Yohana Atuma Wanafunzi Wake Kwa Yesu

11 Yesu alipomaliza kutoa maagizo yake kwa wale wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka pale akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. Basi Yohana Mbatizaji aliposikia akiwa gere zani mambo ambayo Yesu alikuwa akifanya, aliwatuma wanafunzi wake wakamwulize, “Wewe ni yule anayekuja, au tumngojee mwin gine?” Yesu akawajibu, “Nendeni mkamweleze Yohana yale mnayo sikia na kuona: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema. Amebarikiwa mtu ambaye hapotezi imani yake kwangu.”

Wale wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuwaam bia ule umati wa watu kuhusu Yohana Mbatizaji. Akawauliza, “Mli pokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? Kama sivyo, mlikwenda huko kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi maridadi? Lakini wanaovaa nguo maridadi wanakaa katika majumba ya wafalme. Basi kwa nini mlikwenda huko? Kumwona nabii? Naam, nawaambieni yeye ni zaidi ya nabii. 10 Huyo ndiye ambaye anaelezwa katika Maandiko kwamba: ‘ Angalia namtuma mjumbe mbele yako, ambaye atakuandalia njia.’ 11 Nawaambieni kweli kwamba kati ya watu wote waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu zaidi ya Yohana Mbatizaji. Lakini hata hivyo aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni, ni mkuu kuliko Yohana. 12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mungu umekuwa ukishambuliwa vikali; na watu wenye jeuri wanajaribu kuuteka kwa nguvu. 13 Kwa maana manabii wote na sheria walita biri mpaka wakati wa Yohana. 14 Na kama mko tayari kusadiki uta biri wao, basi Yohana ndiye Eliya ambaye kuja kwake kulitabiriwa. 15 Mwenye nia ya kusikia na asikie.

16 “Kizazi hiki nikilinganishe na nini?” Kinafanana na waliokaa masokoni wakiwaita wenzao na kuwaambia, 17 ‘Tuliwapigia filimbi, lakini hamkucheza; tuliwaimbia nyimbo za msiba, lakini hamkuomboleza.’ 18 Kwa maana Yohana Mbatizaji alikuja na akawa hali wala hanywi nao wanasema, ‘Amepagawa na pepo’. 19 Mimi mwana wa Adamu nimekuja nikila na kunywa, nao wanasema, ‘Mta zameni mlafi na mlevi; rafiki wa watoza kodi na wenye dhambi!’ Lakini hekima huthibitishwa kwa matendo yake.”

Ole Kwa Korazini Na Bethsaida

20 Yesu akaanza kuikemea miji ambamo alifanya matendo mengi ya ajabu kwa maana watu wake hawakutubu. 21 “Ole wenu watu wa Korazini! Ole wenu watu wa Bethsaida! Kwa maana kama matendo makuu yaliyofanyika kwenye miji yenu yangelifanyika Tiro na Sidoni, watu wa huko wangelikuwa wametubu tangu zamani na kuvaa magunia na kujipaka majivu, kudhihirisha kujuta kwao. 22 Lakini nawaambia, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Tiro na Sidoni kuliko itakavyokuwa kwenu. 23 Na ninyi watu wa Kapernaumu, mnadhani mtainuliwa hadi juu mbinguni? Mtashushwa hadi kuzimuni. Kwa kuwa kama mambo makuu yaliyofanyika kwenu yangalifanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwapo hadi leo. 24 Lakini nawaam bieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma kuliko itakavyokuwa kwenu.”

Hakuna Amjuaye Baba Ila Mwana

25 Wakati huo Yesu alisema, “Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, na ukawafunulia watoto wachanga. 26 Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. 27 Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: na hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na mtu ye yote ambaye Mwana anapenda kumdhihirisha Baba kwake.”

Yesu Awaita Waliolemewa Na Mizigo

28 “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu; jifunzeni kutoka kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni rahisi, na mzigo wangu ni mwepesi.”