Nanyi aliwafanya muwe hai, mlipokuwa mmekufa kiroho kwa ajili ya makosa na dhambi zenu. Hapo zamani mliishi maisha ya jinsi hiyo, mkimtii mfalme wa nguvu za anga, ambaye ndiye ile roho inayowatawala wote wanaomwasi Mungu. Sisi sote pia tuliishi miongoni mwao hapo zamani, tukiridhisha na kutawaliwa na tamaa mbaya za mwili na mawazo. Kwa hiyo sisi pia tulikuwa kwa asili tunastahili ghadhabu ya Mungu kama binadamu wengine wote. Lakini Mungu, ambaye ana huruma nyingi, kutokana na upendo wake mkuu ambao alitupenda nao, japokuwa tulikuwa bado tumekufa kiroho kwa sababu ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu. Mmeokolewa kwa neema. Mungu alitufufua pamoja na Kristo, akatufanya tukae pamoja naye katika makao ya mbinguni tukiwa ndani yake Kristo; ili katika vizazi vijavyo aonyeshe wingi wa neema yake isiyo na mfano, ambayo imedhihirishwa kwa wema wake kwetu sisi tunaoishi ndani ya Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na si kwa sababu ya matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Na kwa sababu hamkuifanyia kazi, mtu ye yote asije akajisifu juu ya wokovu wake. 10 Kwa maana sisi ni matokeo ya kazi ya Mungu tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tuwe na matendo mema ambayo Mungu alikwisha andaa, tuishi katika hayo. 11 Kwa hiyo kumbukeni kwamba ninyi ambao kwa asili ni watu wa mataifa mengine, mnaoitwa ‘wasiotahiriwa’ na wale ‘waliotahi riwa’ kwa kanuni za binadamu; 12 kumbukeni kwamba wakati ule ninyi mlikuwa mmetengwa na Kristo, mkiwa mmefarakana na jumuia ya Israeli na mkiwa wageni kuhusu yale maagano ya ahadi. Mlikuwa hamna matumaini wala Mungu duniani. 13 Lakini kwa kuwa mmeungana na Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali zamani, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya damu ya Kristo. 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu; yeye aliyetufanya tuwe jamii moja, akavunjavunja ule ukuta wa uadui uliotutenga 15 kwa kuifuta ile sheria na amri zake na kan uni zake alipoutoa mwili wake. Alifanya hivyo ili aumbe taifa jipya kutokana na jamii mbili: Wayahudi na watu wa mataifa, na hivyo alete amani. 16 Kwa kutoa mwili wake pale msalabani, ali patanisha jamii zote mbili na Mungu; na kwa njia hiyo akaua ule uadui uliokuwepo kati yao. 17 Alikuja akahubiri amani kwenu ninyi watu wa mataifa ambao mlikuwa mbali na Mungu, na pia kwa wale waliokuwa karibu na Mungu. 18 Kwa maana, kwa kupitia kwake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa, tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja. 19 Kwa hiyo, ninyi sasa siyo wageni tena wala wapita njia, bali mmekuwa raia halisi pamoja na watu wa Mungu na familia ya Mungu. 20 Ninyi mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni. 21 Ndani yake yeye, jengo lote limeunganishwa pamoja na kusimam ishwa kuwa Hekalu takatifu la Mungu. 22 Katika yeye ninyi pia mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambamo Mungu anaishi kwa njia ya Roho wake. Paulo, Mhudumu Kwa Watu Wa Mataifa