na kum chapa viboko ili aeleze vizuri kwa nini wale Wayahudi walikuwa wanampigia makelele. 25 Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia askari aliyekuwa karibu naye, “Je, ni halali kumpiga raia wa Kirumi kabla hajahu kumiwa kwa kosa lo lote?” 26 Yule askari aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari akamwuliza, “Unajua unalolifanya? Huyu mtu ni raia wa Kirumi.” 27 Kwa hiyo yule jemadari akaja akamwuliza Paulo, “Niambie, wewe ni raia wa Kirumi?” Paulo aka jibu, “Ndio.” 28 Yule jemadari akasema, “Mimi nilinunua uraia wangu kwa fedha nyingi.” Paulo akamjibu, ‘ ‘Lakini mimi ni Mrumi wa kuzaliwa.” 29 Wale wote waliokuwa wamejiandaa kumhoji wakaondoka haraka haraka na yule jemadari akaingiwa na hofu, kwa maana alitambua ya kuwa alikuwa amemfunga raia wa Kirumi kinyume cha sheria.

Paulo Apelekwa Mbele Ya Baraza

30 Kesho yake yule jemadari alimfungua Paulo zile kamba ali zofungwa akaamuru makuhani wakuu na baraza lote likutane. Akamleta Paulo mbele yao ili apate kujua kwa nini Wayahudi wali kuwa wanamshtaki.