Paulo Ahubiri Thesalonike

17 Walisafiri kupitia Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalo nike, ambako kulikuwa na sinagogi la Wayahudi. Paulo aliingia ndani ya sinagogi kama ilivyokuwa kawaida yake, na kwa muda wa majuma matatu akawa akihojiana na Wayahudi akitumia Maandiko kuwaonyesha wazi kwamba ilikuwa ni lazima Kristo ateswe na afu fuke kutoka kwa wafu, akamalizia kwa kusema, “Huyu Yesu ambaye nawaambia habari zake, ndiye Kristo.” Baadhi yao wakakubaliana nao, wakajiunga na Paulo na Sila. Pia umati mkubwa wa Wagiriki waliomcha Mungu, na baadhi ya wanawake viongozi wakaungana nao. Lakini Wayahudi wengi waliwaonea Paulo na Sila wivu, waka chochea baadhi ya wazururaji waovu waanzishe fujo mji mzima; kisha wakashambulia nyumba ya Yasoni ambamo Paulo na Sila wali kuwa wakikaa, ili wawatoe nje. Walipokuta hawako huko, wakawa kamata Yasoni na baadhi ya ndugu waamini wakawaleta mbele ya viongozi wa mji wakipiga kelele: “Hawa watu ambao wamepindua dunia nzima wamefika huku na huyu Yasoni amewakaribisha. Wao wanavunja sheria ya Kaisari kwa kusema eti kuna mfalme mwingine aitwaye Yesu.” Mashtaka haya ya Wayahudi yaliwafadhaisha watu wote pamoja na wale viongozi wa mji. Kwa hiyo wakataka dhamana kutoka kwa Yasoni na waamini wenzake kabla ya kuwaachilia waende zao.

10 Giza lilipoingia, wale ndugu waamini waliwatoa Paulo na Sila wakaondoka kwenda Beroya, na walipowasili wakaingia katika Sinagogi la Wayahudi. 11 Watu wa Beroya walikuwa waungwana zaidi kuliko watu wa Thesalonike. Walisikiliza neno la Mungu kwa hamu wakachambua Maandiko kila siku ili waone kama waliyokuwa wakiam biwa na Paulo ni kweli. 12 Wengi wao waliamini, ikiwa ni pamoja na wanawake maarufu wa Kigiriki na wanaume wengi. 13 Lakini wale Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kuwa Paulo anahubiri neno la Mungu huko Beroya, walikuja wakaanza kuwashawishi watu na kuwa chochea waanzishe vurugu. 14 Na ndugu wa Beroya wakafanya haraka wakamsafirisha Paulo kuelekea bandarini , lakini Sila na Timotheo walibaki Beroya. 15 Wale waliomsindikiza Paulo walienda naye mpaka Athene. Ndipo wakarudi Beroya wakiwa na maagizo kutoka kwa Paulo kwamba, Sila na Timotheo wamfuate upesi iwezekanavyo.

Paulo Ahubiri Huko Athene

16 Paulo alipokuwa akiwangojea wenzake huko Athene alisikit ishwa sana kuona jinsi mji ulivyojaa miungu ya sanamu. 17 Kwa hiyo akawa akienda katika sinagogi kujadiliana na Wayahudi na Wagiriki waliomcha Mungu na katika mahali pa soko ambako aliongea na watu aliokutana nao. 18 Huko sokoni alikutana na vikundi viwili vya wanafalsafa waitwao Waepikureo na Wastoiko. Baadhi yao wakamdhihaki wakisema, “Huyu mpayukaji asiyejua kitu anajaribu kusema nini?” Wengine wakasema, “Anaelekea kuwa mhubiri wa miungu wageni.” Walisema hivi kwa sababu Paulo alikuwa akihubiri juu ya Yesu na ufufuo. 19 Wakamkamata wakampeleka kwenye baraza la Areopago wakamwambia, “Tungependa kufahamu haya mafundisho mapya unayotangaza. 20 Mambo tunayosikia kuwa unafundisha ni mageni kwetu nasi tungependa kuelewa maana yake.” 21 Waathene na hata wageni walikuwa na tabia ya kutumia wakati wao wote katika mazungumzo ya mambo yo yote ambayo yanaonekana kuwa mageni au mapya.

Hotuba Ya Paulo Kwenye Areopago

22 Kwa hiyo Paulo alisimama kati kati ya Areopago akasema, “Ndugu wa Athene! Nimeona katika kila jambo kuwa ninyi ni watu wa dini hasa. 23 Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini niliona sehemu nyingi za kuabudia. Niliona pia madhabahu moja iliyoan dikwa, ‘Kwa Mungu asiyejulikana.’ Huyo Mungu mnayemwabudu bila kumfahamu, ndiye ninayemtangaza kwenu. 24 Mungu aliyeumba dunia na vitu vyote vilivyomo, ambaye pia ni Bwana wa mbingu na nchi, haishi katika mahekalu yaliyojengwa na wanadamu. 25 Wala hahu dumiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji cho chote; kwa sababu yeye ndiye anayewapa watu wote uhai na pumzi na kila kitu. 26 Yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu waishi juu ya nchi kutokana na mtu mmoja. Pia amepanga muda wa maisha ya watu wote, akaweka na mipaka ya mahali watakapoishi 27 ili wamtafute Mungu na wamfahamu. Lakini Yeye hayuko mbali nasi kwa maana 28 ‘Tunaishi na kuenenda na kuwa na uhai ndani yake,’ na kama mtunga mashairi wenu alivyosema, ‘Sisi ni uzao wa Mungu.’ 29 Kwa kuwa sisi ni wa uzao wa Mungu hatupaswi kudhani kuwa yeye ni kama sanamu ya dhahabu au fedha au jiwe iliyotengenezwa kwa akili na ufundi wa mwanadamu. 30 Mungu alisamehe ujinga huo wa zamani, lakini sasa anaamuru watu wote watubu, waachane na miungu ya sanamu. 31 Kwa kuwa amepanga siku ambayo atahukumu ulimwengu kwa haki akimtumia mtu aliyemchagua, ambaye amemhakikisha kwa watu wote kwa kumfufua kutoka kwa wafu.” 32 Waathene waliposikia juu ya ufufuo wa wafu, baadhi yao wakamdhihaki; lakini wengine wal isema, “Tutataka kusikia tena juu ya habari hii.” 33 Kwa hiyo Paulo akaondoka. 34 Lakini baadhi ya watu walimfuata Paulo wakaamini. Kati yao alikuwepo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja aliyeitwa Damari na wengine.