Maagizo Kwa Wazee Na Vijana

Ninawasihi wazee waliomo miongoni mwenu, nikiwa mzee mwenzenu na shahidi wa mateso ya Kristo na mshiriki katika utu kufu utakaofunuliwa. Lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, si kwa tamaa ya fedha bali kwa moyo wenu wote. Msijifanye mabwana wakubwa kwa wale mnaowa chunga bali muwe vielelezo kwa kundi hilo. Naye Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa mtapokea taji ya utukufu isiyofifia.

Kadhalika ninyi vijana watiini wazee. Jivikeni unyenyekevu, mnyenyekeane kwa maana, “Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu.” Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu wenye nguvu, ili wakati wake ufaao utakapotimia, awainue.

Mwekeeni yeye fadhaa zenu zote kwa maana yeye hujishughul isha sana na mambo yenu.

Kaeni macho. Kesheni, maana adui yenu Ibilisi, huzunguka- zunguka akinguruma kama simba, akitafuta mtu atakayemmeza. Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkifahamu kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayo hayo. 10 Na mkisha kuteseka kitambo kidogo, Mungu wa neema yote ambaye amewaita katika utukufu wake wa milele katika Kristo, yeye mwenyewe atawa kamilisheni na kuwathibitisha na kuwatia nguvu. 11 Uweza ni wake milele na milele. Amina.

Salamu

12 Nimewaandikia kwa kifupi kwa msaada wa Silvano, ndugu ambaye namtambua kuwa mwaminifu, nikiwaonya na kuwashuhudia kuwa hii ndio neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo. 13 Mwenzenu mteule hapa Babiloni anawasalimu pamoja na mwanangu Marko .