Mafundisho Kutoka Historia Ya Wayahudi

10 Nataka mkumbuke ndugu zangu, kwamba baba zetu wote wali kuwa wakiongozwa na wingu, na wote walipita katikati ya bahari ya Shamu. Wote walibatizwa kama wafuasi wa Musa katika lile wingu na ndani ya ile bahari. Wote walikula kile chakula cha kiroho, na wote walikunywa kile kinywaji cha kiroho. Kwa maana waliku nywa kutoka katika ule mwamba wa kiroho uliofuatana nao; na mwamba huo ulikuwa ni Kristo. Hata hivyo Mungu hakupendezwa na wengi wao, kwa hiyo maiti zao zilitapakaa jangwani.

Basi mambo haya ni onyo kwetu, tusitamani uovu kama wao walivyofanya. Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyofa nya. Kama Maandiko yasemavyo, “Watu walikaa chini wakala na kunywa, kisha wakainuka kucheza.” Wala tusifanye uasherati kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu elfu ishirini na tatu kwa siku moja. Pia tusimjaribu Bwana, kama wengine walivyofa nya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10 Msilalamike, kama wengine walivyofanya, wakaangamizwa na malaika wa kifo.

11 Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wen gine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia.

12 Kwa hiyo mtu anayejidhania kwamba anasimama, awe na tahadhari asije akaanguka. 13 Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; hata- ruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu. Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.

14 Kwa hiyo rafiki zangu, msishiriki katika ibada za sanamu. 15 Nasema nanyi kama na watu wenye ufahamu. Amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo. 16 Je? Kikombe cha baraka ambacho tuna kibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Na mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa kuna mkate mmoja, sisi tulio wengi, tu mwili mmoja, kwa kuwa tunashiriki mkate mmoja. 18 Fikirini kuhusu Waisraeli, je, Wanaokula kilichotolewa sadaka hawashiriki katika madhabahu? 19 Je, nikisema hivyo nina taka kusema kwamba sadaka iliyotolewa kwa sanamu au kwamba sanamu ina maana yo yote? 20 La, sivyo. Lakini sadaka inayotolewa kwa sanamu inatolewa kwa mashetani, na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi muwe na ushirika na mashetani. 21 Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na kunywa katika kikombe cha mashetani pia. Hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya mashe tani. 22 Je, tunataka kujaribu kumfanya Bwana awe na wivu? Je, sisi tuna nguvu kuliko yeye?

Uhuru Wa Mwamini

23 Vitu vyote vinaruhusiwa, lakini si vitu vyote vina faida. ‘Vitu vyote ni halali,’ lakini si vyote vinajenga. 24 Mtu asita fute yale yanayomfaa yeye peke yake, bali atafute yale yanayomfaa jirani yake.

25 Kuleni cho chote kinachouzwa katika masoko ya nyama bila kuuliza maswali kuhusu dhamiri. 26 Kwa maana, ‘Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.’ 27 Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kitakachokuwa mezani bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri. 28 Lakini kama ukiam biwa, “Hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu,” basi kwa ajili ya huyo aliyekuambia juu ya hicho chakula, na kwa ajili ya dhamiri, usile. 29 Namaanisha dhamiri ya huyo aliyekuambia, si kwa ajili ya dhamiri yako. Lakini kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 30 Kama nakula kwa shukrani, kwa nini nashutu miwa kwa kile ambacho ninatoa shukrani?

31 Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au ni kunywa, fanyeni mambo yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 32 Msiwe kik wazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki, au kwa kanisa la Mungu; 33 kama mimi ninavyojaribu kumridhisha kila mtu katika kila kitu ninachofanya. Kwa maana sitafuti kujiridhisha mwenyewe bali nata futa faida ya walio wengi, ili waweze kuokolewa.